Msaada: Jinsi ya kubadili maji chumvi ili yawe maji laini

Bitabo

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,900
687
Wadau.

Nyumbani kwangu mabomba yanatoa maji ya chumvi japo huwa yanaingia kwenye reservoir then na pump kwenye tank ndo yanaingia ndani.
Sasa natafuta utaalam wa kuyabadili haya maji chumvi ili yawe maji laini (bila chumvi) au maji baridi kama yanavyofahamika kwa wengine.

Ntashukuru zaidi kama mtanishauri na side effects kwa njia mtakazonishauri.

Nawasilisha
 
Bitabo, mbona unaleta challenge kali kiasi hiki! Zaidi ya "evaporation", kuchemsha maji yako na kuchukua mvuke, sijui kwa kweli. Labda uyagandishe halafu kuyayeyusha kwa kiwango fulani, ambapo chumvi inakuwa katikati ya barafu na utakapokuwa unayeyusha barafu unaacha ile barafu ya kati isiyeyuke na kuitupa kwa kuwa ina chumvi kali.

Lakini si unaona njia zote hizi zaweza kuwa na gharama zaidi ya kutafuta maji mengine!
 
kasome kitabu cha 4m two, methods of separating mixtures, simply chemsha maji, yakitoa mvuke, vuna huo mvuke kwa kifaa baridi mfano chupa....hebu google methods of separating mixtures uone had picha.
 
Back
Top Bottom