Mrisho Ngassa ajiunga na Mbeya City

Duuuuh sasa ukweli ndio upi?Naona watu wanatukanana tu hapa.
Ukweli ni huu hapa.... Baada ya kutoka Free State Ngassa akaenda UARABUNI KLABU YA FANJA..... Sasa kama kasajiliwa na Mbeya City mtoa post anatakiwa aseme KATOKEA FANJA KWENDA MBEYA CITY SIO KATOKEA FREE STATE.... TATIZO WANAMUAMINI MNO KUMWEMBE KILA ANACHOPOST WANAOKOTA KAMA KILIVYO WANALETA..... NGASSA NI MCHEZAJI WA FANJA FC....
 
Attachments

  • Screenshot_2016-11-30-18-34-41.png
    Screenshot_2016-11-30-18-34-41.png
    48.1 KB · Views: 41
Ukweli ni huu hapa.... Baada ya kutoka Free State Ngassa akaenda UARABUNI KLABU YA FANJA..... Sasa kama kasajiliwa na Mbeya City mtoa post anatakiwa aseme KATOKEA FANJA KWENDA MBEYA CITY SIO KATOKEA FREE STATE.... TATIZO WANAMUAMINI MNO KUMWEMBE KILA ANACHOPOST WANAOKOTA KAMA KILIVYO WANALETA..... NGASSA NI MCHEZAJI WA FANJA FC....
Mkuu una undugu na Ngassa sio kwa povu hilo
 
Mkuu basi subir mzunguko wa pili uje ufute hizi comments zako

Azifute kwa nini?

Hajakataa swala la Ngassa kuhamia Mbeya City, anachokikataa ni taarifa ya kwamba ametokea FREE STATE kuja Mbeya City, currently yuko Fanja FC, so kama ni kuhama anatakiwa awe ametokea FANJA FC.
 
Sisi huwa hatuna tabia ya kujituma na kukaza mkwiji mpaka tuvuke...
 
Inawezekana ni kweli...

DONEDEAL: Ngasa kasaini Mbeya City
By Dick Dauda - November 30, 2016
Facebook Twitter

ngassa-mbeya-city

Picha inayo-trend kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni ya Mrisho Ngasa na afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten ambayo inaashiria tayari nyota huyo wa zamani wa Yanga ameshakamilisha deal na ‘wagonga nyundo wa Mbeya’ Mbeya City.

Mwezi Septemba mwaka huu Ngasa alijiunga na Fanja FC inayoshiriki ligi kuu nchini Oman (Oman Professional League) ikiwa ni wiki tatu tu, baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Free State Stars ya South Africa.

Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Kagera Sugar, Yanga, Azam FC na Simba vyote vya VPL hajadumu Oman na hatimaye amerejea tena nchini na kusajiliwa na klabu ya Mbeya City ambapo ataungana na kocha wake wa zamani Kinna Phiri aliyemsajili kutoka Yanga kwenda Free State Stars kabla ya kocha huyo kutimuliwa kufatia mfululizo wa matokeo mabovu.

Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten ame-post picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa pamoja na Mrisho Ngasa na kuandika maneno yanosomeka: “Mnapokamilisha jambo kutakiana heri ndio uungwana. Kila la heri anko @mrisho_ngasa_17.”

ngassa-mbeya-city-1

Habari za Ngasa kujiunga na Mbeya City zilianza tangu aliporejea nchini akitokea South Africa baada ya kuvunja mkataba na Free State lakini ghafla akaibukia Oman na kusajiliwa na Fanja FC siku chache baada ya klabu hiyo kumsajili mtanzania mwingine Danny Lyanga mshambuliaji wa zamani wa Simba.

Jana jioni zikaenea tena habari kwamba Mbeya City wameshakamilisha usajili wa Ngasa. Lakini uongozi wa klabu hiyo haukuwa tayari kuthibitisha badala yake ukasema utatoa taarifa rasmi, mwisho wa siku raundi ijayo ya VPL Ngasa atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaokipiga Mbeya City.
 
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba yeye ni mchezaji halali wa Fanja ya Oman na alirejea nyumbani kwa ruhusa maalum.
Aidha, Mrisho Ngassa ameshangazwa na habari kwamba yeye amesaini Mbeya City na akasema alikutana na Ofisa Habari wa timu hiyo, Dismass Ten katika mazungumzo ya kawaida na haikuhusu usajili.
“Alinipigia simu Ofisa Habari wa Mbeya City, tunafahamiana. Tukakutana kwa mazungumzo na kupiga picha tukiwa kwenye mgahawa. Baada ya hapo tukaachana, sijasaini Mbeya City,”alisema.
Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba yeye ni mchezaji halali wa Fanja ya Oman na alirejea nyumbani kwa ruhusa maalum
Ngassa alisema kwamba yeye kama mchezaji soka ni ajira yake na anaamini anaweza kucheza popote wakati wowote, lakini haipendezi kuandikwa mambo ambayo si ya kweli juu yake.
“Inakuwa vizuri inapoandikwa nimesaini timu, wakati nimesaini kweli. Lakini si kusema nimesaini Mbeya City wakati sijasaini. Naiheshimu Mbeya City. Ni timu nzuri na napenda kuichezea siku moja hususan kwa sababu kocha wao, (Kinnah Phiri) nimewahi kufanya naye kazi. Lakini itakuwa vizuri iandikwe nimesaini wakati nimesaini. Kwa sasa napenda ieleweke sijasaini,”alisema.
Mchezaji huyo wa zamani wa Azam, Simba na Yanga amesema tayari amekwishakamilisha kilichomrudisha nyumbani na sasa anasubiri kutumiwa tiketi arudi kazini Oman.
“Mimi nilikuja huku kwa ruhusa maalum kwa ajili ya mambo ya kifamilia. Na baada ya kukamilisha mambo yangu, nimewatumia taarifa Fanja ili wanitumie tiketi nirejee kazini, kwa hiyo ninawasubiri wao,”alisema Ngassa.

Source: binzubeiry
 
Mi mwenyewe nashangaa aje city afanye nini, kule Oman analipwa ma-Rial :D
 
Kweli mrisho Ngasa kaisha habari yake kutoka afrika kusini mpaka Mbeya city wachezaji wa Tanzania we acha tu
 
Back
Top Bottom