Mrisho Ngasa 'kucheza marekani'....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Hivi kuna mtu yeyote wa kuniambia
ile taarifa kuwa Ngasa kafaulu majaribio
huko maerekani
na atakwenda January imeishia wapi?
naona sasa ni April kama sikosei na Ngasa yupo tu Azam anaendelea...

what happened?....
 
Hivi kuna mtu yeyote wa kuniambia
ile taarifa kuwa Ngasa kafaulu majaribio
huko maerekani
na atakwenda January imeishia wapi?
naona sasa ni April kama sikosei na Ngasa yupo tu Azam anaendelea...

what happened?....

Ndugu yangu waTanzania utawaweza kwa maneno? Ngoja tusubiri wenye data zaidi watujuze.
 
ni vema wakala wake aseme ukweli, kwa maana tulisubiri sana kmwona mTz Ngasa akipiga soka USA, Hata kama hii imeshindikana nakutakia kila la kheri Ngasa na wachezaji wengine wa Kibongo. ila nidhani ni kitu muhimu ktk kukufikisha ktk malengo even more than matarajio yetu
 
Nadhani yuko kwenye mipango ya kuoa mke mwingine baada ya yule wa awali kushindwana.......ukumbuke kama Ngasa ni mtu wa maendeleo ya mpira basi mafanikio yake yalikuwa ni Uingereza maana Zola alimwambia arudi Tanzania ajenge stamina halafu atamchukuwa lakini kwa mshangao wa wengi aliporudi Bongo Priority yake ilikuwa ni kuoa mke. waache waendelee kuvuta bangi tu hawana future hawa wachezaji wetu nadhani mnakumbuka ya Haruna Moshi Boban.
 
[h=3]NAFASI YA NGASSA SEATTLE SOUNDERS YACHUKULIWA NA MKONGO - AAMBIWA AENDELEE KUSUBIRI.[/h]
ngasssa.JPG





Hatma ya mchezaji wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC Mrisho Ngassa kwenda kujiunga na timu ya Seattle Sounders imejulikana leo baada ya blog hii kuongea na Rahim Zamunda mmiliki wa African Lyon na mtu aliyehusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha Ngassa kwenda kufanya majaribio nchini Marekani mwaka Uliopita

Z_IMG_0550.jpg

"Ni kweli Ngassa hakuweza kujiunga na Seattle Sounders kwa sasa baada ya nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine ambaye anacheza nafasi kama ya Ngassa uwanjani. Mcongo huyo nae alifanya majaribio na Seattle akafanya vizuri na kocha akapendekeza yeye ndio achukuliwe kwanza kabla ya Ngassa, ambaye ataendelea kuangaliwa kwa ukaribu na itakapotokea nafasi nyingine atachukuliwa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Marekani. Hiyo ndio hali halisi ya mambo yalivyo katika sakata la Ngassa kwenda kucheza Seattle Sounders." - Alimaliza Zamunda.
 
Hivi kuna mtu yeyote wa kuniambia
ile taarifa kuwa Ngasa kafaulu majaribio
huko maerekani
na atakwenda January imeishia wapi?
naona sasa ni April kama sikosei na Ngasa yupo tu Azam anaendelea...

what happened?....

OCHA wa Azam FC, Stewart Hall
amekanusha taarifa kuwa kiungo wa timu
hiyo, Mrisho Ngassa alifuzu majaribio ya
kucheza soka la kulipwa aliyoyafanya
mwaka jana nchini Marekani katika klabu
ya Seattle Sounders.
Ngassa ambaye alipata nafasi ya kucheza
dhidi ya Manchester United alipokuwa
kwenye majaribio hayo, ilielezwa kuwa
amefanya vizuri na angeitwa kufanya
mazungumzo juu ya kusajiliwa mwishoni
mwa msimu uliopita.
Akizungumza na Championi Ijumaa,
Stewart alisema wenyeji wa Ngassa katika
majaribio hayo walifurahishwa na
kiwango kilichoonyeshwa na winga huyo
lakini hakuwa na ubora wa kucheza katika
Ligi Kuu ya Marekani.
"Nilishangazwa na taarifa zilizokuwa
zimeenea mara baada ya Ngassa kumaliza
majaribio yake, hakufuzu, kilichotokea ni
kwamba walimsifia kwa kiwango
alichoonyesha katika mazoezi waliyompa,"
alisema Stewart na kuongeza:
"Ukiangalia Ngassa anatoka katika ligi
yenye ubora mdogo ukilinganisha na ile ya
Marekani, jambo ambalo lingemlazimu
kufanya kazi ya ziada ili kuweza kufikia
kiwango cha kucheza ligi hiyo.
"Nadhani hilo pia ndilo lililosababisha
acheze chini ya kiwango katika msimu huu
wa Ligi Kuu ya Bara kwa kuwa bado
alikuwa na ndoto za kwenda kucheza soka
la kulipwa nje."
Viongozi wa Azam FC, waliwahi kusema
Ngassa alifuzu baada ya kucheza katika
mechi ya kirafiki ya Seattle Sounders dhidi
ya Manchester United ya England.

Chanzo: Gazeti la Champion Ijumaa
 
Back
Top Bottom