Mrema katumia mil. 15 kukodi NYANI..

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Na Boniface Meena

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema amezuliwa jambo baada ya jarida moja la demokrasia kueleza jinsi alivyotumia fedha nyingi kukodisha nyani kwa ajili ya kuvutia watu kwenye kampeni zake za uchaguzi mwaka 2005.

Kwa mujibu wa jarida hilo lililotoka mwezi Oktoba mwaka jana ambalo limeandaliwa na Barak Hoffman na Lindsay Robinson wa Chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani, Mrema anadaiwa kutumia dola 15,000 za Kimarekani kukodisha nyani huyo.

Jarida hilo limeelezea kuwa kitendo hicho ni matumizi mabaya ya fedha za chama.

Lakini Mrema amekanusha tuhuma hizo akiziekezea kuwa zina lengo la kumchafua katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Jarida hilo limedai kuwa wakati Mrema akihama kutoka NCCR Mageuzi kwenda TLP mwaka 1999 alichukua baadhi ya mali za chama.

Alipohamia TLP jarida hilo limeeleza kuwa aliendeleza tabia yake aliyotoka nayo NCCR kwa kuwadharau viongozi wa TLP na kufanya matumizi mabaya ya fedha za wanachama ikiwa ni pamoja na kujinunulia nyumba, na wakati wa kampeni za 2005 alijitengea kiasi cha dola 98,000 za Kimarekani kwa matumizi yasiyo ya msingi.

"Kati ya kiasi hicho cha fedha alichojitengea, alitumia dola 83,000 za Kimarekani kununulia pombe wapigakura wake na dola 15,000 kukodisha nyani kwa ajili ya kuvutia watu kwenye kampeni zake. Lakini pamoja na yote hayo umaarufu wake uliendelea kushuka na alipata chini ya asilimia moja ya kura za urais," limeeleza jarida hilo.

Jarida hilo limeeleza kuwa wakati Mrema anaondoka CCM kwenda NCCR Mageuzi, alionyesha uhai upande wa upinzani kwa kuwa chama hicho tawala kilimwona kuwa ni tishio kwao na kwamba pamoja na kumkashfu katika kampeni zao, Mrema aliweza kupata asilimia 28 ya kura mwaka 1995.

Limeeleza kuwa pamoja na hayo, matendo ya Mrema yanafanya wapiga kura kuwa wagumu kumuunga mkono kutokana na kuvichanganya na kuvikoroga vyama vya upinzani ambavyo amewahi kuwa kiongozi.

Kabla ya kuhama CCM, Mrema ambaye hivi sasa ametangaza kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia TLP, aliwahi kushika nafasi tatu muhimu katika serikali, ikiwa ni pamoja na nafasi tata kikatiba ya naibu waziri mkuu katika serikali tofauti za CCM na kujipati umaarufu kwa kupambana na rushwa.

Baada ya kufukuzwa uwaziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana mwanzoni mwa mwaka 1995, aliamua kuhama CCM na kwenda NCCR Mageuzi ambako alipitishwa kuwa mgombea urais.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akubaliana na ripoti ya jarida hilo kuhusu Mrema akisema kuwa ni kweli wakati kiongozi huyo anaondoka chama hicho, tayari alikuwa amechanganya mambo mengi.

"Alipoingia NCCR hakutaka kusikiliza mtu na wale ambao walikuwa wakimpinga alisema kuwa wanatumiwa na CCM kitu ambacho alikuwa akikizungumza mara kwa mara,"alisema Mbatia.

Kuhusu matumizi mabaya ya fedha, Mbatia alisema kuwa Mrema alikuwa akisumbua kutokana na madai kuwa fedha za chama zinatokana na kura zake na ruzuku iliyopatikana hivyo ana mamlaka nazo.

"Katiba inaeleza kuwa katibu mkuu ndiye anayeshughulika na taratibu za chama pamoja na mambo ya fedha, lakini Mrema alikuwa hatambui hilo kwa kuwa anacho kitu ambacho anakiita Zidumu Fikra za Mwenyekiti ambazo zinamtesa na kutesa vyama alivyoviongoza hadi hivi sasa,"alisema Mbatia.

Alisema Mrema alisababisha mgogoro mkubwa ndani ya NCCR kutokana na msimamo wake wa zidumu fikra za mwenyekiti.

Lakini Mrema aliiambia Mwananchi kuwa hizo ni taarifa za kupikwa na watu ambao wanamchafua tena wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi kwa kuwa kuna watu wanaliwaza jimbo la Vunjo usiku kucha.

Alisema tuhuma hizo za matumizi mabaya ya fedha ni za uongo kwa kuwa hawezi kukodisha nyani kwa kiasi hicho cha fedha kwani mnyama huyo alikuwa ni mali ya kikundi cha kutumbuiza alichokuwa nacho kwenye kampeni.

"Sijawahi kutumia fedha za chama kama ripoti hiyo inavyoeleza, kuna ukaguzi umefanyika hivyo waje niwape ripoti ya ukaguzi na waache kupika mambo... uchambuzi wa matumizi hayo ni uongo,"alisema Mrema.

Alisema kuwa yeye ndiye mdhibiti mkuu wa matumizi ya fedha za chama na matumizi yanayofanyika lazima yapitishwe kihalali na kamati kuu.

"Hao watu hawakunihoji, hawajawahi kufika ofisini kutafuta ukweli ila wanapika mambo tu," alisema.

Alisema hajawahi kutumia fedha za chama kuwanywesha watu pombe kwa kuwa fedha za chama hazitumiki namna hiyo ambavyo imeelezwa.

Kuhusu tuhuma kuwa anavuruga upinzani, Mrema alisema yeye si kibaraka wa CCM kama wanavyoeleza bali anaimarisha upinzani kwa kazi anazofanya hivyo kwa kuwa hana haki ambazo aliziacha CCM ambazo akirudi leo atazipata.


CHANZO: Mwananchi 11 January 2010.
 
"Kati ya kiasi hicho cha fedha alichojitengea, alitumia dola 83,000 za Kimarekani kununulia pombe wapigakura wake na dola 15,000 kukodisha nyani kwa ajili ya kuvutia watu kwenye kampeni zake. Lakini pamoja na yote hayo umaarufu wake uliendelea kushuka na alipata chini ya asilimia moja ya kura za urais," limeeleza jarida hilo.

Habari hii kama ni ya kweli basi inazidi kumpaka matope Lyatonga wa watu, lakini jamani kukodi nyani kwa mil 15 mbona haiingii akilini, lakini haya ndiyo matatizo ya hela za ruzuku, hazina matumizi ya maana.
 
siasa za Tanzania kweli zinachekesha........Mrema kumbe anavituko siku nyingi ?
 
siasa za Tanzania kweli zinachekesha........Mrema kumbe anavituko siku nyingi ?

Mkuu,

Kiongozi aliyedumaza upinzani ni Mrema .... Alitumwa na CCM (Kama mtu wa Usalama pamoja na Mr "X" waanzishe vyama! na huo ndio ulikuwa mwaisho wa upinzania)
 
Nji hii wananichafulia jina babangu.
Yethu na maria...
Yule nyani hakuwa wa milioni kumi na tano.
Tulitumia hela ndogo kabisa ya tudola elfu kumi na tano tu.
 
Re: Mrema katumia mil. 15 kukodi NYANI..

Bujibuji, naomba kufahamishwa kama kwenye vyama vya Siasa vya hapa Tanzania huwa kunafanyika Audit.
 
Vyama vya siasa tanzania hakuna audit, vyote ni chukua chako mapema uondoke, nji hii akuna mwenye uchungu nayo kwa sasa!
 
Wanaweza wakafanyiwa audit ila ccm wanakimbiza sana account yao against mapato na matumizi.................
 
Re: Mrema katumia mil. 15 kukodi NYANI..

Bujibuji, naomba kufahamishwa kama kwenye vyama vya Siasa vya hapa Tanzania huwa kunafanyika Audit.

japo mi si Bujibuji:

wafanyiwa ukaguzi mkubwa....
 
Hii habari imekaa kishabiki zaidi na katika namna ya kumchafua Bwana Mrema kuelekea uchaguzi mkuu,tusipokuwa makini kuzitazama habari na kutambua malengo ya habari tunaweza kuja kutoa hukumu za kijinga.

Bwana Mrema alikodi kikundi cha sanaa kwenye mikutano yake ya kampeni,kikundi hicho pamoja na sanaa nyingine nyingi kilikuwa na Nyani,ngoma,sarakasi,maigizo na nk.Jiulize ni kwanini sanaa zote zimeachwa nyani ndio imekuwa issue.Mbona CCM wantumia mamilioni ya fedha hamtaki kuhoji?????.CHADEMA wanatumia vikundi vya sanaa kwenye mikutano wamewahi kutoa hesabu ya fedha wanayotumia.

Bwana Mrema ana matatizo yake kama iliyo kwa binadamu wote hakuna aliye kamili isipokuwa mwenyezi mungu tu.Leo ikitolewa hesabu ya kile kikundi cha TOT plus nakwambia kila mtu atashangaa tuache ushabiki wa kuchukia watu bila sababu za msingi.
 
Back
Top Bottom