Msaada jamani Mh. Pinda

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Mheshimiwa waziri mkuu kwa niaba ya wananchi ninaomba utupe msaada wako katika kutatua utata na mkanganyiko uliopo hapa.

Kulitokea mitazamo tofauti kuhusu Zanzibar kama ni nchi au si nchi? Mpaka leo kuna watu hatujajua msimamo halali na dhabiti.

Kwa leo utata na mkanganyiko huko hapa. JE TANZANIA BARA NI NCHI?

Mkuu tunaomba ufafanuzi ili kuweza kumaliza kabisa KIU hii ya kutaka kujua kwani kila siku tunasikia miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara.
 
utata huo utamalizwa na katiba mpya ni moja ya agenda tunapoteza muda kujadili sasa
 
kasome pia katiba ya sasa utapata jibu kama kuna utata jipange kuwasilisha utata huo kwenye katiba ijayo ni kwa ajili ya faida yetu sote
 
Pinda alikuta katiba kama kuna viraka sio yeye wa kutupa jibu bali sisi tumpe jibu pinda kupitia maoni yetu kwenye katiba mpya. Katiba hiyo inakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru ni wakati muafaka kuichanachana kadri tutakavyoona inatufaa sio pinda pekee
 
kasome pia katiba ya sasa utapata jibu kama kuna utata jipange kuwasilisha utata huo kwenye katiba ijayo ni kwa ajili ya faida yetu sote

Mkuu tuelimishane kwanza siyo mwanafunzi anauliza swali alafu mwalimu anampa tena assignment.Naomba uwe mwalimu wetu sasa.Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara bila shaka inamanisha nchi na siyo nyumba au kuku.
Tanzania bara ni nchi ya wapi?mwanangu yuko form two kaniuliza ata jana?Nikamwambia ndo hii,akasema raisi ni nani,waziri mkuu,bunge,mahakama,wizara etc umeme ukakatika leo nikienda nyumbani ataniuliza hivyo hivyo,msaada nisije kuaibika wakuu.
 
Achana na wanasiasa wa CCM hakuna kitu uhuru wa Tanzania bara,tunasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
 
Ukweli siku zote unauma,ila humweka mtu huru.Mtazunguka huku na kule kutafuta jibu,pengine hata kwa kulipigia mstari.Jibu:ZANZIBAR NI NCHI KAMA MADAGASCA,SRI-LANKA n.k.Swala la muungano lipolipo tu kwani na kama la kulazimishana vile.Wana bendera yao,wimbo wao wa taifa,tuache unafic,utazamemi uhalisia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom