Mrithi wa Dr. Mponda mnamjua??

Sidhani kama waliobuni huu uwanja walikusudia pawe mahali pa mizaha. Ila kwa wanaopenda mizaha kuna mahali pake humu jamvini!!!????

kama prof angekuwa sio mbunge au sio wanachama wa CCM, basi huo ndio ungekuwa mzaha.
 
Mbona nimesikia ni Babu wa Loliondo? Mh. raisi bado ana nafasi ya viti maalum
 
Nimetumiwa CV ya Prof. Maji Marefu kutoka kwa mpiga kura wake ambaye hakutaka jina lake litajwe ili asije wehuliwa na Mb huyo. Nayo iko hivi:
Jina kamili: Steven Hilary Ngonyani a.k.a Prof. Maji Marefu
Alikozaliwa: Shamba Kapori, Mruazi Kata ya Mnyusi, Wilaya ya Korogwe
Asili yake. Mngoni. Wazazi wake walikuja kama Manamba Mashamba ya Mkonge.
Elimu: Aliishia darasa la 4 kwa kukosa ada ingawa anadai kafika darasa 7
Uzoefu wa kazi: kulima miraba mkongeni, kucheza goroli, kupiga ndege kwa manati, kuchezesha mazingaombwe hasa shule za msingi.
Dini: Mkristo lakini ana wake 4.
Kiini cha kuchaguliwa: Kumwaga pesa kwa zaidi ya miaka 3 kabla ya uchaguzi, kugharimia mazishi na shereha kabla ya uchaguzi.

Yajapo mengine nitawajuza.
 
Ingawa umefanya UTANI lakini kwa JK kila kitu kinawezekana, ila mimi najua ni Dr Faustin Ndugulilek
 
Mwanangu katafute la kufanya kuliko huo mchezo unaoanza wa kufinyanga mambo. Maji Marefu anaweza kuwa waziri wa ushirikina na ramli lakini si afya.
 
Back
Top Bottom