Kitwana Manara aliwezaje kucheza kama mlinda mlango na mshambuliaji?

Marumeso

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
1,410
1,313
Kuna mwenye data za Kitwana Manara? Nilisikia alikuwa akicheza kama golikipa wa timu ya taifa na wakati huohuo akicheza kama senta fowadi pale Yanga.

Naona kama hadithi tu maana huyu mtu alikuwa ni mtu wa namna gani kucheza maeneo hayo mawili tofauti tena katika kiwango cha juu kabisa?

Mwenye data tafadhali.
 
Kitwana Manara yupo dar mjasiria mali. Ni kweli alanza kuwa golikipa wa yanga na Timu ya Taifa. baadaye akanza kucheza kama Centre Forward kuanzia mwaka 1968. Alikuwa hatari sana angani hasa wakati wa kona.
 
Amekuwa akitoa historia yake ya soka kwa wiki mbili mfululizo kupitia mahojiano na BBC. Ni kweli kwamba alikuwa center foward wa yanga na wakati huo huo akiwa kipa namba moja wa timu ya taifa!
 
Mkubwa ni Kitwana Manara. Pia alikuwepo mdogo wao anaitwa Kassimu Manara
Kassim manara alicheza soka ya Kulipwa Austria . Nakumbuka 1990/1991 Taifa Stars ilicheza na Sudan Daresalaam matokeo yakawa 1-1 goli la stars alifunga Kassim manara kwa tiktak nilikuwepo uwanjani . Golikipa wa Sudan alikuwa mrefu sana halafu Mweusi sana . Huu ukoo wa manara walikuwa Yanga wote, kizazi kipya Haji manara ndiyo simba
 
Ukumbuke baba yao kina Sunday na Kitwana alikuwa Simba, ila watoto ni Yanga. Usimlaumu Haji ni mahaba ndio yanayomfanya awe vile.
 
KIONGOZI UNAWEZA KUDADAVUA HUU UBUYU!?

Alishawahi kumatwa na magari ya wizi miaka kadhaa ya nyuma (tena akiwa kiongozi wa ccm ngazi fulani - sikumbuki vema hiyo ngazi - wilaya ya Ilala). Aliepuka kifungo kwa kutumia jina na connection ya baba yake.

Update: alikuwa katibu mwenezi wa ccm wilaya ya Ilala. Na kesi yake ilihusisha utapeli na magari ya wizi.
 
Back
Top Bottom