Msaada - Gharama za ujenzi/ukarabati!

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
128
Kwa wale walioko nyumbani ambao wako kwenye fani ya ujenzi au kwa wale wenye uzoefu na shughuli za ujenzi. Tafadhali ninaomba makadirio ya ukarabati ufuatao:

Ninajaribu kufanya makadio ya ukarabati wa nyumba moja utagharimu kiasi gani. Na kuweza kufanya hivyo, nitahitaji kujua bei ya materials na labor.

Mfano:

Nyumba (ya matofali) yenye 1600 square meter ina matatizo yafuatayo:
  • Sehemu ya bati imechakaa, ina kutu, na inavuja.
  • Haija sakafiwa
  • Kuta hazisawazishwa na kupakwa rangi
  • Hamna choo na bafu la ndani
  • Maji hayajavutwa ndani
  • Madirisha hayana net ya kuzuia mbu

Ninahitaji kujua makadirio ya gharama yatakayowezesha matatizo yote hapo juu kutatuliwa. Ninatafuta gharama za materials na labor.

Kwa haraka haraka nitahitaji bei za materials yafuatayo (katika Tshs.)

Kuweka bati mpya
  • Bati moja
  • Mbao moja ya kushikizia bati
  • Misumari ya bati (kilo 1)
Kuweka Ceiling board
  • Ceiling board per square meter
  • Mbao za kuunganishia (??)
  • Gundi ya kuunganishia (??)
Sakafu na kuta
  • Mchanga lori moja
  • Seruji mfuko mmoja
  • Rangi ndoo moja (maji na mafuta)
  • Kokoto lori moja (??)
Choo na bafu
  • Bomba la choo la kupitishia ushafu
  • Kiti cha choo
  • Sink la kufurashi
  • bomba la kuogea
  • Sink la kuogea
Maji
  • Gharama za kuvuta maji
Madirisha
  • Bei ya dirisha moja na neti yake
Na mwisho kabisa, kadirio la gharama ya labor kwa kufanya kazi yote hiyo.
Any help would be greatly appreciated.
 
I can help... Ila frankly speaking 'Labour only' works sucks!

Check with me on Monday. Halafu it could be healthier if you could send me a PDF format plan or Structural & architectural drawings. From there nitakupa bei.

Remember, nifahamishe nyumba hiyo ni Dar au mikoani? Na kama ni mikoani basi nifahamishe ni Arusha au Mwanza ama Kigoma.

Pia, refurbishment works zina utofauti mkubwa kulingana na extent ya jengo husika. Itapendeza ukanitumia picha za jengo hilo nilifanyie upembuzi juu ya nini kinahitajika na hukukiweka katika maelezo yako. Itanirahisishia hata kama nakupa rough estimate iendane na uhalisia wa kitu chenyewe. Epuka wanaosema ni roughly $250 au $400 kwa square metre, lazima mtu ajue extent ya ubovu wa exisisting building.

My email & phone number are on my signature.

Ningefurahi ningekupa bei detailed including na materials supply ili kama unatumia contractor iwe rahisi ku-judge wapi ulalie na kama unatumia deiwaka basi ujue wapi uanzie na ukabiliane naye vipi.

Mac
 
Thanks Max.

Check your PM kwanza...then email....:)
 
Back
Top Bottom