Mrisho Gambo aongea na wanahabari

Ngoja kijana amwage radhi kwanza. Utasikia moto wake baada ya hapo. Vijana wamechoka na ubabaishaji huu. Utamsikia tu Nape, na wengine wengi saaana sasa watajitokeza hadharani.

nape tangu apewe ukuu wa wilaya ametulia tuli kule bonden....
 
mrisho kweli amejitoa mhanga na anastahili pongezi na kuungwa mkono na vijana wote katika vita dhidi ya mafisadi. hakika muda umefika kwa watz kuacha kufanya kazi za watu na badala yake kufanya kazi ya umma.
 
Mara ya kwanza nilidhani viongozi wa vyama vya upinzani wangeishinikiza Serikali iwapeleke Mafisadi ktk mkono wa sheria, lakini kwa mshangao nikasikia kuwa nao wameishanunuliwa. Nilipofuatilia kwa ukaribu nyendo zao nikakubaliana na aliyeniambia kuwa wamenunuliwa, kwani kila ukisikia wanakemea Ufisadi basi wao humtaja Rais Kikwete huku wakijua wazi kuwa wanaolitafuna Taifa hili ni akina nani.

Kama kweli wanawatetea watanzania basi wajitokeze kwa staili yao ile ile wawabomoe Mafisadi kama alivyofanya Reginald Mengi. Bila ya kufanya hivyo, basi tutaendelea kuamini kuwa mumenunuliwa na Mafisadi kama inavyofahamika huku mitaani.
 
Baraza la Mkoa wa Pwani lilitoa tamko lake. Wakasakamwa saaana, kama vile mbwa aliyeiba mboga za wageni. Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Hon. Pius Msekwa akaliweka sawa, kuwa walichosema UVCCM Pwani hakijakiuka taratibu na kanuni za Chama. Haya ya Mrisho Gambo yanatokea wapi? Nampongeza sana M/Kiti wa UVCCM Pwani kwa msimamo wako thabiti ktk kulitetea Taifa hili. Usibabaishwe na mjinga yeyote anayewaza kwa kutumia tumbo na sio akili.

Mwisho wa watu wa namna hii upo karibu sana kwani hawawezi kushindana na nguvu ya Umma.
 
Thanx, tujuze mkuu... But al n al bora atangaze kuhama tu... Atue cdm tupge kazi

Chadema ya sasa iko imara na imejitosheleza. Hatutaki tena mazagazaga yaliyonyimwa fursa ya kufisadi ndani ya ccm.

Tumeona kupitia Shibuda kwamba it if difficult to unlearn the ccm culture and behavior. Tumeona pia kupitia makamanda wapya wa Chadema bungeni kwamba upya hauna ufisadi na tamaa kama wazoefu
 
Kama kweli UVCCM wanakitakia mema Chama chao na nchi kwa ujumla, basi wajitokeze na kutamka hadharani kuwa hawakubaliani na Ufisadi. Baada ya hapo wawataje Mafisadi hao kwa majina na nafasi zao ktk Chama, na kuwataka waondoke ktk Chama ili watu wafanye kazi za kujenga nchi badala ya kutumia muda mwingi kuchekea "upumbavu" ndani ya Chama.

Tualitaka hili lifanyike pia kwa CCM wenyewe. Kwanini munaoneana haya wakati munaangamia? Munategemea nini? Yaani Chama na nchi viangamie kwa sababu ya watu wachache saaana? Nani kasema maneno hayo? Wakati wa mageuzi ndani ya CCM ni sasa.

Mkuu wangu Chechetuka umeisemea mioyo ya mamilioni ya watanzania wenye mapenzi mema na uchungu wa dhati kwa nchi hii. Mamilioni yanayoiona nchi hii inavyogeuzwa kuwa mradi wa wenye uroho wachache ambao kila siku wanapanga njama za kudhuru maisha na hadhi za wale wote wanaopinga udhalimu wao. Kwa kweli UVCCM wana changamoto kubwa na relevance yao kwa umma iko katika namna watakavyolijibu hili na kama ulivyosema katika hili jicho liko kwa Benno Malisa maana Shigela ana madeni ya kulipa kwa mafisadi hasa baada ya kupokea landcruiser yake kama ujira kwa mema anayoendelea kuwatendea, bila kujali kwamba hao hao ndiyo walimpikia zengwe alipokuwa anateuliwa, mpaka ikafikia hatua ya kutaka Kamati Kuu ya CCM ipeleke majina mawili NEC ili yapigiwe kura kusudi Shigela ashindwe katika kura.

Mimi nasema Gambo Mungu yuko pamoja na wewe na watanzania kwa mamilioni wankuunga mkono. Hila za kukufukuza kwenye jumuiya na hata zile za kukufukuza chuoni Nelson Mandela na sasa kule Manispaa zinafahamika, wanaoratibu wanafahamika , lakini Mungu yuko nawe. La msingi elewa kwamba mengi makubwa yatatengenezwa dhidi yako, lakini kama Nape Nnauye alivyoyashinda, wewe pia utayashinda. Hata Ulega naye anaendelea kupokea vitisho kutokana na matamshi yake kwenye mkutano wa UVCCM Pwani. Aluta continua Gambo!
 
Mara ya kwanza nilidhani viongozi wa vyama vya upinzani wangeishinikiza Serikali iwapeleke Mafisadi ktk mkono wa sheria, lakini kwa mshangao nikasikia kuwa nao wameishanunuliwa. Nilipofuatilia kwa ukaribu nyendo zao nikakubaliana na aliyeniambia kuwa wamenunuliwa, kwani kila ukisikia wanakemea Ufisadi basi wao humtaja Rais Kikwete huku wakijua wazi kuwa wanaolitafuna Taifa hili ni akina nani.

Kama kweli wanawatetea watanzania basi wajitokeze kwa staili yao ile ile wawabomoe Mafisadi kama alivyofanya Reginald Mengi. Bila ya kufanya hivyo, basi tutaendelea kuamini kuwa mumenunuliwa na Mafisadi kama inavyofahamika huku mitaani.

Hili la kununuliwa na ukimya wa wapinzani na mimi sasa linaanza kuniingia na staili hii ya kizamani ya kipolisi ya kulinda ubungo na huku wakijua ujambazi utafanyikia magomeni sasa inatuonyesha kwamba kuna jambo. Hawa hawana ujasiri wakusema wazi kwamba mafisadi ni kina nani kwa vile wanajua kwamba kuna mshiko ambao baadhi yao wanaupokea kutoka kwa mafisadi ili kukaa kimya na kuuyumbisha ufisadi. Matokea yake wako bize kumtukana Rais wetu ambaye hana hata doa la ufisadi. Hao hao mafisadi sasa ndiyo wanashirikiana nao kutoa majarida ya kuwasafisha na hata kutumia magazeti yao kuwasafishia njia ya kuelekea ikulu na wakati huo huo kuwachafua walio wasafi. Nashangaa walivyokaa kimya pale tuhuma za Dr. Mwakyembe kuuawa na wakijua kwamba hata Dr. Slaa naye yumo kwenye orodha. Hawa hawa ndiyo wanaruhusu magazeti yao yamdhihaki mzee Mengi katika kesi yake iliyofunguliwa na mafisadi pale alipoujulisha umma viwavi jeshi wa uchumi wao.

Mimi nasema Ulega, Makonda, Gambo na wengine ni watu ambao nchi hii inastahili kuwaenzi kwa kufanya lile ambalo hao wanaopata ruzuku wameshindwa kulifanya. Wameamua ku-bite the bullet kwa manufaa ya wote halafu watakaoamua kuzunguka kuleta porojo tena kwa hela za mafisadi waendelee kuulea ufisadi wa kweli.
 
Mimi nilipochangia kwenye thread yangu ya kwanza niliwaambia kwamba hii ni kazi ya EL na ninavyomjua na roho yake ya kisasi huo ni mwanzo tu. Atafanya vituko vya namna hiyo vingi na hata kumdhuru huyu dogo na wengine wenye mtazamo kama wake. Huyu ndiye mnataka awe rais wenu! Mimi naandaa orodha ya matukio ya visasi vya huyu mtu na nitakuja kuyarusha muda si mrefu.

Hata Parokwa aliwekwa kwenye kona kwanza wakatia alipotangaza kuwania ubunge wa Monduli. Akafukuzwa kazi CCM, na baada ya kum-down size ndipo akajiondoa na kupelekwa Moshi akatumikie huko na baada ya kutiwa adabu hiyo, sasa anamuona EL kama mungu!

Hata hivyo Gambo wewe usife moyo. Nchi hii siyo ya mafisadi peke yao na kama Chechetuka alivyosema, siku zao zahesabika na hapa wema lazima utaushinda uovu!
 
Post yako nimeikubali mkuu.

Siku zote mie naamini hivo kuwa zengwe lianzishiwe mlemle ndani ya CCM na wanamageuzi wakamate madaraka ndani ya chama, lakini viongozi wa upinzani hawawezi kulikubali hilo kwani nao wamejimega kule kutaka kusaka madaraka, sasa ukileta point hii unawakera sana japo ni ukweli wa kuleta maendeleo ya kitaifa zaidi.

Hii nami huwa naiunga mkono kwani uongozi ndo kitu muhimu. Ukitaka kujua hayo, Angalia CCM imetoa maraisi wanne lakini katika kila awamu kuna mambo yanayotofautisha awamu nyingine. Thereby, kiongozi hasa raisi ni mtu muhimu sana katika kubadiliasha nchi achilia mbali kidogo chama anachotoka. Lakini sasa kila chama kina mfumo na mazoea yake ambayo wanachama wake wamejijengea kwa hiyo mabadiliko ya haraka ya mfumo mzima yanatoka kwenye chama kipya.
 
Chadema ya sasa iko imara na imejitosheleza. Hatutaki tena mazagazaga yaliyonyimwa fursa ya kufisadi ndani ya ccm.

Tumeona kupitia Shibuda kwamba it if difficult to unlearn the ccm culture and behavior. Tumeona pia kupitia makamanda wapya wa Chadema bungeni kwamba upya hauna ufisadi na tamaa kama wazoefu

Kuwa mwangalifu na hao unaowaita makamanda maana tayari kuna makamanda waasi ambao wanatumikia adui! Nakueleza mapema usije ukafa kwa shock ukishalijua tena kwa ushahidi huko mbele!
 
Chechetuka na Sangara nimependa sana misimamo yenu na kwa hakika naungana na Mbopo kwamba kilio na vita hivi ni vya umma na watu wa kuaminka wa kuvipigana vita hivi watatoka ndani ya chama tawala, ambao nina amini kwamba ndiyo wanaowanyima usingizi mpaka wanawapangia njama za kuwaondoa duniani.

Kinachotakiwa ni kwa Mkuu wa nchi, ambaye nina imani naye kwa asilimia zote na ambaye ninafahamu kwamba anachukizwa sana na vitendo vya mafisadi hawa, kuhakikishwa kwamba uhai au damu ya wazalendo hawa haimwagwi na majahili haya ambayo yameshindwa kuelewa kwamba duniani tunapita tu na kwamba utajiri huo utabaki hapa hapa, huku wao wakiwa na maswali ya kujibu kwa Muumba.

Haishangazi kuona kwamba kiasi kikubwa cha utajiri wao wanakimalizia kutengeneza uhalali wa hata kusalimiana na wananchi maana wanajijua kwamba wakipita huko mtaani maisha yao yako hatarini.
 
Gambo na wapenda haki wote!

Huu ndiyo wakati ambao watanzania wanataka kuona pumba zikipambanuliwa na mchele na kwa hakika wewe ni mchele wa kyela. Huhitaji akili nyingi kujua kwamba hizi ni njama za Millya na wala hupati shida kujua Millya ni kitambaa cha deki cha nani! Walichofanya wao ni kukutua mzigo na kuepuka lawama ambazo UVCCM yote ingezipata kwa kutumika kwake, wakati kumbe kuna watu wenye vichwa wanavyovitumia katika kufikiri.

Sisi tunakuunga mkono na kwa hakika umezindua mapambano ya kweli ya kumuangamiza adui huyu. Hakuna aliyetarajia kwamba Arusha kungetokea mtu akapaza sauti dhidi ya jinamizi hili! Big up!
 
Hayo yote amekuwa akiyajua siku zote kabla na baada ya kujiunga na CCM. Mrisho, usiwe mnafiki na kutaka huruma ya wananchi. Kama hujatendewa haki kwa nini usitumie ngazi za chama? Unalalamika wenzako wamekimbilia kwenye vyombo vya habari, ni vyombo hivyo hivyo unatumia. Umekata rufaa? Umelalamikia hatua hiyo? Kwa nini kama umeshachukua hatua unakimbilia vyombo vya habari? Je uongozi wa juu ukibariki maamuzi ya mkoa? Subira yako iko wapi?

Acheni kutumika, nyinyi ndio mnaiua hii nchi kwa njaa na sifa zenu. Kama mtu ana mtoto wa chuo kikuu halafu bado ni kijana unatuambia sisi tufanye nini? Leo ndio mmejua?
 
Hivi kati yake na wewe nani anatumika hapa? Yeye ame-react kwa kitendo kilichofanyika na anajua kwamba rufaa (kama ipo) inakwenda kwenye vyombo hivyo hivyo vyenye Shigela na Bashe. Unategemea atapata haki? Kwani yeye anazuiwa kuzungumza hayo leo, hasa baada ya kugundua kwamba chama alichokijua siyo hiki cha sasa? Mbona Slaa haya anayozungumza sasa, au hata Shibuda alikwa hayasemi alipokuwa ndani? Kila kitu kina mwanzo wake na uache ku-confuse watu hapa!
 
Hivi kwani mtu hawezi kuwa mpambanaji mpaka atoke ndani ya ccm? Mi sikubaliani na wote wanaotaka wanaopambana na ufisadi watoke ccm kwanza.

Wako wapi kina Mpendazoe, Mrema nk? Wote wamechemsha baada ya kuhama CCM.

Mpambano ni lazima uwe ndani ya chama ili kuwang'oa wezi wa nchi hii. Nashauri wapiganaji wote wasihame CCM ila wawe makini na michezo michafu inayofanyika ndani ya CCM.

"msiwaachie nguruwe wale shambani peke yao"

sikubaliani na mawazo yako ndugu yangu! Chama huwa kinajivunia idadi ya wanachama. Na kuwa mwanachama lazima uwe unafanana nao kiitikadi, mtazamo na kimsimamo. Ndio maana mi naona kama Mrisho ametofauthana na wenzake na amefanana na cdm arudi arusha tumpe kadi tufanye kazi. Huku hatufanyi kazi kwa nguvu ya chama. Its people's power!
 
wanajamii

Binafsi sio nafuu ya gambo, UVCCM pwani, UVCCM arusha, Moshi wala UVCCM taifa

Mie naona ni kundi la wahuni wanaotumia mashati ya kijani na suruali nyeusi kutupotezea muda wa kufanya mambo ya maana
:rip: UVCCM, ni afadhali mjiite skuvi
 
Alaa, kumbe machalii wa Arusha hawawezi kupambana hadi mazagazaga ya ccm yaje kuwasaidia? Waombe radhi wana Chadema wa arusha tafadhali. Hawahitaji walioshindikana ccm
 
Yule Kada wa CCM kupitia UVCCM aliyeanzisha sakata la akina EL na RA ataongea na wandishi wa habari leo saa nne asubuhi, hapa Dar es Salaam.

CHINI NI TAMKO LAKE FULL TEXT

=======================

TAARIFA YA NDUGU MRISHO GAMBO KWA VYOMBO VYA HABARI
JUMAPILI TAREHE 3 APRILI 2011

Ndugu zangu wahariri na waandishi wa vyombo vya habari, nimeona leo nikutane nanyi ili niweze kufafanua mambo machache maana mmekuwa mkinipigia simu sana pamoja na kuniandikia ujumbe wa maandishi kwa lengo la kutaka kupata maoni yangu kuhusu maazimio ya baraza la vijana la mkoa wa Arusha na yalio andikwa kwenye magazeti kabla ya baraza hilo na baada ya baraza hilo. Kwa kuwa yaliondikwa yamegusa utu wangu na kwa kweli nisingeweza kukutana na mtu mmommoja ili kuelezea hali halisi hivyo nikaona tukutane sote hapa ili tujuzane sote pamoja na kuweka historia sawa.

Kwenye baraza la vijana la UVCCM mkoa wa Arusha kama sote tulivyo ona kwenye vyombo vya habari maana walitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wamenivua uongozi wa vijana ndani ya UVCCM, japokuwa hadi leo hawajaniandikia barua kuhusu jambo hili, na wakaamua kupeleka kwenye vyombo vya habari taarifa hii kabla hata ya kuniita na kunihoji kama taratibu zilivyo kwenye chama chetu. Jambo hili lingeishia kwenye baraza na uongozi wa Mkoa ukaniandikia barua kimya kimya wala nisingekuwa na haja ya kuja kuzungumza na waandishi wa habari huku ukizingatia kuwa hawana mamlaka hayo ya kunivua uongozi .

Kabla ya kikao hicho cha baraza la Arusha nilipata taarifa mbalimbali kuwa kuna kikundi cha watu kinafanya vikao ili kuhakikisha kuwa ninavuliwa uongozi kutokana na yaliyo andikwa kwenye magazeti kuwa “
Kashfa za Richmond na Dowans zimechangia sana kukipotezea mvuto chama chetu cha Mapinduzi na inaonekana tija kwa wahusika kuwajibishwa kama sehemu ya kujivua gamba kwa chama chetu”. Mimi niliwajibu kuwa kama wanachosema ni kweli chochote watakachopewa wachukue kwa kuwa Mungu ameamua kunifanya daraja la wao kurudishiwa kodi zao.

Pia nataka kuwakumbusha kitu kimoja kuwa agenda za hali ya kisiasa na tathmini ya uchaguzi zilisha fanyika kwa ngazi ya Jumuiya na chama mikoani na wala hapakuwa na malalamiko yoyote kuhusu mimi. Agenda hizi pia zilijadiliwa kwenye baraza la vijana la CCM Taifa hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine lilipitia taarifa zote za tathmini kutoka mikoani huku Mkoa wa Arusha ukiwa ni miongono mwao. Chakushangaza kwenye tamko lao baraza la uvccm mkoa wa Arusha wakairudia agenda ya hali ya kisiasa na tathmini ya uchaguzi ili hali tayari taarifa yao ilishapelekwa kwenye vikao vya juu bila mimi kulalamikiwa chochote.
Hii ni ishara tosha kuwa ilikuwa ni njama maalum.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari na nakala ya tamko la uvccm mkoa wa Arusha kumesemwa kuwa wametangaza kunisimamisha uongozi kwa kuwa sikumpigia kura na nimemsema vibaya Dada yangu mpendwa Batrida Burhani. Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu anajua kuwa kura ni siri na ni haki ya mtu ya kikatiba, hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kuhoji namna mtu anavyo tumia haki yake ya kupiga kura. Hili ni wazo dhaifu na halina tija kwa wao walio litoa na hasa kwa vijana wa Tanzania ambao wana changamoto nyingi kama vile ajira na matatizo ya bodi ya mikopo. Kwa mtazamo wangu binafsi kama wanafanya kazi hii kwa kutumwa na mtu yeyote basi wajue kuwa kazi wanayo mfanyia mtu huyo ni sawa na kupiga rangi upepo.

Watanzania wa leo ni watanzania wa Dot com na si wa BBC (Born before computer), kwa kuwa wana uwezo wa kupata taarifa mapema. Tamko la baraza la vijana mkoa wa Arusha lilitumwa kwa waandishi wa habari kabla hata ya kikao cha baraza kuisha. Ushahidi ninao wa kutosha, ikiwa ni pamoja na maoni ya baadhi ya wajumbe wa baraza wakiwataja watu walio husika na mpango huo. Miongoni mwao ni mjumbe mmoja wa baraza la mkoa kuwakilisha vijana kwenye mkutano mkuu wa CCM Taifa ambaye ana mtoto anae soma chuo kikuu huku bado akijiita kuwa na umri wa ujana kwa maana ya chini ya miaka 30 kwa taratibu za jumuia yetu.

Nimesikitishwa sana na tamko la baraza la vijana mkoa wa Arusha kulifanya tamko la vijana wa mkoa wa pwani kama sehemu ya azimio lao. Hawana uwezo wowote wa kikanuni wa kuujadili mkoa wa pwani na ukizingatia kuwa baraza kuu la vijana la UVCCM Taifa lilokutana karibuni halikutoa tamko lolote kuhusiana na tamko la vijana wa mkoa wa pwani.

Hofu yangu kubwa ni kuwa nini kinawafanya vijana wenzangu hawa watumie muda wao kujadili matamko ya mikoa mingine badala ya kushughulika na changamoto za vijana wenzetu kuanzia kwenye ngazi ya mashina hadi kwenye ngazi ya mkoa wetu.

Tunahitaji tafakuri ya kina sana kama vijana ili tuweze kufanya mambo kwa maslahi ya chama chetu cha mapinduzi na nchi yetu kwa ujumla.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

mrisho-gambo.jpg

MWISHO
Hapo kwenye RED ndio pananipa mwashawasha
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom