Mrema na Cheyo waomba CHADEMA ifutwe

Wadau jana mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema na mwenyekiti wa UDP John Cheyo waliishambulia CHADEMA kwa maneno unayoweza kufananisha na matusi. Eti Mrema ameshauri CHADEMA ifutwe kwa sababu wanataka kuleta vita. Cheyo naye amesema CHADEMA wanataka kuleta mambo ya Libya na Misri.

Hivi kweli hawa ni wapinzani? Na kwanini wote wazungumze lugha moja kwa wakati mmoja. Imetokea kwa bahati mbaya? Eti Mrema anadai CHADEMA hawana uchungu na taifa hili na wanatumiwa na mataifa ya nje...
mrema.jpg

aCheyo.jpg

Unategemea nini?
 
wewe ndo kilaza wakufa mtu hata upepo huoni, mkuu ccm mnakazi kubwa saana ya kuleta mapinduzi kiuchumi acheni mbwembwe!!

Upepo?? Rais fulani wa USA aliwahi kusema kwamba Katika kuogelea,, linapokuja swala la kuogelea kwa mbwembwe,, ogelea tu uende na maji kadiri yanavyokupeleka,, lakini linapokuja suala la msimamo,, simama imara kama mwamba. Amani ndiyo inatufanya wengi wetu tusiunge mkono namna CDM inavyotaka kutupeleka kama maji. Shida zipo, na ni muhimu zikapatiwa jawabu mapema lakini lazima tusimame imara kwenye kulinda amani. Wewe fuata upepo tu.
Napita fasta sana.
 
Kwani lazima CDM kifutwe? Kwanini usihamasishe wananchi kivyako au ukaratibu maandamano ya mapinduzi bila kushirikisha CDM.
 
Upepo?? Rais fulani wa USA aliwahi kusema kwamba Katika kuogelea,, linapokuja swala la kuogelea kwa mbwembwe,, ogelea tu uende na maji kadiri yanavyokupeleka,, lakini linapokuja suala la msimamo,, simama imara kama mwamba. Amani ndiyo inatufanya wengi wetu tusiunge mkono namna CDM inavyotaka kutupeleka kama maji. Shida zipo, na ni muhimu zikapatiwa jawabu mapema lakini lazima tusimame imara kwenye kulinda amani. Wewe fuata upepo tu.
Napita fasta sana.
mKUU NITAKE RADHI USIDHANI KILA MTU ANAYEUNGA MAANDAMANO YA CDM ANAFUATA UPEPO HILO NDO TATIZO LA CCM MNAFIKIRI KWA UFUPI SAANA MNATOA MAJIBU MEPESI KWENYE MASWALI MAGUMU MKUU, CDM HAIKUPELEKI KAMA MAJI WEWE ILA MAFISADI WA CCM NDO WANACHEZA NA HII NCHI MIMI NAWACHUKIA MAFISADI KWA MOYO YOOTE NA HATA WAKITAKA KUNIUA LEO NIPO TAYALI! JK KWA NINI ANASHINDWA KUACT KWENYE HAYO! MWAMBIE JK AFANYE KAZI AAACHE MBWEMBWE!
 
Aaaaah wapi! huu moto hawataweza kuuzima hadi kitakapo eleweka maana huu si moto wa mabua jamaa wamejipanga vizuri sana na wanajua wanachokifanya kwa Wananchi wao kwa maana hata wao pia wana damu na nyama hivyo hizi za kusema wanavunja Amani ni propaganda zisizo na msingi wowote ndugu zangu.

Wananchi wa Tanzania wanaelewa ni nini wanakifanya na kuwafanisha CDM na Mrema si sahihi kabisa kwa kuwa CCM hawawezi kuwachakachua CDM kama walivyo mchakachua MREMA, CHEYO na CUF sasa wamebaki kuwa ni wapiga debe wa CCM tu basi.

Nasema Tendwa tafadhali usije ukatuingiza matatizoni kama KADI YAO RUDISHA ili uwe nutral na Watanzania tutakuheshimu lakini ukiwafuata hao KIDUMU ukakosea tu WATANZANIA DAMU ZETU ZITADAIWA MIKONONI MWAKO!.

CHONDE CHONDE CDM ISIFUTWE NDIO MKOMBOZI PEKEE KWA WATANZANIA.
 
mKUU NITAKE RADHI USIDHANI KILA MTU ANAYEUNGA MAANDAMANO YA CDM ANAFUATA UPEPO HILO NDO TATIZO LA CCM MNAFIKIRI KWA UFUPI SAANA MNATOA MAJIBU MEPESI KWENYE MASWALI MAGUMU MKUU, CDM HAIKUPELEKI KAMA MAJI WEWE ILA MAFISADI WA CCM NDO WANACHEZA NA HII NCHI MIMI NAWACHUKIA MAFISADI KWA MOYO YOOTE NA HATA WAKITAKA KUNIUA LEO NIPO TAYALI! JK KWA NINI ANASHINDWA KUACT KWENYE HAYO! MWAMBIE JK AFANYE KAZI AAACHE MBWEMBWE!

Mkuu,
Ni wewe uliyesema suala la upepo. Na usidhani kila mtu haipendi CDM, au ni mshabiki wa CCM,, ila tu pale ambapo amani inataka kutoweka nchini ndipo wengi hawaungi mkono. Mabadiliko ni jambo jema, lakini kwa njia ipi? Yaanze machafuko hata hiki kidogo tunachopata tukose? Masoko yatafungwa, maduka, mtu kama hajaweka chakula ndani cha mwezi au miwili ataishi vipi? Na watanzania wa kawaida maisha yao ni ya siku kwa siku. Tuone mbali tuache ushabiki.
 
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa watu tunataka kufanya mabadiliko ya kweli, hasa kwa njia ya mapinduzi ya nguvu za umma, hatuwezi tena kusubiri kura mpaka 2015.

Kikwazo kinakuja kwamba, tukitaka kufanya maandamano, serikali/CCM, itasingizia kwamba hawa ni CHADEMA, hata mimi nashawishika kwamba chama kikiongoza mapinduzi ya aina hii itaonekana kama ni uhaini/kupindua serikali, (treason) hata viongozi wake wanaweza kushitakiwa tukishindwa (hata kama watakua wameonewa).

Naomba sana serikali ya JK iifute CHADEMA kama ambavyo wameanza kutishia, tukishafanya mapinduzi, tukatengeneza katiba mpya chini ya jeshi then CHADEMA inaweza kuomba kusajiliwa tena upya, na viongozi walewale, ukombozi wa nchi uendelee, watakua wamekwepa lawama.

PEOPLESSSSSSSS..............

najaribu kulinganisha hilo jina lako na ulichokiandika.......
 
Wangefutwa wao kwanza kwa sababu bungeni wanalala tu hamna wanachokifanya mle. Wao lalishalamba 90m wanaona Tanzania haina shida. Mrema huyu huyu alikua mwanaharakati mzuri ila baada ya kupigwa adabu ya njaa amegeuka. Wao wawili wafutwe kabisa na sio vyama vyao.
 
Wivu wa kisiasa unawasumbua.

Hawa inaelekea bado hawajajua siasa ya vyma vingi. Bado wana mawazo ya udikteta wa chama kimoja.Wanataka Chadema ifutwe kwa misingi ipi, na ili iweje? Mafisadi wazidi kupeta na Watanzania wazidi kutaabika? Kimsingi, wao ndio wangefaa wafutwe!

Sent from my Apad using Tapatalk.
 
Wadau jana mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema na mwenyekiti wa UDP John Cheyo waliishambulia CHADEMA kwa maneno unayoweza kufananisha na matusi. Eti Mrema ameshauri CHADEMA ifutwe kwa sababu wanataka kuleta vita. Cheyo naye amesema CHADEMA wanataka kuleta mambo ya Libya na Misri.

Hivi kweli hawa ni wapinzani? Na kwanini wote wazungumze lugha moja kwa wakati mmoja. Imetokea kwa bahati mbaya? Eti Mrema anadai CHADEMA hawana uchungu na taifa hili na wanatumiwa na mataifa ya nje...
hawana sauti yoyote,,,,,waache wajiropokee walipwe posho zao!!!!
 
Mwaka huu mtaweweseka sana, katika sehemu zote walikopita Chadema ni wapi wamefanya fujo? kwanini serikali isitekeleze madai ya wananchi badala ya kutumia mbinu chafu kujaribu kuzoofisha maadandamano ya CDM....if it will never happen, mnachachawa nini sasa tulieni!![/QUOT

Sioni kitisho chochote kwa Chadema dhidi ya CCM,hawa mnawapa umaarufu tu.Tazama
Maeneo wanayofanya maandamano ni sehemu aidha wamepata wabunge(Mwanza,Musoma na Arusha) kwingine ni pale wanapoamini wanawafuasi (Shinyanga,Maswa,Kahama...n.k).Wahudhuriaji si wa kujaza uwanja wa taifa,wengine mkumbo,wengine njia ya kupora,watoto umri chini ya miaka 9 pamoja na Wazalendo ambao huwa ni kumsikiliza yeyote hata kama ni mpumbavu.Agenda ni Dowans na wala si kuuza sera zao ndio maana walipata watu.Hapa uwezi kusema CDM inatisha,ebu tuache hofu hawa ni wa kawaida sana na kama ni mtaji wa Misri na Libya.Wajaribu kuwambia hao wanaodhani people's power kuingia mtaani kupindua serikali kama watawaona kwa idadi hiyo zaidi ya vibaka tu.
 
Waache waifute ndipo watagundua kuwa watanzania wa leo sio mabwege tena. Wataikaribisha hali ya Libya mlangoni mwetu kwa spidi kubwa ya ajabu wakijaribu kufanya hivyo. Wanaweza kutuua kwa risasi za mtu wafuasi wa CHADEMA wote lakini matokeo ya kufanya hivyo bado yatafanya waifurahia maisha tena hasa ukizingatia muundo wa jamii za taifa letu ulivyo.

Naamini una ujumbe wa nguvu. Hatuwezi kuizuia serikali kuifuta CHADEMA kama wanataka kufanya hivyo. Waliifanyia mizengwe CCJ, wamefanyia mizengwe kanuni ya Upinzani rasmi bungeni na wakaifanyia mizegwe hoja ya Mhe Lema, na sasa wanafanyia mizengwe hoja ya Dowans. Shida hawajui kwa kina mwamko wa wananchi. Watanzania wa sasa wameamka sana katika kudai haki zao. Majukwaa yako mengi sana. Wakifanya hivyo wataamusha hasira za watz na cha moto watakiona.
 
Wamezoe kukurupuka waifute hata Leo, watakiona cha moto....CDM na wapenzi wengi kuliko CCM tena wengi wao vijana sasa kama wanataka vita waifute....
 
mkuu,
ni wewe uliyesema suala la upepo. Na usidhani kila mtu haipendi cdm, au ni mshabiki wa ccm,, ila tu pale ambapo amani inataka kutoweka nchini ndipo wengi hawaungi mkono. Mabadiliko ni jambo jema, lakini kwa njia ipi? Yaanze machafuko hata hiki kidogo tunachopata tukose? Masoko yatafungwa, maduka, mtu kama hajaweka chakula ndani cha mwezi au miwili ataishi vipi? Na watanzania wa kawaida maisha yao ni ya siku kwa siku. Tuone mbali tuache ushabiki.
mkuu bora wewe unapata kidogo heri kwako na unaweza kutibiwa ulaya ukiumwa eeeti! Bali sisi tunaotegemea huduma zoote kupata tz tunataka mabadiliko mkuu hii nchi nitajili mafisadi wameimaliza but not too late kuiokoa! Mkuu taahila yeyoote lazima aongozwe kwa viboko! Ndo serikali yetu hii!
 
Back
Top Bottom