Msaada jamani, ninakufa

GlorytoGod

Senior Member
Sep 8, 2012
158
50
Wana jamvi heshima kwenu,
mimi ninaumwa sana mwili mzima lakini kila nikienda hosp. Naambiwa hawaoni ugonjwa nimeshapima vipimo karibu vyote sasa imebakia kipimo kimoja tu lakini kinaniogopesha naombeni tu ushauri kwenu wandugu kabla cjaenda kwa anayefahamu, je kuna madhara yoyote yatokanayo na kupima afya kwa kutumia kompyuta? Maana ndio kipimo nachotakiwa kwenda kupimwa nacho lakini roho yangu inasita sana jamani nisaidieni ushauri tu.

Mungu awabariki
 
pole mpendwa! ngoja wataalamu waje watakujuza! ila zingatia kusali, usikate tamaa, na DAIMA SALA IWE KIMBILIO LAKO!
 
Amina mpendwa wangu ninamwamini sana mungu ninaamini hata hapa nilipo kama cyo yeye nisingekuwepo
 
Ukibadili mazingira unayoishi mfano ukahamia mkoa mwingine, trust me hutaumwa tena.
 
hapa ushauri upo nje nje ,kuumwa kwa mtu mwili mzma kupo ila ungeweka na kazi unazozifanya au mazingira unayoishi ni rahisi sana kupata ushauri hai na wakukusaidia. AHSANTE SANA.
NDANI YA KAZI UNAZOFANYA UTAKUTANA NA HAYA;
UNAPATA MUDA WA KULALA AU KUPUNZIKA?
UNAPATA MUDA WA KULA
KAZI INATUMIA CALORIES KIASI GANI FROM YOUR BODY
N.K
 
icho kipimo ulichobakisha ndo hicho unachoumwa
pata matibabu yake
 
Kunywa maji ya vuguvugu (lita 2) asubuhi kabla hujala kitu chochote, huku ukiendelea kufanya uchunguzi wa afya yako. Vile vile unaweza kutafuta food supplements za kampuni ya TIENS, wakati mwingine katika miili yetu kuna virutubisho hupungua au kuongezeka na hii inaweza kukufanya kujisikia vibaya wakati wote kwani mwili unakuwa unbalanced.
 
Wana jamvi heshima kwenu,
mimi ninaumwa sana mwili mzima lakini kila nikienda hosp. Naambiwa hawaoni ugonjwa nimeshapima vipimo karibu vyote sasa imebakia kipimo kimoja tu lakini kinaniogopesha naombeni tu ushauri kwenu wandugu kabla cjaenda kwa anayefahamu, je kuna madhara yoyote yatokanayo na kupima afya kwa kutumia kompyuta? Maana ndio kipimo nachotakiwa kwenda kupimwa nacho lakini roho yangu inasita sana jamani nisaidieni ushauri tu.

Mungu awabariki

Nenda kapimwe au unaogopa kupimwa ukimwi wewe? Nahisi kama huumwi ki vile maana nilijua mpaka sasa hivi umeshenda kupima hicho kipimo cha computer sehemu tatu tofati. Kumbe hujaenda? Anza maombi ugonjwa utakimbia wenywe. Hakuna lisolowezekana kwa Mungu!!
 
Pole ndugu, mtumaini Mungu kwake hakuna gumu, pia jaribu kwenda kwenye maombi ukaombewe.
 
Siku ukipima hicho kipimo kingne baaaassssssiii unapata ugonjwa unaokusumbua,,,pima tu maana uliyataka mwenyewe...
 
Mkuu pole, "anayekufa hapigi kelele amakufa,mkuu"
anyway, ninashindwa kujua MWILI WOTE UNAUMAJE!!
Unaamaanisha uchovu? Kujisikia vibaya? Homa au?

-Inawezekana ilikuwa ngumu kujua tatizo("ugonjwa") wako ni nini kwa kuwa magonjwa(huanza dalili fulani kisha nyingine, na nyingine na nyingine,..SI RAHISI kwa kusema tu mwili wote unauma kutamvua/kujua kwa urahisi)
-Una miaka mingapi, jinsia?
-Tatizo lako lina muda gani sasa?..Una jishughulisha na nini?
- Ni vipimo gani ulifanya? Wapi, mara ngapi?


Kujibu swali lako, karibu kila kipimo kina madhara..lakini ni ngumu kupata madhara madhara kwa wakati huo huo(immediate)...MUHIMU ni kupima na kujua afya yako.
 
pole nduugu hakuna kipimo kisicho na madhara hata hivyo ulivyokwishafanya vina madhara xo malizia tu kilichobaki maana nahisi ndo kitachokupa jb
 
Uisiogope
Nenda kafanye tu hicho kipimo cha komputer ili ujue mustakabari wa afya yako
Maisha yako ni mungu pekee anayajua endelea kumuomba na kujikabidhi kwake ..
 
Jipe muda wa kupumzika... hayo hata mimi yaliwahi kunitokea. Kila siku naumwa na Malaria, lakini niligundua sipati muda wa kupumzika. Kunywa maji kula pumzika... God is great utapata picha nzuri ya afya yako. Siku hizi wamezidi, simu inatengenezwa kwa kompyuta, redio kwa kompyuta, saa kwa kompyuta, feni kwa kompyuta, kompyuta kwa kompyuta hata mwili sasa unatengenezwa kwa kompyuta. Sio siri watatumaliza na mionzi. Gomesa
 
Muombe Mungu akutie ujasiri,ni rahisi sana,mimi ninapokuwa na jambo nataka kufanya na ninakosa ujasiri,huwa naomba Mungu usiku na asubuhi kwa muda wa siku tatu mfululizo na Mungu huwa ananijaza ujasiri wa ajabu na huwa najikuta hilo jambo nimeliingia kichwakichwa mpaka huwa naanza kujishangaa huu ujasiri nimeutoa wapi,believe in God kila kitu kinawezekana.Acha kuishi kwa mashaka wakati kila kitu Mungu amekuwekea wazi kwa ajili yako ili ufurahie maisha yako hapa duniani.:smile:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom