Msaada- Jinsi ya kutengeneza maandazi

Yogati

Member
Jan 1, 2013
14
1
Wanajamii habari za asbh, naombeni maelekezo jinsi ya kupika maandazi yawe mazuri kwa ajili ya familia wajameni.
Asanteni
 
mahitaji
andaa unga wako wa ngano, hamira, baking powder, iriki maziwa fresh, maji, mafuta ya kula, chumvi na sukari.

matayarisho
chekecha unga wako kuondoa mabongebonge halafu weka kwenye chombo kisafi halafu weka mayai na maziwa hamiri(weka kwenye maji ya moto iliiyeyuke) pamoja na iriki zilizo sagwa changanya mpaka uwe laini halafu uweke uumuke baada ya kuumuka usukume kwa unavo sukuma chapati halafu kata saizi unayotaka

baada ya hapo sasa

weka mafuta yako kwenye kikaango kwenye moto yakishachemka weka kipande kuangalia kama yamepata moto sana kama ya moto sana halafu punguza moto kisha tia maandazi yako yakishakuwa ya brown geuzi pande zote halafu weka karatasi safi kama tissue hivi ili yanyonye mafuta baada ya kuepua.

hapo ni tayari kwa chai, juisi, maziwa na tusker baridi..
 
ukiataka andazi lainiiiiii.jinsi ninavyopika mimi.
MAHITAJI:
Unga wa ngano,sukari,hamira,siagi kidogo sana,sukari,hiliki na tui na lazi.
JINSI YA KUANDAA:
Unachunga unga wako{tatizo langu nikipika huwa nakisia}ukishakuwa tayari unatia tui la nazi,sukari,hamira kama kijiko kikubwa kimoja, siagi kama kijiko kidogo kimoja na hiliki.unga ukishakandika unaufunika na unauacha mpaka uumuke.ukishaumuka unasukuma, usiwe flat kama chapati,uwe mzito kidogo.unakata shape unayoitaka.
unachukua karai unatia mafuta,yakishapata moto{moto usiwe mkali ukiwa mkali maandazi hayatoiva ndani}unachoma maandazi yako.
 
ukiataka andazi lainiiiiii.jinsi ninavyopika mimi.
MAHITAJI:
Unga wa ngano,sukari,hamira,siagi kidogo sana,sukari,hiliki na tui na lazi.
JINSI YA KUANDAA:
Unachunga unga wako{tatizo langu nikipika huwa nakisia}ukishakuwa tayari unatia tui la nazi,sukari,hamira kama kijiko kikubwa kimoja, siagi kama kijiko kidogo kimoja na hiliki.unga ukishakandika unaufunika na unauacha mpaka uumuke.ukishaumuka unasukuma, usiwe flat kama chapati,uwe mzito kidogo.unakata shape unayoitaka.
unachukua karai unatia mafuta,yakishapata moto{moto usiwe mkali ukiwa mkali maandazi hayatoiva ndani}unachoma maandazi yako.

Asante sana ila kuna kitu bado kinanichanganya, does it mean ukiweka hamira huweki baking powder? Au unaweza weka vyote?
 
Asante sana ila kuna kitu bado kinanichanganya, does it mean ukiweka hamira huweki baking powder? Au unaweza weka vyote?
kwa upande wangu mimi,maandazi siweki baking powder.baking powder inavimbisha,hamira huwa inatosha.kwani hamira inaumusha maandazi
 
maandazi ya oven yakoje yakhe?

Ukishayakata unayatia kwenye oven unayachoma..tena wewe Ndio inakufaa coz maandazi ya mafuta yanakushinda..na maelezo yalotolewa hapa hata ufanyeje huwezi pata andazi zuri sbb andazi linaitaji kupima maranyingi kwa maelezo tu huwezipata andazi zuri uwoni kinachofanyika ujue ulaini wa ungakiasi gani Na mengine mengi
 
FirstLady1 , maandazi ndo hayo....

Unga 3 1/2kg
Maziwa ya vuguvugu (warm) 1 glass
Sukari ½ glass
Maziwa ya unga ½ glass
Iliki ilyosagwa ¼ tsp
Baking powder 1 tsp
Siagi iliyoyeyushwa 4 tsp
Mafuta4 tsp
Viini 2 vya mayai S
Mafuta ya kupakiza

Umusha hamira peke yake kwa kutumia vipimo hivi hapo chini
Hamira 2 tsp
Unga wa ngano 1tspa
Maji 1 ½ glass au nazi
Sukari 1 tsp

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika kibakuli changanya hamira, unga, maji na sukari kwa kijiko na iache iimuke kama dakika 5 hivi. Changanya vipimo viliyobakia ( isipokuwa baking powder) Katika bakuli la mashine. Kisha tia ule mchanganyiko wa hamira na uendelee kuchanganya kwa muda wa dakika 8. Halafu tia baking powder na changanya tena dakika 3 zaidi.Funika na iaache kwa dakika 5.

Chukuwa treya na uipake siagi au mafuta kisha nyunyizia unga kidogo tu. Paka mikono yako mafuta ukishika mchanganyiko wa unga kwani utakuwa unanyata mara ya kwanza. Gawanya donge la unga mara 8 sawa sawa. Kisha funika na iiache dakika 10. Halafu Sukuma kila kidonge kwa kadri ya mviringo wa nchi 5 kwa upana kisha kata mara nne. Panga mahamri katika treya na uwache nafasi ya kiasi baina kila moja. Iache iimuke pahali penye joto kwa muda wa masaa mmoja na nusu hivi, ni muhimu maandazi yaumuke sana

Weka maandazi yako katika oveni iliyokwisha kupata moto wa 180°C kwa muda wa dakika 8 au hadi igeuke rangi .
 
Last edited by a moderator:
@FL1 maelezo hayo hapo juu yanatosha. usiwe tu mvivu wa kukanda unga inabidi uukande ukandike uwe laini kihaswa ndo utaona ulaini na uzuri wa andazi usipoukanda sana hayawi laini.
 
Njiabrahisi zaidi ya kufanya maandazi laini na hata chapati, baada ya kuchekecha unga, tia mafuta ya moto sana kiasi kidogo tu kama nusu kikombe huku unavuruga na uma ama kisu. Then rub in the oil (kwa kumaliza madonge kwa kutumia vidole tu na sio mkono mzima). Unafanya hivyo huku unavuta mikono juu, hii ni kuongeza hewa ndani ya unga.

Unaweza pia.kutumia blue band. Unaweka kwenye unga na kuupikicha kwa vidole. Baadae unaweka hamira na sukari na kukanda kama kawaida.
mie mbona huwa nafata hayo yote mandazi yanakuwa magumu why?
 
fuata maelezo yote huko juu lkn [MENTION=43938]Firstlady kabla hujachanganya na kitu chochote huo unga chemsha mafuta ya kula ka robo kikombe yachemke sn mimina hayo mafuta kwenye huo unga,changanya vizur na anza kuweka hivyo v2 vingine km walivyochangia watu, utajanambia hapa hapa JF ok!!!!!
 
Back
Top Bottom