Mrema wa TANROADS ang'olewa rasmi

Mrema wa TANROADS ang'olewa rasmi

*Ni uamuzi wa Waziri Dkt. John Magufuli
*Akabidhiwa barua na Katibu Mkuu Chambo

Na John Daniel

HATIMAYE kasi na viwango katika utendaji kazi wa Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli umeanza kuonekana wazi baada ya kumwondoa rasmi aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Bw. Ephraem Mrema.Bw. Mrema ambaye
amekuwa akipigiwa kelele kwa kukumbwa na tuhuma mbalimbali za kiutendaji ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 300 huku akikataa kuonana na waandishi wa habari, aliondolewa rasmi Ofisini kwake jana.

Vyanzo vyetu vya uhakika ndani ya serikali vililieleza Majira kuwa Bw. Mrema aliondolewa ofisini kwake saa 9.30 mchana na timu ya maofisa watano kutoka Wizara ya Ujenzi.

"Nakuhakikishia leo (jana) saa 9.30 ulikuwa mwisho wa Mrema Ofisini, walikwenda maofisa watano kutoka Wizarani wakiongozwa na Katibu Mkuu Chambo (Omar) na kumkabidhi barua yake ya kuondoka.

Walimtaka akabidhi Ofisi kwa Mkurugenzi wa Barabara Vijini, Bw. Patric Mfugale, ila nadhani taarifa rasmi itatolewa kesho (leo)," kilisema chanzo chetu.

Vyanzo vyetu ndani ya serikli vieleza kuwa tangu siku ya Jumapili wiki hii, Bw. Mrema alikuwa akihitaji kukutana kufanya mazungumzo na Dkt. Magufuli lakini waziri huyo hakuwa tayari kufanya hivyo.

Waziri Magufuli alikataa kuonana na Bw. Mrema kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuhitaji kuangalia nyaraka mbalimbali zinazohusu utendaji na majibu yake.

Juzi (Jumanne) Waziri Magufuli alidaiwa kutoa maamuzi yake kuhusu Bw. Mrema na kuwasilisha rasmi mapendekezo yake kwa Rais Kikwete jana kabla ya kuondolewa kwa mtendaji huyo.

Katika mapendekezo yake, Dkt. Magufuli alirejea tuhuma mbalimbali za Bw. Mrema na hali halisi ndani ya TANROADS pamoja na matarajio yake ya kiutendaji ndani ya wizara hiyo.

Ilielezwa kwamba baada ya muda wa Bw. Mrema kumalizika Novemba 27, mwaka huu kulikuwa na jitihada kubwa kuhakikisha anaendelea na nafasi hiyo, lakini kuteuliwa kwa Dkt. Magufuli kunatajwa kuwa ni kikwazo kwa juhudi hizo.

"Magufuli ni kiboko, hana cha tajiri wala maskini, akiona uovu anashughulikia, huyu mkubwa alikuwa tishio lakini kuondoka kwake ni hatua kubwa ya utekelezaji wa ahadi za Kikwete kuhusu barabara," kilisema chanzo chetu.Baadhi ya tuhuma za Bw. Mrema ni pamoja na kusababisha mgongano kati ya Bodi ya Tanroads, na wakala hiyo pamoja na wizara yenyewe.

Pia Bw. Mrema alidaiwa kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji wa TANROADS waliokuwa hawako na nia moja na kuitisha kikao cha wafanyakazi Oktoba 30, mwaka huu kutangaza maamuzi hayo.

Waliokumbwa na sakata hilo walikuwa ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara, Bw. Thomas Mosso, Mkurugenzi wa Mipango, Bw. Jason Rwiza, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dodoma, Bw. Gerson Lwenge.

Wengine ni aliyekuwa Meneja Mkoa wa Morogoro, Bw. Charles Madinda, Meneja Mkoa wa Ruvuma, Bw. Abraham Kissimbo na Mhandisi Makao Makuu TANROADS, Bw. William Shilla.

Uchunguzi wa Majira ulibaini kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliwahi kuchunguza mradi wa barabara ya Bagamoyo-Msata ambayo TANROADS ilidaiwa kusaini mkataba kiaina na kampuni moja ya Korea.
Katika sakata hilo serikali ilisitisha na kupata hasara ya mabilioni ya fedha huku zabuni mpya ikitangazwa kwa mizengwe kupotosha ukweli.

Bw. Mrema amekuwa akiandamwa na mivutano mikubwa kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu. Mwaka 2008 alidaiwa kushtakiwa na PPRA ikitaka wizara kumchukulia hatua kwa kukiuka sheria, taratibu na kauni za manunuzi, jambo ambalo halikufanyika. Hata hivyo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake hivyo kuzua hofu kuwa alikuwa akilindwa na vigogo.
Tuhuma nyingine iliyodaiwa dhidi ya Mrema ni uongozi wake kuukosesha serikali sh. bilioni 12 kutoka Benki ya Dunia (WB) zilizotolewa kujenga jengo la TANROADS.

Katika tuhuma hiyo ilidaiwa kuwa Bw. Mrema alikataa kujenga Ofisi za TANROADS eneo la Mabibo kwa madai kuwa anataka katikati ya Jiji la Dar es Salaam, hivyo kusababisha WB kuondoa fedha zao huku serikali ikiwa imelipa mshauri mwelekezi sh. bilioni tatu za kodi za Watanzania.

Juhudi za Majira kuwasiliana na Bw. Mrema ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila muda mrefu bila kupokewa.

Source: Majira

Pombe pekee ndio imemuweza Bw. Mrema!!!!
 
Kila kitu kina mwisho wake.. ila cha kusikitisha ni hyi tu asara aliyisababishia serikali na rais kumwaangalia na kumuacha madarakani bili tatizo . Ahsante magufuli na bado iko shida hapo.....:redfaces:
 
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameanza kazi kwa kufanya maamuzi magumu kwa kumfukuza kazi Mtendaji Mkuu (Ceo) wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Ephraim Mrema.
Habari za uhakika ambazo NIPASHE limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa Dk. Magufuli alifanya uamuzi huo jana.
Vyanzo hivyo havikueleza sababu za kumtimua Mrema, zaidi ya kusema kuwa uamuzi huo unaanza mara moja.
Habari zaidi zinasema kuwa Dk. Magufuli alimtaka Mrema kukabidhi ofisi jana mchana na nafasi yake inashikiliwa kwa muda na aliyekuwa Mkurugenzi wa Barabara za Vijijini, Patrick Mfugale.
Hata hivyo, NIPASHE lilimtafuta Dk. Magufuli jana usiku kwa ajili ya kuthibitisha habari hizo, lakini simu yake ya kiganjani ilikuwa imezimwa.

CHANZO: NIPASHE
 
I don't understand this; kwani Kawambwa alishindwa na kitu gani au Magufuli kaja na nguvu gani nje ya zile ambazo Kawambwa alikuwa nazo; this just make Kawambwa aonekane vibaya. Haiwezekeni watu wamsubiri Magufuli. Msije kuniambia kuwa hata ATCL sasa imepata kiongozi?
 
Huyo mrema inatakiwa ashtakiwe kwa kutumia fedha za umma na madaraka vibaya,magufuli endelea na kasi hiyo hiyo hadi kieleweke.
 
Sijui kama wanajamvi kuna kitu tunajifunza hapa sijasikia hoja ya uonevu au kaondolewa kwasababu ya dini yake ?.Ngoja mtendaji mkuu wa NSSF aguswe utasikia hana kosa anaonewa kwasababu ni .......ebo wakati mwingine tunatakiwa kukua kidogo mtu akikosa asitetewe kwa vigezo vya dini au kabila lake.
 
SAFIII MAGUFULI, ukishamaliza hapo naomba vamia watu wa mizani na hasa mzani wa kibaha, pale pana kila aina ya uvundo na uchafu, ni rushwa na ubadhilifu wa kila namna, malori mengi yanahonga yakiover load na wanaruhusiwa kusafiri na ndio chanzo cha kutokudumu kwa barabara zetu- BIG UP POMBE!!!
 
Safi sana pombe. Tunaomba kikwete asikuingilie Kwenye maamuzi haya. Endeleeaaa mwanawanee tupo nyuma yako
 
hii safi sana.....uozo umezidi pale Tanroads....akitoka hapo ahamie ATCL!!
 
I don't understand this; kwani Kawambwa alishindwa na kitu gani au Magufuli kaja na nguvu gani nje ya zile ambazo Kawambwa alikuwa nazo; this just make Kawambwa aonekane vibaya. Haiwezekeni watu wamsubiri Magufuli. Msije kuniambia kuwa hata ATCL sasa imepata kiongozi?

hii safi sana.....uozo umezidi pale Tanroads....akitoka hapo ahamie ATCL!!

ATCL ipo chini ya Wizara gani; Ujenzi au Uchukuzi?
 
Mrema wa TANROADS ang'olewa rasmi

*Ni uamuzi wa Waziri Dkt. John Magufuli
*Akabidhiwa barua na Katibu Mkuu Chambo

Na John Daniel

HATIMAYE kasi na viwango katika utendaji kazi wa Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli umeanza kuonekana wazi baada ya kumwondoa rasmi aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Bw. Ephraem Mrema.Bw. Mrema ambaye
amekuwa akipigiwa kelele kwa kukumbwa na tuhuma mbalimbali za kiutendaji ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 300 huku akikataa kuonana na waandishi wa habari, aliondolewa rasmi Ofisini kwake jana.

Vyanzo vyetu vya uhakika ndani ya serikali vililieleza Majira kuwa Bw. Mrema aliondolewa ofisini kwake saa 9.30 mchana na timu ya maofisa watano kutoka Wizara ya Ujenzi.

"Nakuhakikishia leo (jana) saa 9.30 ulikuwa mwisho wa Mrema Ofisini, walikwenda maofisa watano kutoka Wizarani wakiongozwa na Katibu Mkuu Chambo (Omar) na kumkabidhi barua yake ya kuondoka.

Walimtaka akabidhi Ofisi kwa Mkurugenzi wa Barabara Vijini, Bw. Patric Mfugale, ila nadhani taarifa rasmi itatolewa kesho (leo)," kilisema chanzo chetu.

Vyanzo vyetu ndani ya serikli vieleza kuwa tangu siku ya Jumapili wiki hii, Bw. Mrema alikuwa akihitaji kukutana kufanya mazungumzo na Dkt. Magufuli lakini waziri huyo hakuwa tayari kufanya hivyo.

Waziri Magufuli alikataa kuonana na Bw. Mrema kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuhitaji kuangalia nyaraka mbalimbali zinazohusu utendaji na majibu yake.

Juzi (Jumanne) Waziri Magufuli alidaiwa kutoa maamuzi yake kuhusu Bw. Mrema na kuwasilisha rasmi mapendekezo yake kwa Rais Kikwete jana kabla ya kuondolewa kwa mtendaji huyo.

Katika mapendekezo yake, Dkt. Magufuli alirejea tuhuma mbalimbali za Bw. Mrema na hali halisi ndani ya TANROADS pamoja na matarajio yake ya kiutendaji ndani ya wizara hiyo.

Ilielezwa kwamba baada ya muda wa Bw. Mrema kumalizika Novemba 27, mwaka huu kulikuwa na jitihada kubwa kuhakikisha anaendelea na nafasi hiyo, lakini kuteuliwa kwa Dkt. Magufuli kunatajwa kuwa ni kikwazo kwa juhudi hizo.

"Magufuli ni kiboko, hana cha tajiri wala maskini, akiona uovu anashughulikia, huyu mkubwa alikuwa tishio lakini kuondoka kwake ni hatua kubwa ya utekelezaji wa ahadi za Kikwete kuhusu barabara," kilisema chanzo chetu.Baadhi ya tuhuma za Bw. Mrema ni pamoja na kusababisha mgongano kati ya Bodi ya Tanroads, na wakala hiyo pamoja na wizara yenyewe.

Pia Bw. Mrema alidaiwa kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji wa TANROADS waliokuwa hawako na nia moja na kuitisha kikao cha wafanyakazi Oktoba 30, mwaka huu kutangaza maamuzi hayo.

Waliokumbwa na sakata hilo walikuwa ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara, Bw. Thomas Mosso, Mkurugenzi wa Mipango, Bw. Jason Rwiza, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dodoma, Bw. Gerson Lwenge.

Wengine ni aliyekuwa Meneja Mkoa wa Morogoro, Bw. Charles Madinda, Meneja Mkoa wa Ruvuma, Bw. Abraham Kissimbo na Mhandisi Makao Makuu TANROADS, Bw. William Shilla.

Uchunguzi wa Majira ulibaini kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliwahi kuchunguza mradi wa barabara ya Bagamoyo-Msata ambayo TANROADS ilidaiwa kusaini mkataba kiaina na kampuni moja ya Korea.
Katika sakata hilo serikali ilisitisha na kupata hasara ya mabilioni ya fedha huku zabuni mpya ikitangazwa kwa mizengwe kupotosha ukweli.

Bw. Mrema amekuwa akiandamwa na mivutano mikubwa kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu. Mwaka 2008 alidaiwa kushtakiwa na PPRA ikitaka wizara kumchukulia hatua kwa kukiuka sheria, taratibu na kauni za manunuzi, jambo ambalo halikufanyika. Hata hivyo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake hivyo kuzua hofu kuwa alikuwa akilindwa na vigogo.
Tuhuma nyingine iliyodaiwa dhidi ya Mrema ni uongozi wake kuukosesha serikali sh. bilioni 12 kutoka Benki ya Dunia (WB) zilizotolewa kujenga jengo la TANROADS.

Katika tuhuma hiyo ilidaiwa kuwa Bw. Mrema alikataa kujenga Ofisi za TANROADS eneo la Mabibo kwa madai kuwa anataka katikati ya Jiji la Dar es Salaam, hivyo kusababisha WB kuondoa fedha zao huku serikali ikiwa imelipa mshauri mwelekezi sh. bilioni tatu za kodi za Watanzania.

Juhudi za Majira kuwasiliana na Bw. Mrema ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila muda mrefu bila kupokewa.

Source: Majira

Pombe pekee ndio imemuweza Bw. Mrema!!!!
Ohh!!! Tayari Pombe imeshaanza Kunyweka Tanroads ..
 
I don't understand this; kwani Kawambwa alishindwa na kitu gani au Magufuli kaja na nguvu gani nje ya zile ambazo Kawambwa alikuwa nazo; this just make Kawambwa aonekane vibaya. Haiwezekeni watu wamsubiri Magufuli. Msije kuniambia kuwa hata ATCL sasa imepata kiongozi?

Huyu Kawambwa kashabadilishwa Wizara nne toka JK awe Rais...kila reshuffle inamuafekti...sijui tatizo ni nini
 
Back
Top Bottom