Msaada jamani!

Unapouliza kitu mkuu jaribu walau kufafanua kidogo, unaposema sauti ngapi unamaanisha nini,
pengine ungejiuliza sauti maanayake nini, kifupi ni mlio wowote unaosababishwa na kitu fulani, mfano ukikohoa, radi, upepo mkali, kingora nk hiyo yote ni sauti zinazotokana na kitu husika.
Labda inawezekana unaongelea lafudhi, kama una maanisha hivyo basi ujue kuwa watumiaji wa kiswahili wana lugha zao zinazopelekea kuathiri lafudhi ya utamkaji wa maneno ya kiswahili.
Mfano mchaga, msukuma, msambaa,mkurya,nk wakiongea tu unaweza kujua ni mtu wa kabila gani.
Mara nyingi lugha ya asili ukikua nayo toka utotoni ningumu sana kupotea ktk utamkaji wa maneno wa lugha nyingine, mfano hata muhindi au muarabu akiongea kiingereza utajua tu.
Katika kiswahili watu wa pwani ndio wanachukuliwa kuwa wanaongea kiswahili kilichonyooka na sababu ni kuwa huku ndiko liliko chimbuko lake.
Natumai nimejaribu na haya ni mtazamo wangu
 
bila shaka unarefer phones....kiswahili kina sauti 25.....tano ni sautiza irabu na 20 za konsonant......
 
Back
Top Bottom