Msaada kuhusu kuacha kazi 24 hours notice

hahahahahahahahahahahahahahahahaha
:A S-frusty2::hand:
Mshahara wowote duniani unalipwa mwisho wa mwezi wa kazi, mwisho wa wiki ya kazi au mwisho wa kipindi chochote cha kazi mlichokubaliana, kama vile labda sisi wabeba zege, kazi ya siku ikiisha tu tunashikishwa chetu saa hiyo hiyo, hapo hapo, hutaki hatuondoki, ukikomaa tunamwaga sabuni kwenye zege, tunasepa, hatuna TUCTA wala mikataba sisi!

Sasa kama uki quit kazi unarudisha hela kwa mwajiri, unarudisha hela ipi wakati hakuna mtu duniani analipwa mshahara in advance?

In fact, uki quit kazi ghafla leo, bado kuna hela yako uliyofanyia kazi 'bure,' haijalipwa, toka kipindi cha mshahara wa mwisho hadi leo. Kwa hiyo wewe ndio unadai. Sijui nyinyi mnalipwa lipwaje huko, una quit halafu unaambiwa rudisha mshahara...! Hahahahahahaaa....
 
Yaani wewe ndo umenielewa vizuri hoja yangu. una haki zote za kuweka avatar ya maradona. say mimi tarehe ya mshahara ni 20 kila mwezi, then naacha kazi tarehe 19 kabla hata sijapata mshahara, bado napaswa kurejesha mshahara? upi? au nikipokea tu salary yangu naacha kazi, nirudishe mshahara wa nini ambao nimeufanyia kazi? naona bado pana utata hapo
Jamani jamani!!!!!,

kumlipa mwajiri mshahara wa mwezi mmoja alafu na we ukaacha kazi; lengo ni kumwezesha mwajiri kumtafuta mbadala atakaye ziba nafasi uliyoiacha ghafla ni sawasawa na mwajiri kukufukuza kazi ghafla na kukulipa mshahara wa mwezi mmoja mbele ili ukusaidie kuendelea kuishi wakati ukitafuta kazi nyingine.

Ndo maana tunasema kama mtu anaona ni mzigo basi itolewe NOTISI ya mwezi mmoja ili kila upande ujiandae kupambana na mabadiliko.
 
Hapo kwenye red, what if kazi kaanza February mwaka jana, hadi leo hii march si mwaka tayari au ukishaanza kazi wanahesabu kuanzia January, no matter kazi mtu kaanza mwezi upi? Naomba ufafanuzi pliz!
ukishapita mwaka 1 yaani miezi 12 na wewe ujaenda likizo na wala ktk kipindi hicho ukomba kwenda likizo; Likizo yako inakuwa imekufa. Labda tu uonyeshe kwamba uliomba kwenda likizo na mwajiri kakukatalia.
 
  • Thanks
Reactions: bht
Jamani jamani!!!!!,

kumlipa mwajiri mshahara wa mwezi mmoja alafu na we ukaacha kazi; lengo ni kumwezesha mwajiri kumtafuta mbadala atakaye ziba nafasi uliyoiacha ghafla ni sawasawa na mwajiri kukufukuza kazi ghafla na kukulipa mshahara wa mwezi mmoja mbele ili ukusaidie kuendelea kuishi wakati ukitafuta kazi nyingine.

Ndo maana tunasema kama mtu anaona ni mzigo basi itolewe NOTISI ya mwezi mmoja ili kila upande ujiandae kupambana na mabadiliko.

Anyway mimi bwana kutokana na mazingira nitampa notisi ya siku 14 tu. Nipate tu muda wa kuweka sawa ofisi na kuikabidhi. Kama atakuwa fair nitampa nusu mshahara
 
huwezi kulipwa kwa kuacha kazi na wala hutakiwi kulipa kwa kuacha kazi. Hawa waliotunga sheria hii kimsingi kama walifanya kumpendelea mwajiri vile. Hii sheria ni ya kizamani sana na inafaa kurekebishwa.........mazingira ya sasa siyo
 
41.​
-(1) If a contract of employment can be terminated on notice, theperiod of notice shall not be less than-
(a) seven days, if notice is given in the first month of employment;and(b) after that-(i) 4 days, j f t he e mployee is e employed o n a daily o rweekly basis; or(ii) 28 days, if the employee is employed on a monthlybasis.(2) An agreement may provide for a notice period that is longer thanthat required in subsection (1) provided that, the agreed notice periodis of equal duration for both the employer and the employee.(3) Notice of termination shall be in writing, stating -​
34 No. 6​
(i) the reasons for termination; and(ii) the date on which the notice is given.(4) Notice of termination shall not be given -(a) during any period of leave taken under this Act; or(b) to run. concurrently with any such period of leave.(5) Instead of giving an employee notice of termination, an employer may pay the employee the remuneration that the employee would have received if the employee had worked during the notice period.(6) Where an employee refuses to work during the notice period, anemployer may deduct, from any money due to that employee on termination,the amount that would have been due to the employee if that​
employee had worked during the notice period.

Mkuu uliyekua unauliza kifungu hebu soma hapo juu
Na uproove nilichokuwa nasema
Hiyo ni under the Employment and Labour Relations Act ya mwaka 2004

NA vile vile inategemea na aina ya Mkataba kati ya mwajiri na mwajiriwa unasemaje
 
JF Moderator 1,

Tafadhali acha ku abuse u moderator wako kwenye mijadala ambayo umejiingiza mwenyewe kwa jina la u moderator.

Acha kufuta post zangu na zako na kuniandikia pm za kuni harangue.

Kama umekosea futa kauli zako mwenyewe sio na zangu.

Kama unataka nifungie kabisa maana umekuja na ari mpya ya kufungia watu for no sensible reason, kuna ma moderator veterans hapa kina Mwnkjj wametulia tu na wanamudu discussion bila kufungia watu, we vipi wewe?

Hebu achilia positive unrestricted environment for discussion iweze ku flourish.

Umeshindwa kuonyesha panaposema ukiacha kazi bila notice utawalipa waajiri mshahara.

JF Moderator 1:
Waliotunga sheria hawajui utatoa wapi hiyo pesa au utaitoa wapi kulipa huo mshahara wa mwezi mmoja ni juu yako kujua

Well, hakuna sheria inayosema ukiacha kazi bila notice utawalipa waajiri mshahara!
 
JF Moderator 1

Tunaomba utupe maelezo ya kwa nini wewe ukitumia cheo chako cha u-moderator umefutilia mbali mabandiko ya Anheuser

Tupe kifungu na kanuni ya JF uliyotumia kufanya kitendo chako hicho

Ahsante
 
Mmh ikawaje kwani tena? mara ya mwisho niliposoma hapa sikuona mahali watu 'wanauza chai' wala kutoa lugha isiyofaa bali tu niliona comments ambazo zilikuwa ni kama chachu ya kujadili udhaifu unaoonekana kwenye sheria husika.

hii dhamana ya kutumoderate wakati mwingine mnaitumia sivyo na ndio mnasababisha mkanganyiko kwenye mijadala jamani
 
hii dhamana ya kutumoderate wakati mwingine mnaitumia sivyo na ndio mnasababisha mkanganyiko kwenye mijadala jamani

Madamu tupo kwenye jukwaa la sheria hapa, aje na kifungu au muongozo unaompa hayo mamlaka ya alichokifanya.
 
Jamani jamani!!!!!,

kumlipa mwajiri mshahara wa mwezi mmoja alafu na we ukaacha kazi; lengo ni kumwezesha mwajiri kumtafuta mbadala atakaye ziba nafasi uliyoiacha ghafla ni sawasawa na mwajiri kukufukuza kazi ghafla na kukulipa mshahara wa mwezi mmoja mbele ili ukusaidie kuendelea kuishi wakati ukitafuta kazi nyingine.

Ndo maana tunasema kama mtu anaona ni mzigo basi itolewe NOTISI ya mwezi mmoja ili kila upande ujiandae kupambana
na mabadiliko.

kukatana mshahara wa mwezi in lieu of notice ni busara tu inayotumika maana tayari unapoacha kazi ghafla kuna athari mwajiri anaweza kuzipata; yaweza kuwa ngumu au ikachukua muda kupata replacement yako na akapoteza mapato kwa njia moja au nyengine. (sina hakika kuna kifungu kimeanisha wazi hili ila waajiri wengi kwenye mikataba wanaweka hiyo clause)

Sawa kama vile mwajiriwa akiachishwa kazi ghafla, sheria imekuwa considerate kwamba ulipwe mshahara wa mwezi ili uwe na pakuanzia.
 
JF Moderator 1

Tunaomba utupe maelezo ya kwa nini wewe ukitumia cheo chako cha u-moderator umefutilia mbali mabandiko ya Anheuser

Tupe kifungu na kanuni ya JF uliyotumia kufanya kitendo chako hicho

Ahsante
hee! umetoka lini gerezani? Hivi aliyekufungia ni huyu huyu JF Moderator 1 au? Mlikuwa mnajadili nini yakamshinda? Ukisikia na mimi nimefungiwa usishangae maana huwa sina hulka ya Kitanzania ya kukubaliana kubaliana na kila hogwash inayosemwa lakini kwa wewe nimeshangaa sana maana huwa huna hiana na mtu.

Gaijin, hebu nisaidie tafadhali hapo kwenye hiyo sheria aliyobandika juu page zima, ni wapi paliposemwa uki quit kazi unamlipa mwajiri mshahara, matter of fact ni wapi hapo pameongelea notice ya mfanyakazi kwenda kwa mwajiri at all?

Ndo maana huwa nasema Tanzania hatuna wataalam halafu naonekana nina kiburi, nilishapima sana kufikia kusema hivyo, sasa hawa ma lawyer jamani ndio mnategemea wakawaandikie international contracts za kuuziana technical product kama umeme na Uranium? Please.

kukatana mshahara wa mwezi in lieu of notice ni busara
Wapi sheria imesema hivyo shemeji?
 
Madamu tupo kwenye jukwaa la sheria hapa, aje na kifungu au muongozo unaompa hayo mamlaka
ya alichokifanya.

I believe atafanya hivyo...
ila ujue kuwa hospitali si 'garantii' ya kupata matibabu
 
Wewe muuliza swali ngoja nikuulize........

Wakati ukisaini huo mkataba ulliusoma??? Na kama uliusoma ulisemaje??

tuanzie hapo ndo tuendelee................

Sabaabu kwa mfano mimi niliwahi kusaini mikataba mbalimbali
Mmoja ukasema ukitaka kuacha kazi toa notice ya miezi mitatu au ulipe mshahara wa mwezi mmoja
Na mwajiri akikufukuza kazi anakulipa mshahara wa mwezi mmoja na kama unaarreas za leave anakulipa
Mwingine ukasema mwajiri akikufukuza anakulipa mshahara wa mwezi mmoja
Na ukitaka kuacha kazi utoe notice ya mwezi mmoja ama ulipe mshahara wa mwezi mmoja.
Inategemea na vile mlivyokubaliana kama wewe ulisaini bila kusoma imekula kwako
Hapa sheria haihuu saana sababu yeye atabezi kwenye kile mlichosainishana unless otherwise.
 
hee! umetoka lini gerezani? Hivi aliyekufungia ni huyu huyu JF Moderator 1 au? Mlikuwa mnajadili nini yakamshinda? Ukisikia na mimi nimefungiwa usishangae maana huwa sina hulka ya Kitanzania ya kukubaliana kubaliana na kila hogwash inayosemwa lakini kwa wewe nimeshangaa sana maana huwa huna hiana na mtu.

Gaijin, hebu nisaidie tafadhali hapo kwenye hiyo sheria aliyobandika juu page zima, ni wapi paliposemwa uki quit kazi unamlipa mwajiri mshahara, matter of fact ni wapi hapo pameongelea notice ya mfanyakazi kwenda kwa mwajiri at all?

Ndo maana huwa nasema Tanzania hatuna wataalam halafu naonekana nina kiburi, nilishapima sana kufikia kusema hivyo, sasa hawa ma lawyer jamani ndio mnategemea wakawaandikie international contracts za kuuziana technical product kama umeme na Uranium? Please.

Wapi sheria imesema hivyo shemeji?

Shem vifungu vya hapo juu vinaelezea haki ya mwajiriwa iwapo mwajiri ataamua kusitisha mkataba bila notisi ya mwezi, kuna mahali nimewekea mabano kwenye bandiko langu kuwa 'sina hakika' na provision ya aina hiyo inayompa haki mwajiri kama muajiriwa ataamua kuacha kazi bila kutoa notisi ya mwezi lakini hata hivyo waajiri wengi kwenye mikataba ya kazi wanaweka hiyo 'clause' kuwa akikuachisha bila notisi ya mwezi atakulipa mshahara wa mwezi na wewe ukiacha kazi bila notisi ya mwezi utamlipa pesa inayolingana na mshahara wako wa mwezi.
 
Wewe muuliza swali ngoja nikuulize........

Wakati ukisaini huo mkataba ulliusoma??? Na kama uliusoma ulisemaje??

tuanzie hapo ndo tuendelee................

Sabaabu kwa mfano mimi niliwahi kusaini mikataba mbalimbali
Mmoja ukasema ukitaka kuacha kazi toa notice ya miezi mitatu au ulipe mshahara wa mwezi mmoja
Na mwajiri akikufukuza kazi anakulipa mshahara wa mwezi mmoja na kama unaarreas za leave anakulipa
Mwingine ukasema mwajiri akikufukuza anakulipa mshahara wa mwezi mmoja
Na ukitaka kuacha kazi utoe notice ya mwezi mmoja ama ulipe mshahara wa mwezi mmoja.
Inategemea na vile mlivyokubaliana kama wewe ulisaini bila kusoma imekula kwako
Hapa sheria haihuu saana sababu yeye atabezi kwenye kile mlichosainishana unless otherwise.

maelezo yako mazuri...

hapo kwenye red lazima sheria ihuu sana Dena vinginevyo mkataba utakuwa batili
 
Back
Top Bottom