Msaada katika Elimu....

Juniors

Member
Jul 30, 2011
6
2
Hello Wanajamii, ni mara yangu ya kwanza kuomba ushauri hapa ukumbini baada ya kuvutiwa na fikra za maana hapa. Mm ni mwanafunzi wa BA Political science and Economic mwaka wa mwisho nchini India, matumaini yangu ni kua Balozi mbeleni kuiwakilisha nchi yangu ni kozi nogo zipi zinanifaa ili kufanikisha malengo yangu?
 
Nafurahi kuona una malengo mazuri. Ila kwa siasa za Tanzania ni ngumu kusema elimu yako unayotaka kusoma ndio ikufanye uwe balozi. Mabalozi wa Tanzania ni wateuliwa wa rais....na hivyo ni watu wa karibu, au wenye undugu na viongozi wakubwa, na ni wana CCM. Angalia list ya mabalozi wote wa Tanzania niambie ni wangapi wameteuliwa kutokana na elimu yake ya kidiplomasia nk.

Hakuna kozi ya kuwa balozi. Balozi ni "rais" wa nchi husika katika nchi anayoiwakilisha. Hivyo basi hakuna kozi ya kusoma ili uje kuwa rais. Kinachotakiwa unachosoma chochote kile soma na bobea kwenye nyanja hizo ambapo zitakusaidia kukubeba.

Ila kwa kuwa unasoma sasa Political Science and Economics, unaweza kusoma International Relations, Diplomacy, Conflict Resolution, International Economy, Political Economy, Public Administration, nk...ni kozi nyingi sana ambazo ni related na ulichosema kwenye degree yako ya kwanza ambapo inabidi ujiendeleze

MAKULILO
 
Back
Top Bottom