Msaada huyu dada wajameni

huyo dada asitoe hiyo mimba ajipange kuwa single mam kwani huyo mwanaume anaonyesha sio muoaji, aanze kutafuta kibarua chochote kwa ajili ya mwanae.
 
Ila kuna watu wengine wanajitafutiaga matatizo wenyewe! Mimba ya kwanza umeona umeambiwa uitoe... asa kwanini ajipeleke tena? afu kavikavu sasa! Kwa mtu mwingine...angeshtuka mapema baada ya kuona kilichotokea mara ya kwanza...au angeachana nae...au angekuwa na msimamo kuwa hakuna kufanya kavukavu tena au hakuna kufanyana tena kbs!
Lakini asitoe hiyo mimba...na kama yuko kwa jamaa basi amgande.. na awe makini naye asije akamuwekea kitu kibaya kwenye chakula au kinywaji thn ikawa balaa juu ya balaa...!
Kuna siku mshikaji mmoja alikuwa anampeleka mwanamke wake kutoa mimba nikamuuliza hivi unajisikiaje akanijibu "Sasa nitafanyaje" nikamwambia wakati mnafanya bila kinga hamkuwa makini akanijibu "Ajali Kazini" nilichoka kweli
 
Kwa kweli nadhani huyu dada atakua ana tatizo kisaikolojia na inawezekana limeanzia kwenye hiyo familia yao! Atafutiwe mwana saikolojia ili aweze kumpa msaaada, maana katika hali ya kawaida mtu mwenye akili timamuhuwezi kufanya hivyo.

Asiitoe hiyo mimba maana itazidi kumpa wakati mgumu! Pia, kama wadu walivyo comment, inaelekea jamaa hamjali na ndio maana anamuambia atoe mimba hovyo hovyo! Maana mi naamini huyo mwanaume angekua anajali basi angelazimisha kutumia kinga ili asimtundike mimba nyingine. Kwa vile ameona binti ni mdhaifu anatumia huo mwanya kumkandamiza.

Pia binti asilazimishe penzi, mtu mwenye nia na wewe hatasubiri kulazimishwa akajitambulishe, atafanya hivyo bila kushinikizwa hapo hamna mapenzi kabisa!
 
Back
Top Bottom