Msaada juu ya sheria za ndoa

drphone

JF-Expert Member
Sep 29, 2009
3,542
281
jamani naomba mchango wa mawazo kuhusu ndoa hivi mke anapoamua kutelekeza ndoa yake mwenyewe bila kufukuzwa na mume wala kupigwa na kusema sipo tayari kuishi na ww zaidi ya mwaka alafu anakufata anakwambia umpe kiasi fulani cha pesa ili asikupeleke mahakamani mgawane nyumba na gari ambavo akuchangia ata senti moja na anakiri ivyo ila anasema nikigoma atakwenda mbele ya sheria ili mahakama ipige mnada tugawane pasu pasu hii imekaaje wadau naombeni ushauri. ivikweli sheria ndio inavyofanya mke akufanyie makusudi ili mkagawane mali wakati tuna mtoto wa 4yrs
 
Mwambie aende mahakamani akajitie kitanzi mwenyewe!!!
 
Kama sijakosea, sisi tunafuata sheria kama za Uingereza. Hivyo kama ameondoka nyumbani basi hata mahakamani hatapata kitu!!
 
Sheria ya ndoa ipo wazi kuhusu haki na wajibu katika ndoa, talaka na kuachana zinautaratibu wake. Hata kugawana mali pia kuna utaratibu wake. Hofu ondoa kuhusu kwenda mahakamani.

Kama unaugomvi au matatizo ya kuwaachanisha, hayo ni maelezo ya kiushahdi kama utafikishwa mahakamani. Tafuta thread ya "Sheria za ndoa" katika hii forum, kuna michango ya kutosha ilikwishatolewa kuhusu masuala ya ndoa, talaka, kutengana nk.
 
jamani nashukuru kwa michango yenu angalau hofu imetoweka sasa na nitatafuta mwanasheria kwa msaada zaidi
 
Back
Top Bottom