Msaada kisheria kuhusu kurushiwa matope barabarani

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,465
20,211
Jamani msaada wenu wa kisheria Kuhusu huyu jirani yangu ambaye ustaarabu mdogo umemshinda

Iko hivi kila siku asubuhi huwa natoka nje ili kusubiria bajaji au pikipiki kwa ajili ya kwenda kwenye mizunguko yangu,tatizo linakuja kuna jamaa flani jirani yangu imetokea zaidi ya mara 3 kila akiniona anasubiria sehemu yenye maji hapo ndipo utamuona ananipita kwa nguvu na gari lake na kunirushia maji,

Wajuzi wa sheria ili suala naweza kumpandisha jamaa mahakani na Kuweza kushinda hii kesi ikiwezekana aweze kunilipa fidia kwa usumbufu alionifanyia hizi siku mbili tatu?

Je na mimi nikianza kutembea na kakopo kadogo kamatope ili akinirushia tu na mimi namrudishia hapohapo on the spot.Je kisheria anaweza kunishitaki kwa hilo au imekaaje hii?


Na kama kuna mtu ana kitu cha kuongezea nitashukuru sana kwa msaada wake
 
hahaaaa nimemkumbuka wolper wa diamond....apo huna namna ni kuvumilia tu au ukimuona anakuja usimame sehem ambayo haina maji......sasa wewe unajilengesha apo kwenye mimaji???:D
 
kuna jamaa dar ....alikua anatoka law school anaenda zake kituoni simu2000...daladala ikapita na kumwagia tope..
alichofanya ni kuchukua Namba ya gari na kuwaonyesha matrafiki...
katimka na elfu 50 yake ya sabuni...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom