Mrithi wa REGIA ni Cecilia Paresso

chadema kimejipanga vyema,makamanda wote wako mstari wa mbele,mwanzo mwisho.
 
Yule mwanamke alikuwa Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Chadema aliyeikimbia Chadema na kwenda NCCR kwa kukosa ubunge wa kuteuliwa angekuwa na subira leo angeingia mjengoni Dodoma maana nasikia ni jina lililokuwa linafuata katika orodha, mambo mengine papara unakuja jutia baadaye.
 
Politicians are all the same, JK (CCM), Mbowe (CHADEMA), Lipumba (CUF), Mbatia (NCCR-Mageuzi), Cheyo (UDP), Mtikila (DP), Jahazi Asilia, (Kuga) APPT Maendeleo, etc.. They are the same passengers in different vehicles! So it is a technucal mistake to expect miracles from any of these for the mistakes done by any of them.
 
naomba kuuliza wakuu,hivi inapotokea ishu kama hii uteuzi unafanywa na chama husika au na tume ya taifa ya uchakachuaji,aaaaaaaaaaaahh,samahani uchaguzi.
 
Wanazidi kutudhihirishia kuwa hiki chama ni cha watu wa KASKAZINI!!!

Kila chama kina taratibu zake, kama alikuwa after RED LINE hakuna tatizo, nyie watu wa pwani mnataka mcheze mduara then mpate ubunge kirahisi
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mwanamke aliyeshika nafasi ya 26 katika majina 102 yaliyopelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), mwaka 2010 kwa ajili ya kufanyiwa uteuzi wa ubunge wa viti maalum, ndiye atakayemrithi marehemu Regia Mtema, aliyefariki dunia wiki iliyopita. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willibrod Slaa, alisema hayo alipotakiwa na NIPASHE kutoa ufafanuzi kuhusu nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha marehemu Regia. Habari zilizopatikana kutoka makao makuu ya Chadema, zinaeleza kuwa mwanamke aliyeshika nafasi ya 26 katika majina 102 yaliyopelekwa Nec, mwaka 2010 kwa ajili ya kufanyiwa uteuzi wa ubungewa viti maalum, ni Cecilia Daniel Pareso.

Cecilia ni Diwani wa Kata ya Qurus, iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha. Habari nyingine zinaeleza kuwa awali, mwanamke aliyekuwa akishika nafasi ya 26 ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Leticia Mosore, ambaye baadaye alihamia chama cha NCCR-Mageuzi. Dk. Slaa alisema utaratibu wa kuwapata wabunge wa viti upo wazi kwa mujibu wa sheria na kwamba Chadema hawana mamlaka ya kuongeza wala kupunguza kitu chochote. Alisema Chadema imeishamuandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumuarifa rasmi kwamba kuna nafasi iliyo wazi, ambapo naye ataiandikia barua Nec kwa ajili ya kufanya uteuzi rasmi.

Dk. Slaa alisema kuwa kama kutakuwa na mabadiliko ya mtu aliyeshika nafasi hiyo ya 26, ikiwamo mtu huyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge kwa kuhama chama ama kuonekana na upungufu mwingine ambao unamnyima sifa, Chadema itaiandikia barua Nec ili achukuliwe mtu mwingine aliyeshika nafasi ya 27. Alisema kama namba 26 na 27 wote hawatakuwa na sifa, Nec itachukua jina litakalofuata namba 28 ili kufanya uteuzi wa kiti hicho.

"Sisi kwa hili tulishalimaliza mwaka 2010 na tunachoweza kufanya kwa Nec ni kuisaidia itakapotaka maelezo yetu juu ya jina linalotakiwa kufanyiwa
uteuzi," alisema Dk. Slaa. Alisema mwaka 2010 walifanya kazi kubwa na kupata majina 102 ambayo yote yana sifa za kuwa wabunge wa viti maalum na kwamba, Nec ndiyo yenye mamlaka yote ya mwisho na sio Chadema. Chadema kina wabunge wa viti maalum 25 katika Bunge la 10.
 
Sasa wewe unataarifa za uhakika halafu unaombe ssis tukupe cv yake?

SnS mi nashangaa, kuna watu humu huwa siwaelewi na mmoja wapo ni huyu mtoa sredi!!! Yeye ndo kaleta habari halafu anatuomba sisi CV, kwa nini hakufanya hiyo home work yake ndo alete tumjadili!!!

Bana eeh, mi sina cha kuchangia maana habari ni kama uzushi tu!!! Fanya hoework yako njoo tuongeee kama GT!!
 
Sina tatizo hata kidogo hata kama wabunge wote watatoka familia moja. Cha muhimu kwangu ni uwezo wa mbunge huyo. Ana sifa za kuwa mbunge? anafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi? ni mbunifu katika kutatua matatizo ya wananchi? Nadhani haya ndio muhimu ya kujadili badala ya kuangalia mahusiano au eneo analotoka kiongozi.

Sijui ni lini hii tabia imeanza lakini ni makosa makubwa sana kuteua viongozi kwa kuangalia maeneo, dini, etc? Kwenye baraza la mawaziri kuna watu ambao hawafai hata kuwa balozi wa nyumba 10 lakini inashangaza wamepewa Wizara nzima!

Kama kweli Bi Cecilia ameteliwa kuwa mbunge na hata kama ni kweli ana mahusiano na kiongozi yoyote hilo lisiwe hoja. Afanye kazi za uhakika, basi. And if it take a single familiy rather than 50 families to fix this country let it be.
 
Mh...hongerakamanda;Lakini Dr,hivi wana CHADEMA Ifakara hawapo?
Ni vema kujiepusha na lawama toka kwa magamba kwa kuhakikisha si tu haki inatendeka,bali inaonekana kuwa imetendeka
 
Wanazidi kutudhihirishia kuwa hiki chama ni cha watu wa KASKAZINI!!!

Kama ni kweli Hongera zake!

Wewe ulitaka atoke wapi kama siyo kusini, mashariki, kaskazini, kati au magharibi? labda mbinguni.
Tunaamini CDM siyo wazembe kihivyo lazima wana vigezo na ni kwa kutumia hivyo wamempata.

Huku twendako uteuzi utabidi uwe unapelekwa kwa jopo la malaika for vetting kwani kila mtu anatoka mahali na ni ndugu wa mtu.

Songa mbele mteule
 
Kumbe hujui chama kinawenyewe hv watamteuje wa nam2mbo wakati hana nasaba na kaskazin,kaz ipo
 
Azimio la Arusha- Kaskazini
Headquarter of EAC -Kaskazini
UN ICTR- Kaskazini
TANAPA HQ - Kaskazini
NA UKOMBOZI WA TANZANIA UTAANZIA KASKAZINI

Wanazidi kutudhihirishia kuwa hiki chama ni cha watu wa KASKAZINI!!!
 
Sina tatizo hata kidogo hata kama wabunge wote watatoka familia moja. Cha muhimu kwangu ni uwezo wa mbunge huyo. Ana sifa za kuwa mbunge? anafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi? ni mbunifu katika kutatua matatizo ya wananchi? Nadhani haya ndio muhimu ya kujadili badala ya kuangalia mahusiano au eneo analotoka kiongozi.

Sijui ni lini hii tabia imeanza lakini ni makosa makubwa sana kuteua viongozi kwa kuangalia maeneo, dini, etc? Kwenye baraza la mawaziri kuna watu ambao hawafai hata kuwa balozi wa nyumba 10 lakini inashangaza wamepewa Wizara nzima!

Kama kweli Bi Cecilia ameteliwa kuwa mbunge na hata kama ni kweli ana mahusiano na kiongozi yoyote hilo lisiwe hoja. Afanye kazi za uhakika, basi. And if it take a single familiy rather than 50 families to fix this country let it be.

Jk alipomtumia Ridhwan na mama Salma mbona maneno matamu kama haya sikuyasikia?
 
Kumbe hujui chama kinawenyewe hv watamteuje wa nam2mbo wakati hana nasaba na kaskazin,kaz ipo
 
Back
Top Bottom