Mrema awaponda CHADEMA live Bungeni

Kuna wabunge ukisikia wanatajwa kwenye orodha ya kuongea inabidi ikifa zamu yake ubadilishe channel kwanza mpaka amalize bcse the end of the day atakuboa tu! mmojawapo ni huyo Lyatonga. Ameshachoka kisiasa akapumzike
 
Hua napenda kuangalia Prime ministers question bunge la uingereza. Liko entertaining cos ni utani mtupu japo hoja hutolewa. Wabunge wetu wanaboa na hoja zao za kukopy and paste. Mrema knows how to entertain and get you Shmucks to talk bout him and the papers to write about him. Chadema hampendi lakini Hutu kweli ni mwanasiasa
 
Jaman hivi katika watu Mrema nae ni mtu???? Ni kumsamehe tu kwani nae sie. yule hata akiongea kitu cha maana hawez kuwa considered kwani tushamtoa kwenye watu na kumgroup kwenye ignore list. Mrema yupo duniani kama hayupo duniani vile.
 
Dah huyu jamaaa hana tena Sera kasema ana siri nyingi sana za Serikali akiwa naibu waziri so wamlipe aitetee serikali (CCM)
 
Hizo ni dalili za mtu anapokaribia kufa. Mrema yuko karibu kabisa na kaburi, kimwili na kimawazo.
Natoa wito kwa wanachama wa tlp tz nzima wajiondoe kutoka ktk chama hicho na kumwacha mrema pekee. Msipo utii wito wangu, basi ninyi nyote si wapiganaji bali ni waganga njaa. Endeleeni.
 
Hizo ni dalili za mtu anapokaribia kufa. Mrema yuko karibu kabisa na kaburi, kimwili na kimawazo.Natoa wito kwa wanachama wa tlp tz nzima wajiondoe kutoka ktk chama hicho na kumwacha mrema pekee. Msipo utii wito wangu, basi ninyi nyote si wapiganaji bali ni waganga njaa. Endeleeni.
umetoa kauli mbaya sana mkuu,humu jf wa2 2napondana bt hakuna anae mponda mwenzie kama wewe ulivofanya,kifo kipo ndio lakn co kumzungumia mwenzio hvo bana.
 
Mh.Mrema Njaa itamuua,anaifagilia serekali ya CCM kwa sababu ya njaa tu!!!
 
Nimesikia akitoa reference ya Misri na Madagascar na kwingineko kuwa hali sasa ni mbaya ya kimaisha. Hii si sauti ya mpiganaji kwani mwanamapinduzi yeyote atakubaliana nami kuwa ukombozi wa nchi una gharama zake. Nilisema huko nyuma na narudia tena, CCM haiwezi kuondoka kwa sanduku la kura. Ni lazima maandamano yaimarishwe na JK aondolewe madarakani, ndiyo baada ya hapo hali itakuwa mbaya, lakini uzalendo utakuwa umejengwa na given time chini ya serikali yenye utawala bora hali itatengemaa. Bila maandamano hakuna ukombozi wa kweli. Mrema akae apumzike tu, na ajue hakika kuwa wakati ni ukuta. Peoples power kwa kwenda mbele.

Aluta Continue CDM.
 
Muda mfupi uliopita mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema ametoka kuchangia hotuba ya bajeti ya Waziri mkuu! Nimemuangalia na kumsikiliza kwa makini sana na nikajikuta namuonea huruma sana! Ameanza kwa kuponda sana mikutano na maandamano ya CDM kwa kisingizio kisicho na mashiko cha amani kama wanavyotumia wenye chama cha magamba! Akanukuu habari inayozungumzia hali ilivyo nchini Misri kwamba watalii hawaendi na uchumi unaelekea kubaya! Akabwabwaja utumbo mwingi akizitaja nchi kama Tunisia, Libya, Misri, Kenya na nyinginezo akijaribu kuboresha hoja yake! Kumbe muda wote huo alikuwa akijikomba kwa Chama cha magamba kwa sababu baada ya hapo akadai kuwa yeye alikuwa NAIBU WAZIRI MKUU kwa hiyo apewe mafao yake ya nafasi hiyo. Bila ya aibu aksema "MMENIFUNDISHA MAMBO MENGI, NAJUA MAMBO MENGI, KWA HIYO MKITAKA NIENDELEE KUTETEA MAMBO YA NCHI HII NIPENI HAKI YANGU". Ina maana kuwaponda CDM na kuunga mkono hoja kwa 100% ilikuwa ni kuwatetea ili wampe mafao ya UNAIBU WAZIRI MKUU FEKI! Huyu mzee njaa itamuua!
 
Mrema ni kada wa siku nyingi wa CCM, ameshindwa kueleza ni lini alirudisha kadi na kampa nani. Hata jimbo la Vunjo sote tunajua kwamba kapewa makusudi baada ya kuliomba siku ya mkutano mkuu wa CCM ambapo alihudhuria. Na wamemzawadia kamati nzito ya LAAC, sasa hv anakula tu na wakurugenzi wa halmashauri. Kwa nini asiiponde CHADEMA. Hata ukajaribu kumsikiliza, hana hoja, anaongea kwa kurudia rudia, hafanyi maandalizi ya kujenga hoja, amechoka sana kisiasa.
 
Anataka mafao kama naibu waziri mkuu mstaafu,jamaa kachizika

A man without soul! Kama anataka mafao aseme waziwazi lakini asitumie CHADEMA (kwa kuwaponda CDM) kama daraja la kuombea pesa. Huko nyuma Mrema alifanikiwa sana kusambaratisha vyama vya upinzania ili kuwafurahisha mabosi wake-ccm kwa hii tabia yake ya u-ndumilakuwili. Lakini kwa mshangao bado huyu mufilisi anaonekana kuegemea hii mbinu chovu na yenye ku-mfedhesha yeye kama mwanaume na kama mwakilishi wa wana-vunjo. Aibu iliyoje kwa mtu mzima kutojuwa unasimamia nini?

Kama analaani maandamano tafsiri yake anatulaani sisi watanzania tulipigika kimaisha tuakaamuwa kuweka hisia zetu hadharani ili watawala wajue wametukosea. Anatulaani kwa sababu tumetaka bei ya sukari ishuke? au ametulaani kwa sababu tumetaka police watulinde badala ya kutulia watoto wetu kwa kisingizio cha kudumisha amani nutulivu kwa wawekezaji? Mrema anatoa wapi ujasiri wa kulaani maandamano ambayo hata kikatiba yana ruhusiwa? Lakini Mrema anatakiwa ajue kwamba hata kama serikali ya mashoga zake -ccm watampa mafao anayodai atakuwa ameuza si tu utu wake bali pia atakuwa ameridhia serikali inayonyonya wananchi wake, inayojali maslahi ya wachache huku umma ukiishi kwa 'kubaingaiza' na mbaya zaidi Mrema atakuwa ameridhia serikali inayouwa raia wake wasio na hatia. Mrema anafanya yote haya ili apate mafao kama kiongozi mufilisi-mstaafu. It is called 'Bloody Money'.
 
Hua napenda kuangalia Prime ministers question bunge la uingereza. Liko entertaining cos ni utani mtupu japo hoja hutolewa. Wabunge wetu wanaboa na hoja zao za kukopy and paste. Mrema knows how to entertain and get you Shmucks to talk bout him and the papers to write about him. Chadema hampendi lakini Hutu kweli ni mwanasiasa

There is nothing entertaining kwa mwanaume mzima kulamba miguu ya mwanaume mwingine. Is sucks! Mrema aliomba kura kutetea wanavunjo au kusifia ccm bungeni? The man is completely out of order!
 
Ni muhimu kuwachuja wapinzani uchwara. Leo wanafanya hiki kesho wanakemea kile. Unaweza ukamsamehe Mrema sababu ya uzee na ugonjwa lakini sio msomi kama Hamad Rashid. Purukushani zote za ngangari na jino kwa jino na maandamano ya kutosha yaliyopoteza hadi maisha ya watu, leo Rashid anaponda maandamano ya chadema na kusema wafanye usiku. Anayasema hayo wakati hata chama chake kilikuwa kinapanga kufanya maandamano kupinga yaliyotokea TBR. Hawa ndo wapinzani wetu!
 
Alishafika kileleni sasa anashuka chini - memory pamoja na nguvu ya kutengeneza hoja hamna tena.
 
Mrema ameamua kuwa kichekesho! kumbe maneno yoote yale ilikuwa kujaribu kuitisha serikali au la sivyo hata watetea tena kuhusiana na issue ya maandamano,alicho gundua mrema ni serikali kuogopa maandamano sasa yeye anajionesha kwamba ana dawa ya kudhibiti maandamano!

Mrema watanzania wa sasa sio wale wa enzi zako,wengine hawakujui ulikuwa na umaarufu gani ambao hata hivyo nao kumbe ulikuwa ni msaliti mkubwa na mnafiki tu,utatuambia nini watanzania wa leo wakati ulishachezea wakati wako! wewe sasa ni mtu wa kale wala hatukusikilizi unaonekana kama comedi tu mchekeshaji umeongea na umeonekana kituko tu!
 
Zama za Mrema zimeshapita kale...uwepo wake bungeni leo ni hisani ya wana Vunjo kwa aliyowatendea kipindi akiwa "Mheshimiwa Mrema"...Hana jipya!
 
Back
Top Bottom