Msaada: Je ni benki gani inafaa kwa kufungua account ya biashara?

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Habari zenu wana JF. Mimi ni mfanyabiashara. Nina kampuni yangu ambayo nimeianzisha hivi karibuni ambayo ninataka kuifungulia account yake. Ninaomba msaada wenu kwa yeyote mwenye ufahamu wa kutosha kuhusu mambo ya mabenki aweze kunishauri benki nzuri inayofaa kwa kufungua account ya biashara au kampuni. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa yeyote ambaye atajitokeza kunisaidia katika hili. Asante
 
Nakushauri fungua CRDB imekaa kirafiki na mteja, NBC ni ya kibiashara zaidi, NMB soi mbaya sana ingawa ina urasimu wake. Pia ushauri utakaoupata jukwaani hapa hata nawe utaufanyia kazi kwani mpaka unafikia kufungua buz accont ina maana hukuwa unatumia kibubu.
 
Young_Master,

Mimi ningependa kujua kwanza wewe biashara yako kubwa? ndogo ? au ya kati?

Pili je unategemea kufanya transactions za aina gani? ni TISS transfers Ambayo ni kutuma pesa account ya benki moja kwenda nyingine? au utafanya sana Telegraphic Transfers (swift) nje ya nchi au transactions nyingi ni ku deposit na ku withdraw, au kubadilisha currency tofauti?

Zingatia yafuatayo utakapoenda kuongea na benki (1) Charge ya kila mwezi (2) Charge ya kila transactions (3) Charge ya ku deposit/withdraw pesa kwenye acc yako (4) Kiwango cha kutoa bila notice

Kuna benki ambazo huwezi siku kukurupuka kwenda kuchukua milioni 20 wanataka notice ya siku moja, kama biashara yako ipo spontaneous aisee uta suffer.

Mimi ningeshauri uende kwenye benki ndogo ambazo ni more customer focused and hazina mlolongo na mistari, ukiwa mfanyabiashara hutakiwi ukae benki 1 - 2 hrs. Achana na NMB , CRDB na NBC.
 
nadhani CRDB ni nzuri; Hii analysis imetokana na mazungumzo nilyokuwa na ma Director wa Business Accounts hapo Tanzania; lakini ni siku za mwanzoni, tunaendelea kuwafahamisha kuhusu nini kinaendelea;
 
mimi nimefungua access bank -- mikopo hawanaga longo longo nyingi kama mambenki makubwa. ile ina deal na wajasiriamali wadogo wadogo.
 
samahani mkuu nadhani umetoka nje ya mada kidogo. Mimi ninahitaji kufungua account kwa ajili ya biashara au kampuni na si vinginevyo
 
avatar yako inaonyesha wewe ni mpole na una macho malegevu basi moja kwa moja benki inayokufaa wewe ni VICOBA maana haina viungulia kama benki nyingine..umenisikia eeeh
 
Nakushauri fungua CRDB imekaa kirafiki na mteja, NBC ni ya kibiashara zaidi, NMB soi mbaya sana ingawa ina urasimu wake. Pia ushauri utakaoupata jukwaani hapa hata nawe utaufanyia kazi kwani mpaka unafikia kufungua buz accont ina maana hukuwa unatumia kibubu.

Hata mimi kwa mawazo yangu nadhani benki ya CRDB inafaa sana kwa kufungua account ya biashara japo kuwa sina taarifa za kutosha kuhusu benki hiyo. Nashukuru sana kwa ushauri wako mkuu. nitaufanyia kazi
 
samahani mkuu nadhani umetoka nje ya mada kidogo. Mimi ninahitaji kufungua account kwa ajili ya biashara au kampuni na si vinginevyo

Unapofungua account na hasa kwa ajili ya biashara ni muhimu sana kuangalia benki amabayo iko friendly na ina uwezo wa kukuwezesha kwa njia mbali mbali hasa mikopo ya masharti nafuu ili uweze kukuza biashara yako zaidi. Kwa hiyo mdau aliyekushauri kuhusu Access bank hajakosea kabisa. Kumbuka inaweza ukawa na mtaji leo, kesho mtaji ukapungua au ukapata opportunity nzuri ya biasha ambayo itakuhitaji kuongeza mtaji ili kum meet requirements, kwa hiyo if you are running with good bank they will be there to assist you.
 
Sawa sawa mkuu. nimekuelewa. Kwa hiyo kutokana na uzoefu ulionao na maoni yako unanishauri nifungue account katika benki gani?
 
nadhani CRDB ni nzuri; Hii analysis imetokana na mazungumzo nilyokuwa na ma Director wa Business Accounts hapo Tanzania; lakini ni siku za mwanzoni, tunaendelea kuwafahamisha kuhusu nini kinaendelea;

Unaweza kunipa maelezo zaidi kuhusu benki ya CRDB mkuu???
 
Young_Master,

Mimi ningependa kujua kwanza wewe biashara yako kubwa? ndogo ? au ya kati?

Pili je unategemea kufanya transactions za aina gani? ni TISS transfers Ambayo ni kutuma pesa account ya benki moja kwenda nyingine? au utafanya sana Telegraphic Transfers (swift) nje ya nchi au transactions nyingi ni ku deposit na ku withdraw, au kubadilisha currency tofauti?

Zingatia yafuatayo utakapoenda kuongea na benki (1) Charge ya kila mwezi (2) Charge ya kila transactions (3) Charge ya ku deposit/withdraw pesa kwenye acc yako (4) Kiwango cha kutoa bila notice

Kuna benki ambazo huwezi siku kukurupuka kwenda kuchukua milioni 20 wanataka notice ya siku moja, kama biashara yako ipo spontaneous aisee uta suffer.

Mimi ningeshauri uende kwenye benki ndogo ambazo ni more customer focused and hazina mlolongo na mistari, ukiwa mfanyabiashara hutakiwi ukae benki 1 - 2 hrs. Achana na NMB , CRDB na NBC.

Kwa sasa biashara yangu ni ndogo ila nitahitaji account ya benki ambayo haitanipa shida hata mtaji wangu ukikua. Namaanisha sitaki account za temporary.
Pia nadhani biashara yangu itafanya TISS transfers Ambayo ni kutuma pesa account ya benki moja kwenda nyingine, pia itafanya Telegraphic Transfers (swift) nje ya nchi na pia ku deposit na ku withdraw
 
Mkuu nenda FNB kafungue account, service zao ni nzuri

Ni kwa nini nikafungue account FNB badala ya benki nyingine. Unadhani FNB inatoa huduma gani bora ambazo zitanishawishi mimi kama mteja kwenda kufngua account kwao? Na je benki hiyo itaninufaishaje mimi na bishara yangu?
 
Kama una maswali nenda Bank ukaulize mimi sio mfanyakazi wa Bank au msemaji wa hiyo Bank, unauliza Bank gani nzuri kwa kufungua account yako ya biashara kama ushauri, ila kilichonifurahisha hiyo Bank ni Huduma yao wanayoitoa kwa wateja. Kama una maswali nakushauri tembelea Bank zote halafu uchambue mwenye
 
Back
Top Bottom