Mrembo wa Tanzania Aolewa na Kibabu cha Kiingereza, Anusurika Kukatwa Mikono Yake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
6105014.jpg

Saluni ya urembo inayomilikiwa na William Porter
Sunday, December 04, 2011 7:58 PM
Mwanamke mrembo wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 25 tu amekiona cha moto baada ya kukubali kuolewa na babu wa Uingereza mwenye umri wa miaka 69 na matokeo yake kujeruhiwa kwa kisu alipolalamika pafomansi mbovu ya babu kitandani.
Mwanamke wa Kitanzania aliyejulikana kwa jina la Saada Mwiazimu mwenye umri wa miaka 25 amenusurika maisha yake baada ya kujeruhiwa kwa kisu na mumewe mfanyabiashara wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 69 anayejulikana kwa jina la William Porter.

William anamiliki saluni maarufu ya masuala ya urembo inayojulikana kwa jina la Tan Express iliyopo kwenye mji wa Scarborough, kaskazini mwa Uingereza.

Kasheshe la Saada kujeruhiwa kwa kisu lilitokea mwezi juni mwaka jana wakati Saada na mumewe walipokuwa kitandani wakiangalia DVD.

Mazungumzo yao yalipelekea Saada kuzungumzia pafomansi mbovu ya William kwenye malavi davi na kupelekea William kukasirika sana.

William alimdondosha chini Saada na baadae kumjeruhi kwa kisu mikononi huku akitishia kuikata mikono ya mke wake huyo aliyemleta toka Tanzania.

Kesi ya William kumjeruhi Saada ilifikishwa mahakamani na wiki iliyopita ndiyo hukumu ilitolewa ambapo William alipatikana na hatia ya kufanya shambulio la kudhuru mwili na kuhukumiwa kwenda jela miezi 15.

Mwanzo wa yote ilikuwa mwaka 2009 wakati William aliposafiri kuja Tanzania kuonana na Saada ambaye alimjua kupitia dada yake ambaye yupo Uingereza na kuanza kuwasiliana naye kwa kutumia email.

Kukutana kwao kulipelekea kuanza kwa uhusiano wa mapenzi ambapo William alimualika Saada Uingereza ili pia aje akutane na dada yake. Ujio huo haukudumu muda mrefu kwani Saada alikamatwa akiishi Uingereza akiwa amepitiliza muda wake wa kuruhusiwa kuishi Uingereza. Alirudishwa Tanzania na maafisa wa uhamiaji wa Uingereza.

William aliamua kutumia njia ya kumuoa Saada ili waweze kuishi pamoja Uingereza. William kwa mara nyingine alikuja Tanzania na kumuoa Saada mwezi januari mwaka jana na kuanza mikakati ya kumtafutia viza ili aruhusiwe kuishi Uingereza. Baada ya vipingamizi vya hapa na pale hatimaye Saada alipewa viza na kuwasili Uingereza mwezi mei mwaka jana.

Saada aliishi pamoja na William kwenye nyumba ya juu katika ghorofa linalomilikiwa William ambapo mke wa zamani wa William alikuwa akiishi nyumba ya chini.

Hatimaye mwezi mmoja baada ya kuhamia kwenye nyumba hiyo ndipo sakata hilo lilipotokea na kupelekea Saada abaki na makovu kwenye mikono yake.

Akijitetea kabla ya kuhukumiwa kwenda jela miezi 15, William aliiambia mahakama kuwa kesi hii ilipangwa na mkewe ili aweze kumkimbia aendelee kuishi Uingereza.

Mahakama ya York Crown Court ilimuona William ana hatia ya kumshambulia mkewe kwa kisu cha urefu wa inchi 12 na kumhukumu kwenda jela.
chanzo: Mrembo wa Tanzania Aolewa na Kibabu cha Kiingereza, Anusurika Kukatwa Mikono Yake
 
Angekatwa 2 maana mabinti wa sasa wanapenda mkwanja sana m2 wangu kuliko hata penzi lenyewe.
 
Back
Top Bottom