Mrema: CCJ ni matokeo ya kongamano la kina Butiku

adui yako muombee njaa, maana CCM wamemuomba njaa Mrema na shetani kawasikia kamtia Lyaatonga njaa, nnjii bwana.
 
Naona huyu mzee anazeeka vibaya.

Hivi watu wa usalama wa Taifa wanajisema kweli? Akijisema sema hovyo mitaani kama Mrema sia anahatarisha maisha yake? Maneno ya Mrema yanatia shaka kama kweli ni mtu anayeweza simama kwa maslahi ya nchi yake ya Tanzania
 
What is CCJ? ikishapewa usajili tutajua tu waliomo, tuache speculation, tuwe na subira.
 
Tanzania ni huru na kila mtu yu huru mradi havunji sheria na katiba, mbona CCJ ni kitu ya kawaida tu na mkisikia ni chama cha bwana mkubwa mwenyewe anataka fanya ya mutharika mtasemaje?


Naomba Mungu iwew hivyo,Jk atakua hero wangu..but mhh!angeanza kuonyesha dalili za huo ujasiri
 
Hivi Mrema alipelekwa na nani vile kutibiwa India? Maana sidhani kama TLP inaweza kumgharamia kwa jinsi ilivyo jichokea
 
Bila shaka Mrema ameshapata uchovu wa kisiasa (political fatigue) baada ya ukweli kumdhihirikia kwamba katika Tanzania yetu hakuna political career nje ya CCM. Aidha, ameshakwenda mbali sana kuweza kurejea tena ndani ya Chama. Hivyo, kilichobaki ni kujaribu kujishikizashikiza tu. Wako wengine kama akina Wassira waliofanikiwa kurudi lakini hawa hawakuwa na stature ya Mrema. Kwa hali ilivyo sasa, TLP wajue hawana rubani na upinzani, kwa ujumla, umfute Mrema katika rasilimali zake. Na hakuna haja ya kumlaumu au kumkejeli sana zaidi ya kumuonea huruma tu.

Nafikiri Mh. Mbowe wa CHADEMA alikuwa na point aliposema kujenga upinzani Tanzania ni kazi ya maumivu sana. Mrema is now a spent force, could we say thanks to the nasty but brilliant strategy of the ruling party? Ona akina Maalim Seif & Co. kule Zenj wanavyotafuta njia mbadala baada ya kuugundua ukweli wa politiki za TZ. Imagine wapinzani kupigia chapuo hoja ya kumuongezea muda rais wa CCM!
 
Mrema ni B/S kabisa na nadhani ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha upinzani Tanzania.

Unfortunately mwaka 1995 nilipa kura yangu huyu Bogasi Mrema wakati akiwa NCCR-Magezui. Uchaguzi ule wa Oktoba ulinikuta nikiwa Dar ambapo niliweza kujiandikisha na kupiga kura yangu kwake baada ya kuhudhuria mkutano wake mmoja pale viwanja vya shule ya uhuru. Najuta sana kuwa nilipoteza hela yangu bure kwa kuendelea kukaa Dar eti ili nimpigie kilaza huyu kura yangu.
 
Code:
Tangu lini Mrema akawa mpinzani...sasa anajiibua mwenyewe kuwa ni pandikizi na boya la kuwaraghai watanzania. Hatujasahau kuwa enzi za utawala wa Mobutu kule Zaire alipandikiza makumi ya vyama feki vya upinzania!!!
Code:
Sasa mbona amekumbuka shuka Alfajiri?
 
mi nadhani umefika wakati mrema atafute mbinu mpya tushamgundua zamani kuwa ni kibaraka wa uharibifu wa hari ya hewa katika siasa za bongo, ye ndiyo alikuwa wa kwanza kushauri watanzania kuuheshimu umaruhani wa mwenzie shekhe yahaya toooooooooooka pepo mkuu wa kuzimu kwa jina la YESU huna mamlaka tena katika akili za watanzania
 
Na Waandishi Wetu

MWENYEKITI wa TLP, Augustine Mrema amesema Chama Cha Jamii (CCJ) kimeanzishwa ikiwa ni matokeo ya kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere inayoongozwa na Joseph Butiku, ambaye ameyaelezea madai hayo kuwa "upuuzi".

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mrema alisema vigogo wa CCM waliozungumza kwenye kongamano hilo na kutamka wazi kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kufanya maamuzi magumu, ndiyo waanzilishi wa CCJ.

CCJ ni chama kipya cha kisiasa ambacho kuanzishwa kwake kunahusishwa na mkakati wa vigogo na baadhi ya wabunge wa CCM ambao hata hivyo hadi leo hawajajitokeza hadharani.

Mrema, ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kabla ya kutofautiana na mawaziri wenzake mwaka 1995 na kujiunga na chama pinzani cha NCCR Mageuzi, alidai kuwa ametumia mbinu zake za usalama wa taifa kuwatambua vigogo hao.

Bila kuwataja kwa majina, Mrema alisema vigogo hao wanatumia mwamvuli wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuandaa makongamano kwa nia ya ya kumtukana na kumhujumu Rais Kikwete.

"Wanatumia mwavuli huo kumtukana rais kwamba anazungukwa na wezi na kwamba hana maamuzi magumu wakati wenyewe hawana maamuzi hayo," alisema Mrema.

"Ni aibu kwa vigogo hao wa CCM tena wanaojifanya kuwa wapo chini ya mwamvuli wa Tasisi ya Baba wa Taifa kuandaa makongamano ya kumtukana rais wetu hadharani wakati wenyewe pia hawana mamuzi magumu na kama wanayo basi wajitangaze hadharani kuwa wao ndiyo CCJ," alisema Mrema.

Mrema, ambaye alikuwa nchini India kwa matibabu na ambaye alikanusha kuwa safari yake ilidhaminiwa na Kikwete, alisema: "Kumwambia rais maneno makali kama hayo tena hadharani ni kutaka wananchi wamdharau na kumwona mwizi pia na kimsingi huu ni uhaini.

"Nimetumia uzoefu wa taaluma yangu ya Usalama wa Taifa na kubaini machafu yanayofanywa na vigogo... simtetei Kikwete bali natetea rais yeyote wa taifa hili siyo Kikwete tu kama wanavyosema nipo kwenye mtandao wa Kikwete na wengine kudai kuwa nimenunuliwa.

"Kikwete hawezi kuninunua; mimi ni mtu wa gharama sinunuliki, ila kwenye ukweli panastahili kuzungumzwa; natumia taaluma yangu kutetea taifa, siwezi kuona taifa linayumba halafu nikae kimya; mimi na mkurugenzi mstaafu wa Usalama wa Taifa bwana."

Hata hivyo, hakueleza alikuwa mkurugenzi wa kitengo gani cha Usalama wa Taifa.

Mrema aliongeza kusema: "Siingii jikoni kupika, lakini nina utaalamu wa kupika. Ninataka wale vigogo wanaomhujumu rais kwa maneno ya kijeli, kama wana uwezo na kujiamini wajitokeze hadharani wasema wao ndiyo wenye CCJ."

Hata hivyo mwenyekiti wa taasisi hiyo, Joseph Butiku alipuuza madai hayo ya Mrema akisema hawezi kuzungumzia upuuzi.

"Sitaki kuulizwa maswali yasiyo na maana; nenda kamuulize aliyekwambia upuuzi huo," alisema Butiku.

Katika hatua nyingine wakati Mrema akitoa tuhuma hizo nzito, CCJ imeanza mapambano kupigania usajili wake kwa kumhoji Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa sababu za kushindwa kuwapa usajili wa muda.

Tamko hilo la CCJ kwa Tendwa limekuja katika kipindi ambacho Msajili amekuwa akisisitiza kuwa uwezekano wa chama hicho kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 haupo kwa sababu muda hautoshi kwa chama hicho kukamilisha taratibu zote ili kipate usajili wa kudumu.

Usajili wa muda, ambao unahusisha chama kipya kitafuta angalau wanachama 200 kutoka mikoa 10 au zaidi, huchukua miezi sita ambayo hufuatiwa na uhakiki unaofanywa na Msajili kabla ya kupata usajili wa kudumu.

Tendwa alisema hata kama chama kipya kitakamilisha sharti hilo la kwanza katika muda mfupi, sheria ya miezi sita inabakia kama ilivyo.

Ndani ya kipindi hicho cha usajili wa muda na uhakiki, Tume ya Uchaguzi itakuwa imeshaanza taratibu za uchaguzi kwa kuruhusu wagombea waliopitishwa na vyama vyao kuanza kuchukua fomu.

Lakini uvumilivu uliwashinda CCJ ambao jana walimshukia Tendwa wakidai kuwa anadhofiisha mipango hiyo ya kukipa chama usajili wa muda kwa malengo anayojua mwenyewe.

Renatus Muabhi, ambaye ni katibu mkuu wa CCJ, alitoa tamko linalosema: "Hali iliyopo sasa imesababisha viongozi pamoja na wanachama watarajiwa wa CCJ kuwa katika hali ya utata na kuhofia mustakabali mzima wa upatikanaji wa usajili wa muda wa CCJ.

"Tunapata taarifa za maelezo ya msajili wa vyama vya siasa nchini yanayokinzana na wajibu wake kupitia vyombo vya habari pasipo sisi kuwa na taarifa yoyote inayoonyesha hatua ipi imefikiwa juu ya usajili wa CCJ.

"Kwa mfano, tarehe 26/01/2010 siku ya Jumanne gazeti la Daily News lilichapisha maneno ya msajili ambayo kwetu sisi yanatuingiza katika utata na hofu juu ya usajili wa chama chetu."

Tamko hilo linaendelea kueleza kuwa Tendwa anakwenda kinyume na taratibu pamoja na dhamana aliyopewa na kuhakikisha kwa vitendo ya kwamba nchi ya Tanzania ni ya kidemokrasia na inayofuata mfumo wa vyama vingi, badala ya kuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu kuunda na kujiunga katika vyama vya siasa ili kuleta demokrasia ya kweli.

Linamtuhumu Tendwa kuwa anakatisha tamaa na kuwavunja moyo Watanzania kuhusu tafsiri ya kuanzishwa kwa CCJ hasa pale anaposema chama hicho ni sawa na vyama vingine vilivyopo.

Habari hii imeandaliwa na Ramadhan Semtawa, Mussa Mkama na Minael Msuya.

SOURCE: Mwananchi
Hivi alipokwenda India hakupimwa na akili yake kama iko sawa sawa? Hapo alipata tiba ya ugonjwa gani maana naona ugonjwa wa kisukari ulikwisha athiri na ubongo wake. Si bure.
Naona sasa anatutishia na usalama wa taifa sijui anadhani ni enzi zao walivokuwa wanatutisha kwa kuhesabu vizibo vya soda na bia tunazokunywa?
Leo hiyo si kazi ya kutishana Mrema. Umekwishnei.
 
kila mtu alikuwa anajua kuwa Mrema akirudi lazima aropoke. si arudi CCM basi tujue moja.
 
""Kuna sources zinasema kuwa CCJ ni creation ya Rostam, ni 'red herring' ili kuwafanya watanzania kuacha kufuatilia mambo muhimu yaliyopo kwa sasa kama Utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu mkataba wa kifisadi wa Richmond"" Kama ni kweli basi haka kagabachori ni ka thinker!
 
""Kuna sources zinasema kuwa CCJ ni creation ya Rostam, ni 'red herring' ili kuwafanya watanzania kuacha kufuatilia mambo muhimu yaliyopo kwa sasa kama Utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu mkataba wa kifisadi wa Richmond"" Kama ni kweli basi haka kagabachori ni ka thinker!


Sources zipi zitaje
 
anayoyaongelea mrema sometimes yakipuuzwa yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi...tuchukulie mfano huko madagasca nchi haina amani..WHY..kwasababu the current president Rajoelina was a DJ kwenye redio moja..nae alikuwa akisema maneno ya uchochezi kwenye redio kwamba raisi Ravolonmana ni mwizi, fisadi hafai and so on. then wat happen, wananchi wakaona hawawezi kuongozwa na raisi fisadi. wakishirikiana na DJ and the army, the president was cast out..then they made Rajoelina the president. wakati anaapishwa he was only 33 yrs old kinyume na katiba ya madagasca....na mpaka sasa nchi haina amani.

what i am tryn to say, Butiku and the rest wangeweza kusema hayo maneno kwenye halmashauri ya CCM or kamati kuu ya CCM kwa sababu yanamuhusu bosi wao. sasa wao wakaropoka tu.kikwete amezungukwa na wezi, the president is compromised, raisi hawezi kufanya maamuzi mazito, 2010 tumtose

maneno kama haya ni ya uchochezi, na wanatuambia wananchi ili tufanye nini, kwamba kikwete hatufai tuwachague wapinzani, or what. wanataka sisi tumchukie raisi pekeyake or CCM kwa ujumla, sasa tukimtosa raisi tumweke nani?

thats my opinion on what Mrema is tryn to say. na hiyo CCJ nmesikia inawahusisha watu wa rwanda or burundi not sure...


but wat i no for sure 2010 will be the year tanznians we will never forget.....
 
Back
Top Bottom