Kunuka kikwapa: Fahamu chanzo, tiba na namna ya kuepuka tatizo

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,489
79
Kwapa2.jpg

Wakuu,

Kunuka harufu mbaya (kikwapa) ni ugonjwa au uchafu? kama ni ugonjwa kuna dawa?

Kuna hii hali ambayo mtu ananuka kikwapa wakati wa kula tunda (wakati mwingine aaaah yuko safiii tu). Je, inatokana na nini? Na nini kifanyike ili kuzuia hali hiyo?


MASWALI NA MAHITAJI YA WADAU WENGINE
Jamani naomba msaada kwenu kwa anayeifahamu dawa ya kumaliza tatizo hili kwa sababu ninaye mtoto wa miaka 11 wa kike anasumbuliwa na tatizo hili (la kunuka kwapa) hata atoke bafuni kuoga au ni ugonjwa wa kurithi?
Watalaam,

Naomba kujuzwa dawa ya kutumia ili kuondoa harufu ya kikwapa.

Asante.
Jamani naombeni msaada kwenye hili suala kutoa harufu makwapani.

Nina uhakika kwamba, hakuna mtu miongoni mwetu, ambaye ameishafikia balehe, na hajawahi kukumbwa na tatizo hili la kunuka KIKWAPA. Wengi wetu tunakabiliana na hali hiyo kwa kutumia DEODORANTS za aina mbalimbali na PODA kwa wakina dada. Lakini maelfu, hususani kwa huko nyumbani, aidha kwa sababu ya hali ngumu ya maisha au kutokuwa aware na hali hii au kwamba kuna vitu unavyoweza kutumia ili kukabiliana na hali hii, basi suala hili limepuuzwa.

Mpaka miezi miwili iliyopita, nilikuwa nafanya kazi kwenye NGO moja hapa Ughaibuni, ambayo inayojishughulisha na kuwa-integrate the newly arrived immigrants katika mambo ya Lugha (English/French), local culture, na Employment. Hivi karibuni tulipokea wageni kadhaa kutoka Zimbabwe na Congo, na ambao baada ya kuwakaribisha na kuwaonyesha sehemu mbalimbali za kupata huduma (Hospital, School, na Metro Transportation), tuliwapeleka sehemu mbalimbali ili kuanza ajira. Sasa, katika kufuatilia maendeleo yao huko makazini, hakukuwa na malalamiko kuhusu utendaji wao wa kazi. Malalamiko makubwa kutoka kwa ma-supervisors wao ni kwamba baadhi ya hawa jamaa wanatoa harufu kali sana (Kikwapa), haswa wakati wa kupiga boksi. Wakatuomba tuwashauri hawa jamaa wawe WANAOGA kila siku. Nimejaribu kuwafahamisha hawa jamaa kwamba hawa wageni wanaoga kila siku, isipokuwa hawajazoea kutumia Deodorant. Supervisors hawaamini kwamba mtu anayeoga kila siku atakuwa ananuka kikwapa kiasi hicho.

Kivumbi kilichonipata ni kwamba, nilipowashauri hawa jamaa kuhusu tatizo hili na kuhusu matumizi ya Deodorants, baadhi yao hawakufurahishwa na ushauri wangu. Moja wao (kutoka Congo- Kinshasa) kanishutumu kwamba nimeishabadilika kimaadili kwa kuiga tabia za wazungu!!!

Sasa swali ni je, ni kweli kwamba Waafrika peke yao ndio wenye kunuka KIKWAPA? Pili, utamshauri vipi mtu kuhusu suala personal kama hili? Na mwisho kabisa, je dada zetu wanadeal vipi na hali kama hii katika mahusioano yao? Haswa tukizingatia kwamba mke au rafiki lazima anajuwa kilema cha mume au boyfriend wake.

Je, wakina dada wanawaambia ukweli waume na marafiki zao ili kukabiliana na hili TATIZO? Nasita kutumia neno AIBU kwa sababu nafahamu kwamba kuna baadhi ya jamii na makabila ambayo yanatumia zaidi harufu zao (Olfaction) kuliko kuona au kugusa katika maisha yao ya kawaida. Lakini nimeishashuhudia mara kadhaa Wazungu na makabila mengine wakiwanyanyasa watu weusi kwa sababu ya tatizo la KIKWAPA. Msemo kwamba WAAFRIKA WANANUKA ndio imekuwa joke kwenye sehemu nyingi za kazi.

Things in Perspective:
Suala la kutoa harufu (yoyote) linaweza kuangaliwa katika sehemu kuu mbili au tatu muhimu: 1. Power 2. Classs, 3. Racism kama inavyoelezwa na Ruth Finnegan (2007): Odour is a peculiarly emotive basis for social inclusion and exclusion, often invoked by powerful groups to both distinguish and stigmatised those they classify as inferior or alien (Finnegan 2007).

Mfano:-England wakati wa Industrial Revolution; the Bourgeoisie class waliwashutumu the Proletariat class kwa kutoa harufu mbaya.

-Britons walipokuwa wanaitawala India waliwashutumu Wahindi kwa harufu mbaya.
Racism/Discrimination: Nchini Marekani, haswa wakati wa UTUMWA, wakati wa Civil Rights Movement na mpaka leo wanawashutumu Wamarekani weusi kwa kutoa harufu mbaya.

-German (Third Reich) iliwashutumu European Jews kwamba wanatoa harufu mbaya, pengine kuliko binadamu yoyote yule Duniani.

-Wakati huohuo kuna baadhi ya makabila au jamii ambazo hutumia harufu katika maisha yao ya kila siku. Kwa mfano, The Desana- Amazon Rain Forest, the Umeda- Papua New Guinea, na the Dassanetch- Ethiopia. Kwa tamaduni za haya makabila; harufu ya kila kitu ni muhimu kuliko kuona (Smell outdistance sight).:A S 39:
Watu tunapokuwa au tunapotoka vibaruani, kunuka jasho au vikwapa inachukuliwa kawaida muda huo coz mwili unakuwa umeshachemka kwa majukumu.

Kunachonishangaza ni asubuhi watu wanatoka majumbani wakiwa wametoka kuamka na wanaenda kazini au mashuleni (wanafunzi) wakiwa wamependeza kwa mavazi na ngozi lakini wananuka vikwapa na jasho asubuh asubuh tena karibia kila siku wanakuwa hivyo.

Huwa najiuliza wana matatizo gani?

View attachment 1185857
Jamani Wana JF,

Naomba mnielezeni inakuwaje mtu ananuka kwapa bila yeye mwenyewe kujishitukia? Kuna jamaa alikuwa na demu wake ikabidi waachane kwa ajili ya kwapa! Hali hiyo iko hata mpaka kwa baadhi wasanii wetu, huwa wakiperform wanatema kiasi kwamba hutamani hata kuwa pale mbele. Mfano Twanga Pepeta. Wakimaliza pepeta ule uvundo huwa mandhari haikaliki? Je, wanamatatizo na pua zao?


MAJIBU NA MICHANGO YA WADAU
Jambo hilo huwakwaza watu wengi na hivyo kujikuta wakitengwa bila kujua sababu.

Kunuka kikwapa ni tatizo kubwa katika mwili wa binadamu. Tatizo hili husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu chini ya kwapa.

Sasa basi, kuna njia nyingi ambazo watu wengi huzitumia ili kwapa liwe na harufu nzuri, kavu na safi.

Wengine hutumia njia za kisasa ambazo ni pamoja na kupaka doodoranti au pafyumu zinazosaidia kuondoa harufu mbaya mwilini.

Lakini kama hiyo haitoshi, kuna njia za kisasa zinazoweza kuzuia harufu ya kwapa ambazo ni pamoja na kupaka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya.

Kuvaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufi zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kuwa kavu, safi na bila harufu mbaya.

Kuoga kila siku na kusafisha nguo kwa maji safi kunasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya.

Pia kunywa maji mengi kila siku kunakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.

Njia nyingine inayoshauriwa ni kuhakikisha kuwa unaosha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps).

Aidha, kupunguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu. Inasemekana kuwa kula vitunguu vingi kunachangia mwili kutoa harufu kali.

Licha ya pafyumu na spray kusaidia kuondoa harufu mbaya mwilini, hii si dawa endelevu kwani baada ya muda harufu inaweza kurudi palepale hivyo ni vema kutumia njia za asili kukabiliana na hali hiyo. Pafyumu haiwezi kutibu tatizo moja kwa moja.

Pia inashauriwa kuwa baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao huwavutia bakteria kukua katika maeneo yaliyojificha (yenye mikunjo).

Mbinu nyingine ni kujitahidi kunyoa nywele za kwapa mara kwa mara na kuepuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.

JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA KWAPANI

Hakikisha unaoga kila siku ili kupunguza idadi ya bakteria kwapani kwani husababisha kuweka harufu mbaya kwenye mwili hasa majira ya joto kwa kuwa mara nyingi joto ndilo husababisha jasho na harufu kwapani hivyo unahitaji kuoga mara mbili kila siku, unaweza kutumia sabuni au anti-bacterial na maji ya moto.

Safisha nguo katika maji ya moto na sabuni ya kuondoa uchafu na mafuta, vaa mashati safi. Inapendekeza kuvaa mavazi yenye nyuzi za asili, kama vile pamba na hariri ili kusaidia kunyonya unyevunyevu na kuruhusu ngozi kupumua.
Wakati unafanya mazoezi, tumia nguo zenye vitambaa ambavyo vitanyonya unyevunyevu kwapani ili kuzuia harufu mbaya.

Vinega ‘siki' na mafuta ya chai ' tea tree oil'
Apple cider siki na vinega nyeupe, hupunguza harufu kwapani. Ili kukabiliana na harufu, loweka pamba katika vinega, paka kwenye makwapa badala ya deodorant. Mbali na tiba hiyo, tumia tea tree oil, inaweza pia kuwa na manufaa kwa sababu ni anti-bacterial.

Limao
Kata limao au ndimu nusu kwa kisu. Paka kipande cha limao ulichokata kwenye kwapa lako na hakikisha unalisugua mpaka litoe maji yake. Weka kwapa lako lipate hewa ili hiyo juice ya limao uliyopaka ikauke.

Asidi citric katika maji ya limao inasaidia kutoa tezi ya jasho hivyo kuondoa harufu.

Hatua tano za kusaidia kuondoa harufu mbaya ya mwili

1.) Be Clean in Body and Dress
Since bacteria are mainly responsible for producing BO, cleanliness is an important part of the total solution. Bathe daily, using a mild soap (deodorant soaps are not only harsh to the skin; they also encourage the growth of resistant bacteria). Change into a clean set of clothes after bathing.

2.) Examine Your Diet
There are some foods that can contribute to body odors. Meats, alcohol, strong curries are some of them. Try to examine what you eat and its effects on your body.

Body odor is a condition with multiple possible causes. Many therapies exist, ranging from self-care to medical or surgical treatment.

3.) Drink Plenty of Water
You need to be clean inside as well as outside. Water is a good cleansing agent; it helps to flush out unwanted poisons from our bodies. Start your day with a glass or two of fresh clean water (this also helps to stimulate bowel movement) Strive to drink the usual norm of eight glasses a day.

4.) Practice Daily Elimination
Daily elimination helps your body to remove harmful waste substances that will make you sick. Strive for a diet that is more alkali than acidic. Reduce meats, fats and sugar intake Eat more fiber rich foods, especially fruits and vegetables. This will even positively contribute to your overall health.

5.) Use a Natural Deodorant
Have you tried baking soda? Its the best kept deodorant secret! Baking soda is effective, natural and economical too. Just keep a box handy in the shower and rub a good amount in your armpits after you towel yourself dry. If you want to add some scent, mix some baby powder. If you want to feel extra dry, you can also add some cornstarch. Baking soda is good for many other cleaning and deodorizing uses around the home, the kitchen and even the garage.

Body odor is something that all of us can do without. Apply these tips and banish BO forever from your life!
Tumia Anti-perspirant deodorant

Siyo tu atumie deodorant. Anachotakiwa kutumia ni 48 hr clinical strength ANTI-PERSPIRANT deodorant. Kuna tofauti baina ya deodorant na ANTI-PERSPIRANT deodorant.

Mtu mwenye tatizo kubwa la kikwapa deodorant pekee haitasadia kuondoa tatizo. Inapaswa atumie deodorant zinazokata utokwaji wa jasho kwenye kwapa na hizo ndiyo ANTI-PERSPIRANT deodorants.

Baadhi ya watu huwa hawajui hilo. Wakiona tu container lina neno deodorant basi anakimbilia kununua. Sasa deodorants zisizo na anti perspirant ingredients huwa haziko effective kwa watu wenye vikwapa vinavyotema na ndiyo maana utakuta watu wanalalamika kuwa wamejaribu kutumia deodorant lakini wapi.

Ni muhimu sana kusoma ni deodorant ya aina gani mtu unanunua. I always recommend ANTI-PERSPIRANT deodorants.
Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo
  1. Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya
  2. Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya
  3. Oga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya
  4. Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.
  5. Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (magadi au medicated soaps)
  6. Punguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu
  7. Kumbuka kutumia pafyume na Spray zitasaidia kuondoa harufu mbaya kwa muda na sio kutibu tatizo moja kwa moja.
  8. Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.
  9. Jitahidi kunyoa nywele za sehemu hii mara kwa mara.
  10. Epuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.
MATIBABU YA HARUFU MBAYA YA JASHO/MWILI NA KUTOKWA NA JASHO JINGI

Kutokwa na jasho ni kitendo chema kwa afya na mwili hufanya kwa makusudi mazuri kabisa. Kutokwa jasho kunasaidia mambo yafuatayo
  1. Kusaidia kupunguza joto na kupoza mwili
  2. Kusaidia kutoa takataka kutoka mwilini pamoja na maji ya ziada
Hizo ndio sababu baada ya kutokwa na jasho unajihisi mwili kupoa au hata baridi. Pia jasho lina ladha ya chumvichumvi na uchungu, hiyo inatokana na hizo takataka ilizozibeba.
Kwenye kutoka jasho huko kunaweza kukawa na matatizo kidogo hususan kwenye upande wa kiasi na harufu.

SABABU ZA MATATIZO HAYO
Kutokwa na jasho jingi kunaweza kusababishwa na kazi au shughuli anazofanya mtu, aina za vyakula (vyakula vyenye viungo vingi au mafuta mengi nk), magonjwa (mfano mmoja kifuakikuu) na msongo (stress)

Harufu mbaya ya jasho/mwili huweza kusababishwa na uchafu unaotoka na jasho hilo, uchafu wa makwapani pamoja na maambukizi ya vijidudu (bakteria) katika ngozi

MATIBABU YAKE
Kama tunavyosema mara kwa mara, njia nzuri zaidi ya kutibu tatizo ni kujua chanzo chake kisha kuanzia hapo na kuondoa kabisa tatizo hili.
  1. Kama ni ugonjwa au maambukizi ya vijidudu vya magonjwa basi ni vyema kupata matibabu mazuri ya magonjwa hayo na kisha tatizo hili litaondoka kwa urahisi tu
  2. Kama ni uchafu ni vyema kujisafisha mara kwa mara kwa kunyoa na kuoga vizuri kwa sabuni inayosaidia kuondoa uchafu vizuri na vijidudu vya magonjwa. Sabuni zenye dawa kama vile Protex (Aina zote), Dettol (Aina zote), Rungu, Family Medicated Soap nk
  3. Kwa tatizo la jasho jingi unaweza kutumia Antiperspirant na itakusaidia sana. Hiki ni kipodozi maalum kabisa kwa ajili ya kupunguza au kuzuia jasho kutoka. Hupatikana famasi, maduka ya vipodozi na supermarkets
  4. Kwa tatizo la harufu mbaya ya jasho/mwili unaweza kutumia Deodorant na itakusaidia sana. Hiki ni kipodozi maalum kabisa kwa ajili ya kupunguza au kuzuia kabisa harufu mbaya. Hupatikana famasi, maduka ya vipodozi na supermarkets
Oga vizuri na safisha makwapa yote kwa sabuni yenye dawa, hakikisha makwapa yote hayana nywele kubwa na kisha tumia deodorant (kama tatizo ni harufu mbaya) au antiperspirant (kama tatizo ni jasho jingi).


ZAIDI, SOMA:

Kunuka kikwapa ni nini?

Hii ni harufu kali inayotoka kwenye sehemu ya juu kabisa ya mkono kwa chini au kwa jina la kikwapa.

Chanzo ni nini?
kimsingi harufu hii hutokana na bacteria kutumia jasho la binadamu na kutengeneza aina fulani ya tindikali ambayo hutoa harufu. Katika hali ya kawaida jasho binadamu hua halina harufu mpaka pale linapokutana na bacteria ambao hushambualia jasho lako. Mara nyingi binadamu huanza kutoka harufu sana akibalehe au kuvunja ungo ambapo manyoya huanza kuota kwenye kikwapa lakini pia watu wanene sana, wanaokula vyakula vyenye viungo vingi na wenye baadhi ya magonjwa kama kisukari.

Harufu kwenye mwili wa binadamu ukiachana na makwapa pia hutoka sehemu za siri, miguuni, kwenye mikunjo ya nyama kwa wanene, nyuma ya masikio, sehemu ya haja kubwa, katikati ya mapaja, na kwenye nywele za sehemu za siri. Apocrine gland ni sehemu ya mwili ambayo inatengeneza jasho, huapatikana sehemu mbalimbali za mwili kama kwapa, ngozi, matiti,na kadhalika.

Jinsi ya kuzuia harufu
  • Weka safi kwapa lako kwa kuosha na maji safi na sabuni ya kuua bacteria.
  • Tumia deodorant na body spray, mara nyingi hupunguza wingi wa jasho na kukupa harufu nzuri
  • Oga kila siku angalau mara mbili asubuhi na jioni kwa maji ya moto kwani maji ya moto yanasaidia sana kuu bacteria walioko kwenye ngozi.
  • Vaa nguo nyepesi ambazo zinakupa nafasi ya mwili kukausha joto kwa upepo, hivyo usivae nguo nzito sana.
  • Usile vyakula vyenye viungo vingi sana kama kitunguu swaumu lakini pia utafiti umeonyesha kwamba ulaji mwingi wa nyama nyekundu huweza kuongezea harufu ya mwili.
  • Kunywa maji mengi sana kwani yanasaidia kusafisha mwili wako.
  • Nyoa manyoya ya kwapani kila yakiota kwani ni kihifadhi cha harufu kali.
Matibabu
  • Upasuaji; wakati mwingine upasuaji kitaalamu kama endoscopic thoracic sympathectomy ambayo hufunga mishipa ya fahamu ambayo hufanya jasho litoke jingi hufanyika kutibu tatizo hili..
  • Baadhi ya magonjwa ya figo, maini, fangasi, kufunga kwa hedhi kwa akina mama wa umri mkubwa huweza kusababisha hali hii hivyo muone daktari kwa vipimo zaidi na matibabu kama haupati nafuu.
Ni wakati gani unatakiwa umuone daktari?
  • Kutokwa na jasho sana wakati wa usiku.
  • Kutokwa jasho zaidi kuliko mwanzoni.
  • Jasho linaanza kukuzuia na kazi zako za kawaida.
  • Kutokwa na jasho sana wakati wa baridi.
  • Kuwashwa sana na ngozi.

Chanzo: sirizaafya.info
 
Naomba nikuambie hivi mwambie awe anasafisha maeneo yake mpka ndani kila akikoga na pia atumie fame wash kwa ajili ya kukata harufu na usafi pia. Zipo fame wash za oriflame, na nyingine nyingi tu.
 
sanaa mkuu hajui huyu!.
bytheway nimekugongea senksi, thibitisha hapahapa:

Nimekujibu mpwa! Kaangalie. Watu wengine bana! Eti wanaogopa harufu ya kikwapa wakati wenzao hata harufu ya ushuz.i mzito kwao burudani!
 
Pole journal!! kutoa harufu ya kikwapa huwa haina sababu maalum, inawezekana ikawa ni maumbile au ufanyaji wa kazi za kutumia nguvu na nk. Dawa yake niijuayo mimi ni deodorant!! but also kuna vitu kama sabuni ya omo.

Huyo anaetoa harufu awe anaosha kikwapa chake na omo kila mara anapopata nafasi. Au anaweza akapaka ndimu katika kikwapa huwa inakata harufu. Apake mara kwa mara anapopata muda, ataona matokeo yake.
 
Pole journal!! kutoa harufu ya kikwapa huwa haina sababu maalum, inawezekana ikawa ni maumbile au ufanyaji wa kazi za kutumia nguvu na nk. Dawa yake niijuayo mimi ni deodorant!! but also kuna vitu kama sabuni ya omo. Huyo anaetoa harufu awe anaosha kikwapa chake na omo kila mara anapopata nafasi. Au anaweza akapaka ndimu katika kikwapa huwa inakata harufu. Apake mara kwa mara anapopata muda, ataona matokeo yake.

Du! Huo utafiti ulifanywa na dr. gani? nipeni jina lake nimfute kazi. Unamshauri mwenzio apate cancer siyo?
 
Jamani hii harufu naipenda sana kuisikilizia, huwa sipendi kabisa kuona shemeji yenu anatumia deodrant, na mara nyingine huwa nazificha ili nipate kusikia hii harufu, sometime akilala huwa naweka pua yangu kwapani kwake nisikie vizuri harufu hii, nimekuwa kama teja.

Hivi hii kitu kuna wengine wenye kupenda?
 
Unajua kucheka nako kunasaidia ngoja niendelee kujichekea maana mkuu Bwabwa una mambo, kama jina lako lilivyo!Lol
 
Jamani hii harufu naipenda sana kuisikilizia, huwa sipendi kabisa kuona shemeji yenu anatumia deodrant, na mara nyingine huwa nazificha ili nipate kusikia hii harufu, sometime akilala huwa naweka pua yangu kwapani kwake nisikie vizuri harufu hii,nimekuwa kama teja.Hivi hii kitu kuna wengine wenye kupenda?
Jicheki mzee, maana unaweza ukaanza kupenda harufu ya ****** halafu hasa vile vya stendi na sokoni.
 
Haya mambo ni mtu na mtu. mnaijua harufu ya watu wazima ambayo hata akioga bado unaisikia? nadhani ndiyo anayoiongelea.

Niliwahi kuwa na uhusiano na binti mmoja mwaka 96 alikuwa na harufu kali sana hata akioga namna gani haiishi hata akipiga pafyum, ukimkumbatia unaisikia. loh, nilitokea kuipenda sana ukichanganya na ujana wangu wakati ule ilikuwa inanipa wazimu kabisaa.
 
Jamani hii harufu naipenda sana kuisikilizia, huwa sipendi kabisa kuona shemeji yenu anatumia deodrant, na mara nyingine huwa nazificha ili nipate kusikia hii harufu, sometime akilala huwa naweka pua yangu kwapani kwake nisikie vizuri harufu hii,nimekuwa kama teja.Hivi hii kitu kuna wengine wenye kupenda?

Mmmh, watch out!! Unaweza kuwa mjamzito, manake nilisikia waja wazito ndo huwa wanavutiwa na hizo harufu.
 
Kama harufu uipendayo ni ile kabla ya kutumia deodorant, inategemea kama ana mkwapa unatema ka viatu vya michezo na we unafurahia basi we mgonjwa. Lakini its good to be natural mwambie aoge mara kwa mara. Halafu we badala ya kumfurahisha mkeo kwa kumtimizia haki yake ya ndoa we unang'ang'ania kutia pua yako kubwa kama kiganja kwenye kwapa la mwenzio basi we mgonjwa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom