Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,359
aongezewe sleeping allowances
Dozing allowance, so to speak.
aongezewe sleeping allowances
Nasikia kuna mbunge wa CCM kalalamika eti huyo mwandishi wa habari anae toa picha za wabunge wanao sinzia bungeni anatafuta umaarufu
Kama utapata gazeti la Mwananchi tarehe 30/06/2011 ukurasa wa mbele kabisa basi utakutana na picha ya muheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema mbunge wa jimbo la Vunjo akiwa amelala na udenda ukiwa unamtoka kwenye kikao cha bajeti bungeni. Kweli kwa mtazamo wangu mimi binafsi siungi hoja ya wapiga picha kutoa picha kama hii hata kama ni uhuru wa viombo vya habari huku ni kumzalilisha mtu, gazeti la Mwananchi tena wanasema gazeti la watu makini huku sasa ni kuvuka mipaka naomba wanaJF wenzangu mimi sio mwanachama wa TLP naona ifikie wakati pale bungeni wapiga picha wawe wanapewa mipaka ya kupiga picha. Nawasilisha lakini siungi hoja picha kama hizi au tulifananishe gazeti na magazeti ya udaku?
Anatafakari 'inji' anavyoidanganya kuwa yeye ni mpinzani kumbe ni CCM damu!Mzee wa Kiraracha amechoshwa na kikombe cha babu.
Kuna wakati huwa nashindwa kuelewa kama kweli TZ ipo siku tutakuwa na maisha safi, mawaziri wanasinzia kwenye vikao pia wabunge wenye jukumu la kuisimamia serikali wanasinzia, mrema na wabunge wa ccm yani huwezi kujua kama wamejiandaa kuchangia hoja au vipi
Ni aibu sijui anajisikiaje?mwenyewe amechoka sijui kwa nini asistaafu hizi kazi akabaki kuangalia vijana wanafanyaje kazi na kuwashauri na hili ndio tatizo la wazee walioko kwenye vinafasi wanadhani watoto walio walea hawajakua, wanang'ang'ania wanakufa vibaya, ni vizuri wazee wakawaacha vijana wachukue nafasi wao wabaki washauri tu. au tuseme hawakujiandaa kuwa wazee kwa hiyo bado wanatafuta maisha?
Kuna wakati huwa nashindwa kuelewa kama kweli TZ ipo siku tutakuwa na maisha safi, mawaziri wanasinzia kwenye vikao pia wabunge wenye jukumu la kuisimamia serikali wanasinzia, mrema na wabunge wa ccm yani huwezi kujua kama wamejiandaa kuchangia hoja au vipi
Baadaye aliamka akadai pensheni ya unaibu Waziri Mkuu. Akasema ni yeye na SAS ndio wamewahi kufikia ngazi hiyo.watu wa VUNJO pole zenu.
Aliyeileta humu JF ndiye mbaya zaidi. Kwenye gazeti denda hili halionekani vizuri kwa kiwango hiki.Pamoja na hayo. Ni picha mbaya ambayo itamuandama mjwahuzi (mpiga picha) hadi atajisikia vibaya. Zaidi ya huyo dada aliyetapika. Mujwahuzi ni mwanahabari asiye na maadili ya kazi wala mipaka ya kiutendaji na maamuzi. Hata huyo mhariri wa gazeti naye ana kasoro. Mbona huu ni udhalilishaji? Kuna suala la umri, maradhi, majukumu, pamoja na kukabiliana na tusiyoyajua kesho. Sasa huyu mwandishi hayaoni haya. Familia yake inajisikiaje? Nasema tena, huu ni udhalilishaji na matumizi mabaya ya maamuzi