Mrema wa TANROADS ang'olewa rasmi

Habari from TANROAD zinathibitisha kuwa Katibu mkuu, Naibu katibu mkuu na HR wa Miundo mbinu wamempa dispatch Mr Mrema na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa barabara vijijini Mr Mfugale. Na aliyekuwa meneja wa Tanroad Dar (Mr Nyabakari) amekuwa mkurugenzi wa Miradi-director of projects.

Nafasi hizo yapasa wazitangaze...............wasipeane kiundugunazesheni.........itakuwa ni ufisadi tu wakifanya hivyo................
 
Nafasi hizo yapasa wazitangaze...............wasipeane kiundugunazesheni.........itakuwa ni ufisadi tu wakifanya hivyo................

Mkuu inakuuma vipi? Wanapomtema mtu lazima ujue kwamba kuna walakini na wameshajipanga huo ushuri/mawazo chacha hivi ni zero. Lets wait and see who comes, what he could change and may be deliver.
 
HATIMAYE Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Ephraim Mrema, ameong’olewa rasmi katika nafasi hiyo na kukabidhi ofisi hiyo jana kwa Kaimu Mtendaji aliyeteuliwa, Injinia Patrick Mfugale.

Mwanzoni mwa wiki hii Waziri mpya wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alimtaka Mrema afanye kazi huku akiamini haondoki katika wadhifa huo na aweke matumaini ya kuishi kwa miaka 100.

Kwa kirefu Mrema amekuwa akiandamwa na tuhuma mbalimbali za kifisadi katika wakala huo, ikiwa ni pamoja na kudaiwa kuvunja mikataba na makandarasi bila kufuata taratibu.

Hata hivyo, taarifa za kuaminika ambazo Tanzania Daima inazo kutoka TANROADS, zilieleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa jana baada ya viongozi wakuu wa wizara hiyo kukutana na kujadili juu ya suala la Mrema na kufikia hatua ya kumuengua.

“Huu uamuzi umefikiwa leo na viongozi wetu wakuu, kwa kweli tumefurahishwa sana maana ukiangalia kwa kipindi chote alichokaa katika uongozi wake Wakala huu umepoteza sifa, huku akivunja mikataba kila mara ya makandarasi bila kufuata utaratibu,” alisema mtoa taarifa wetu.

Alisema kuwa Mrema hajafurahishwa na uamuzi huo ambapo inadaiwa iwapo serikali itaamua kumchukulia hatua atakuwa tayari kuwataja vigogo wote waliokuwa wakiomba fedha ndani ya wakala huo.

Wakati huo huo, taarifa hizo zilifafanua kuwa kwa sasa ameandika barua akieleza kuwa amepata nafasi ya masomo nchini Uingereza kwa ajili ya shahada ya uzamivu ya ‘Civil Engineering’.

Uamuzi huo wa Mrema kuelekea nje ya nchi umeelezwa kuwa ni wa kutaka kukwepa ushahidi, kwa kile kilichoelezwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kuwa inaweza kumchunguza kwa tuhuma za kuisababishia hasara serikali.
 
.... ikiwa ni pamoja na kudaiwa kuvunja mikataba na makandarasi bila kufuata taratibu....huku akivunja mikataba kila mara ya makandarasi bila kufuata utaratibu,”
tatizo lake ni kuvunja mikataba ya makandarasi bila taratibu? na wao mbona hawaelezi wamevunjaje mkataba wa ajira yake?
 
tatizo lake ni kuvunja mikataba ya makandarasi bila taratibu? na wao mbona hawaelezi wamevunjaje mkataba wa ajira yake?

Muda wa mkataba wake ulishaisha,
Alitaka kuongezewa muda kinyemela na jk ndo maana wabunge last time wakapiga kelele sana nafasi itangazwe upya.
 
HATIMAYE Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Ephraim Mrema, ameong’olewa rasmi katika nafasi hiyo na kukabidhi ofisi hiyo jana kwa Kaimu Mtendaji aliyeteuliwa, Injinia Patrick Mfugale.

Mwanzoni mwa wiki hii Waziri mpya wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alimtaka Mrema afanye kazi huku akiamini haondoki katika wadhifa huo na aweke matumaini ya kuishi kwa miaka 100.

Kwa kirefu Mrema amekuwa akiandamwa na tuhuma mbalimbali za kifisadi katika wakala huo, ikiwa ni pamoja na kudaiwa kuvunja mikataba na makandarasi bila kufuata taratibu.

Hata hivyo, taarifa za kuaminika ambazo Tanzania Daima inazo kutoka TANROADS, zilieleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa jana baada ya viongozi wakuu wa wizara hiyo kukutana na kujadili juu ya suala la Mrema na kufikia hatua ya kumuengua.

“Huu uamuzi umefikiwa leo na viongozi wetu wakuu, kwa kweli tumefurahishwa sana maana ukiangalia kwa kipindi chote alichokaa katika uongozi wake Wakala huu umepoteza sifa, huku akivunja mikataba kila mara ya makandarasi bila kufuata utaratibu,” alisema mtoa taarifa wetu.

Alisema kuwa Mrema hajafurahishwa na uamuzi huo ambapo inadaiwa iwapo serikali itaamua kumchukulia hatua atakuwa tayari kuwataja vigogo wote waliokuwa wakiomba fedha ndani ya wakala huo.

Wakati huo huo, taarifa hizo zilifafanua kuwa kwa sasa ameandika barua akieleza kuwa amepata nafasi ya masomo nchini Uingereza kwa ajili ya shahada ya uzamivu ya ‘Civil Engineering’.
 
Hongera magufuli, nafikiri wangekupa UWAZIRI MKUU MAANA PINDA ANAWAOGOPA MAFISADI, NINGEFURAHI SANA
 
yaani huyu ndo waziri sasa anajiamini na anafanya maamuzi kwa ujasiri mkubwa sio kawambwa
 
Kweli magufuli mwanaume, tungekuwa na viongozi kama kumi wa hivi i am sure tungeenda mbali maaana magufuli haogopi mtu, Kila anakoenda lazima atimue mtu pale ardhi, TIBAIJUKA FANYA MAMBO FUKAZA HAO, WIZARA YA AFYA Dr HAJI angalia hao, hela za wahisani zinapotea tu, tunapewa net badala ya kuua masalia ya mbu?? HUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU, ELIMI, UTALIIIIIIIIIIIIIII PAMEOZA, KULE BANDARINI KUMEOZAAAAAAAAAAAA
 
He has been relieved of his duties and Mr. Patrick Mfugake, the agency's Director of Rural roads took over as an acting CEO.

Source: The Guardian december 02,2010.
 
Mrema wa TANROADS ang'olewa rasmi

*Ni uamuzi wa Waziri Dkt. John Magufuli
*Akabidhiwa barua na Katibu Mkuu Chambo

Na John Daniel

HATIMAYE kasi na viwango katika utendaji kazi wa Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli umeanza kuonekana wazi baada ya kumwondoa rasmi aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Bw. Ephraem Mrema.Bw. Mrema ambaye
amekuwa akipigiwa kelele kwa kukumbwa na tuhuma mbalimbali za kiutendaji ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 300 huku akikataa kuonana na waandishi wa habari, aliondolewa rasmi Ofisini kwake jana.

Vyanzo vyetu vya uhakika ndani ya serikali vililieleza Majira kuwa Bw. Mrema aliondolewa ofisini kwake saa 9.30 mchana na timu ya maofisa watano kutoka Wizara ya Ujenzi.

"Nakuhakikishia leo (jana) saa 9.30 ulikuwa mwisho wa Mrema Ofisini, walikwenda maofisa watano kutoka Wizarani wakiongozwa na Katibu Mkuu Chambo (Omar) na kumkabidhi barua yake ya kuondoka.

Walimtaka akabidhi Ofisi kwa Mkurugenzi wa Barabara Vijini, Bw. Patric Mfugale, ila nadhani taarifa rasmi itatolewa kesho (leo)," kilisema chanzo chetu.

Vyanzo vyetu ndani ya serikli vieleza kuwa tangu siku ya Jumapili wiki hii, Bw. Mrema alikuwa akihitaji kukutana kufanya mazungumzo na Dkt. Magufuli lakini waziri huyo hakuwa tayari kufanya hivyo.

Waziri Magufuli alikataa kuonana na Bw. Mrema kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuhitaji kuangalia nyaraka mbalimbali zinazohusu utendaji na majibu yake.

Juzi (Jumanne) Waziri Magufuli alidaiwa kutoa maamuzi yake kuhusu Bw. Mrema na kuwasilisha rasmi mapendekezo yake kwa Rais Kikwete jana kabla ya kuondolewa kwa mtendaji huyo.

Katika mapendekezo yake, Dkt. Magufuli alirejea tuhuma mbalimbali za Bw. Mrema na hali halisi ndani ya TANROADS pamoja na matarajio yake ya kiutendaji ndani ya wizara hiyo.

Ilielezwa kwamba baada ya muda wa Bw. Mrema kumalizika Novemba 27, mwaka huu kulikuwa na jitihada kubwa kuhakikisha anaendelea na nafasi hiyo, lakini kuteuliwa kwa Dkt. Magufuli kunatajwa kuwa ni kikwazo kwa juhudi hizo.

"Magufuli ni kiboko, hana cha tajiri wala maskini, akiona uovu anashughulikia, huyu mkubwa alikuwa tishio lakini kuondoka kwake ni hatua kubwa ya utekelezaji wa ahadi za Kikwete kuhusu barabara," kilisema chanzo chetu.Baadhi ya tuhuma za Bw. Mrema ni pamoja na kusababisha mgongano kati ya Bodi ya Tanroads, na wakala hiyo pamoja na wizara yenyewe.

Pia Bw. Mrema alidaiwa kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji wa TANROADS waliokuwa hawako na nia moja na kuitisha kikao cha wafanyakazi Oktoba 30, mwaka huu kutangaza maamuzi hayo.

Waliokumbwa na sakata hilo walikuwa ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara, Bw. Thomas Mosso, Mkurugenzi wa Mipango, Bw. Jason Rwiza, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dodoma, Bw. Gerson Lwenge.

Wengine ni aliyekuwa Meneja Mkoa wa Morogoro, Bw. Charles Madinda, Meneja Mkoa wa Ruvuma, Bw. Abraham Kissimbo na Mhandisi Makao Makuu TANROADS, Bw. William Shilla.

Uchunguzi wa Majira ulibaini kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliwahi kuchunguza mradi wa barabara ya Bagamoyo-Msata ambayo TANROADS ilidaiwa kusaini mkataba kiaina na kampuni moja ya Korea.
Katika sakata hilo serikali ilisitisha na kupata hasara ya mabilioni ya fedha huku zabuni mpya ikitangazwa kwa mizengwe kupotosha ukweli.

Bw. Mrema amekuwa akiandamwa na mivutano mikubwa kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu. Mwaka 2008 alidaiwa kushtakiwa na PPRA ikitaka wizara kumchukulia hatua kwa kukiuka sheria, taratibu na kauni za manunuzi, jambo ambalo halikufanyika. Hata hivyo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake hivyo kuzua hofu kuwa alikuwa akilindwa na vigogo.
Tuhuma nyingine iliyodaiwa dhidi ya Mrema ni uongozi wake kuukosesha serikali sh. bilioni 12 kutoka Benki ya Dunia (WB) zilizotolewa kujenga jengo la TANROADS.

Katika tuhuma hiyo ilidaiwa kuwa Bw. Mrema alikataa kujenga Ofisi za TANROADS eneo la Mabibo kwa madai kuwa anataka katikati ya Jiji la Dar es Salaam, hivyo kusababisha WB kuondoa fedha zao huku serikali ikiwa imelipa mshauri mwelekezi sh. bilioni tatu za kodi za Watanzania.

Juhudi za Majira kuwasiliana na Bw. Mrema ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila muda mrefu bila kupokewa.

Source: Majira

Pombe pekee ndio imemuweza Bw. Mrema!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom