Msaada hapo tutani jamani wana MMU!

Sabry001

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,064
353
Nina rafiki yangu tuko wote hapa chuoni, amenijia ako na tatizo linamtatiza na anahtaji ushauri.
Tatizo: Alikuwa na mwanaume ambae walikaa ktk uhusiano kwa mwaka na miezi km minne hv. Ktk kipindi hicho walikuwa wanagombana na kupatana km ilivyo ada ya wapendanao. Mwezi February mpenzie alikuja kumtembelea pia ikiwa ni kuja kusuluhisha ugomvi uliokuwa baina yao. Anasema walisuluhisha then walifanya mapenzi ila cku chache bdae aliamua kuachana jumla na yule kaka maana mambo yalirudi kuwa worse. Sasa baada ya kuachana na yule kaka jambo moja limetokea, she is pregnant! Anafikiria kumwambia yule kaka lakini hana pa kuanzia kwani kuna mambo mengi yalijitokeza walipoachana. Yule kaka alimtumia msg za kumkashfu huyu dada akimwambia yeye dada ni kichaa na ni muuaji wa wanaume. Yule dada nae alimpasha yule kaka kwa kuwa weak, irresponsible and betrayer. Sasa amenijia anataka nimpe ushauri, kwanza anataka amuambie yule kaka, pia anapanga autoe ujauzito. Mimi km mimi nimepima maji kwa kweli ni marefu kwamba
1. That guy hampendi yule dada so
2. Anaweza kuikataa mimba kwa vile walishatengana na pia
3. Abortion ni hatari na dhambi juu ya dhambi.
So nimebaki ktk dilema nimshauri lipi ili bdae nisibebe mzigo wa lawama?
Najua hapa MMU kuna watu wenye upeo mkubwa so nitapata mawazo tofauti tofauti toka kwenu! KARIBUNI kuchangia.
 
Amwambie NA asitoe mimba hata kama akikataa toka nizaliwe sijaona mtoto kafa kwa kukosa baba!mtoto asilipie makosa ya wazazi ya kutoepuka ngono zembe
 
Haya ngoja wanawake waje kwani ndo umesema ndo wanatakiwa watoe ushauri!
 
Ajifungue tu kwa kitanda hakizai haramu.
Na akizaa haimaniishi kutakuwa na commitment na baba wa mtoto.
Kutoa mimba ni ukatili wa hali ya juu
OTIS
 
Cjaspecify kwa wanawake we Eiyer! Nimesema watu wote.

Ok,kwanza ni lazima amwambie mwenye ujauzito kama haki yake ya mwenye ujauzito kujua,but sio amwambie kwa lengo la kupata sapoti yoyote,yeye atoe taarifa tu.Awe mwangalifu na huyo jamaa ujauzito usijekuwa kigezo cha kumsumbua huyo dada!
 
Mwanamke hasingiziwi mimba - Mpoki.

Azae, mwanachuo mzima anaogopa mimba? Darasa la saba wenyewe wanazaa sembuse huyo?
 
Ok,kwanza ni lazima amwambie mwenye ujauzito kama haki yake ya mwenye ujauzito kujua,but sio amwambie kwa lengo la kupata sapoti yoyote,yeye atoe taarifa tu.Awe mwangalifu na huyo jamaa ujauzito usijekuwa kigezo cha kumsumbua huyo dada!

sa ulikuwa unabania ushauri wa nini?
 
naona masuala ya kinga huwa yanashadidiwa JF tu, lakini tukiwa faragha ni mambo mdundo tu...
 
Ajifungue tu kwa kitanda hakizai haramu.
Na akizaa haimaniishi kutakuwa na commitment na baba wa mtoto.
Kutoa mimba ni ukatili wa hali ya juu
OTIS

Umeongea km wamfaham that guy! He is so irresponsible kwa kweli so hatutarajii kujicommit kwake ktk malezi.
 
Wao ndio wanamakosa, hayamuhusu huyo kiumbe alioko tumboni, pia kutoa mimba sio dhambi tu bali kunaweza kumgarimu hata maisha yake...

Nadhani amwambie tu kama muhusika wa hyo mimba pasi na kujali tofauti zao, then atunze mimba ...
 
hakuna haja ya kujifikiria wa la kujilaumu, mwambie atunze mimba maana ndo kitu pekee alicho a uwezo nacho.. mahusiano huja na kupotea mtoto si wa kubahatisha . cha msingi amwambie mhusika basi ajitulize
 
ASIITOE hiyo mimba na amweleze huyo mkaka no matter what mtoto ni wa kwake. Hata akiikataa haijalishi tena mtahadharishe kabisa huyo best wako kuwa mkaka anawezaikataa so ajiandae kisaikolojia. Mwenyewe atajamtafuta mwanae ukubwani.
 
Asanteni kwa micango yenu mizuri na nimeshaifikisha kwa muhusika hope atayatekeleza! Muwe na wkend njema
 
Daaa kama ni ndogo atoe tu ila kuanzia miez minne aache ila itakuwa vigumu msela kukubali mzigo huo. Kama mliachana kwa namna hiyo unalo dada
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom