Msaada jamani hospital gani nzuri kwa watoto hapa dar?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Nauguliwa na mtoto wa mwaka mmoja na miezi mitatu, anatapika na kuharisha kila akipewa chakula tangu juzi. Nilimpeleka jana kwa dr Koya pale Lumumba wakampa dawa lakini sioni nafuu yoyote na dawa amemaliza!
 
Hapo wanachukua namba asubuhi na kumuona dk jioni (kama unataka kuwaon wale ma specialist- Massawe/Doulla).

Dah hii kidogo itanichanganya maana ninahitaji kama inawezeka nimpeleke jioni hii au asubuhi na afanyiwe vipimo na kuanza matibabu. Sasa nitafanyaje jamani yani mwanangu anaharisha sana, kutapika na kula hataki!!!!
 
mpeleke mwananyamala ndo kuna madokta bingwa wa mambo ya kuharisha na kutapika ...ikibidi wamu operate wacheki utumbo inawezekana una tatizo
 
Mpeleke kwa Dr. Kuboja. Huwa anafanya part-time pale TMJ. Unaweza piga simu TMJ uwaulize ratiba yake na siku anazokuwepo
 
Kuna Dr. Yohani pale mtaa wa Umoja wa wanawake ;jengo ilipo ofisi za QATAR airways , he is the best!!
 
Mimi nakushauri kutokana na uzoefu wangu na watoto. Moja Kama ni kuharisha na kutapika fanya ifuatavyo, kwanza dalili zinaonyesha ni kuota kwa meno.

1. Badala ya kumpa chakula mnunulie matunda na umtengenezee Juice (machungwa na papai)
2. kama dawa amemaliza usimpe dawa nyingine hadi akamilishe mzunguko wa hiyo Juice ya Papai na Chungwa.
3. Mpe maji ya kutosha na kama bado ananyonya atumie maziwa ya mama kama chakula mbadala.

Papai na chungwa ni lishe na dawa tosha kwa mtoto. Usijaribu kumpa hizi juice za dukani au zilizotengenezwa tayari. Hakikisha unakamua chungwa la kweli na papai la kweli. Unaweza mpa Juice ya chungwa pekee na papai peke au unavichanganya pamoja.

Julisha matokeo tafadhali.
 
Pole mkuu...Chemsha maji yakipoa kiasi cha uvuguvugu mpe ntoto anywe......usimwekee Fan au kitu chochote cha kupuliza upepo......then Baada ya saa moja nifahamishe kinachoendelea
 
Nawashukuru sana nawahakikisheni kuufanyia kazi ushauri wenu, mungu awepe baraka zaidi!!!
 
Pole sana. Mimi nimesha zunguka hospital nyingi, mara nyingi huwa swali kama hilo nakushauri uwaulize akina Mama watakusaidia vizuri,kwani sisi akina baba ni wachache ambao huenda na watoto wetu hospitalini.

Nenda pale Kariakoo mtaa wa mafia kuna Dr bigwa wawatoto anaitwa Dr.Koya hapo naaminia ndani ya siku moja utaona utofauti mkubwa. hana gharama kubwa,kwani kumuona ni bure kisha dawa zake bei zake nzuri bajeti yako elf15 na pesa zingine utarudi nazo. Huko TMJ labda kama unatibiwa kwa kadi, otherwise kumuona Dr haiwezi kuwa bure. Nenda kwa Dr Koya naamini utajionea ambako akina mama hupeleka watoto.
 
Mimi nakushauri kutokana na uzoefu wangu na watoto. Moja Kama ni kuharisha na kutapika fanya ifuatavyo, kwanza dalili zinaonyesha ni kuota kwa meno.

1. Badala ya kumpa chakula mnunulie matunda na umtengenezee Juice (machungwa na papai)
2. kama dawa amemaliza usimpe dawa nyingine hadi akamilishe mzunguko wa hiyo Juice ya Papai na Chungwa.
3. Mpe maji ya kutosha na kama bado ananyonya atumie maziwa ya mama kama chakula mbadala.

Papai na chungwa ni lishe na dawa tosha kwa mtoto. Usijaribu kumpa hizi juice za dukani au zilizotengenezwa tayari. Hakikisha unakamua chungwa la kweli na papai la kweli. Unaweza mpa Juice ya chungwa pekee na papai peke au unavichanganya pamoja.

Julisha matokeo tafadhali.

BILA KUSAHAU ORS NI MUHIMU SAAAANA. Pole
 
Back
Top Bottom