Elections 2010 Mrema amtimua Mwenyekiti wa Kijiji

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
MWENYEKITI wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Agustine Mrema (TLP), amemvua madaraka Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyala, Kata ya Marangu Magharibi, Agustino Fabiani kwa madai ya unywaji wa pombe haramu ya gongo.

Mrema ametoa uamuzi huo wakati wakiwa katika operesheni maalumu ya Ulinzi Shirikishi kwa lengo la kukabiliana na uhalifu na ujambazi katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Mwanasiasa huyo ni Mbunge wa jimbo hilo. Katika operesheni hiyo ambayo ilifanywa kwa ushirikiano na Polisi, timu hiyo ya viongozi ilipita katika baadhi ya vijiji katika jimbo hilo na inadaiwa ilimkuta Mwenyekiti huyo wa Kijiji akiwa amelewa.

Mrema alidai kuwa, pamoja na kwamba Mwenyekiti huyo alikuwa mwanachama wa TLP, lakini yeye hawezi kulea viongozi aliodai hawana maadili kwa kuwa watazorotesha maendeleo ya wananchi.

Mbunge huyo alidai kuwa, taarifa za wanakijiji alizonazo zilieleza kuwa Mwenyekiti huyo alikuwa akisikika akiwahamasisha wananchi wanywe pombe hiyo kwa kuwa haina madhara kwa madai ni sawa na bia zilizopimwa kitaalamu.

“Mimi ni Mbunge wa wananchi wote wakiwemo wasio na vyama..nikimtetea huyu Mwenyekiti, wananchi hawatapata maendeleo, nimemvua madaraka yake ili iwe mfano kwa viongozi wengine wasio na maadili,” alisema.

Wakati wa operesheni hiyo ilibainika kwamba Kijiji cha Nganjoni ni kitovu cha utengenezaji wa pombe hiyo baada ya kukutwa kwa mitambo ya utengenezaji pombe hiyo huku wananchi wa eneo hilo wakihama makazi yao kwa hofu ya kutiwa mbaroni.

Mrema alisema, Jimbo la Vunjo limeathiriwa na vitendo vya uhalifu kutokana na kukithiri kwa uzalishaji wa pombe hiyo pamoja na unywaji wake na uvutaji wa bangi, hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa huku baadhi ya ndoa zikivunjika na wazazi kuacha kupeleka watoto shule.

Mbunge ana mamlaka ya kisheria kumvua madaraka Mwenyekiti wa Kijiji aliyechaguliwa kwa kupigiwa kura?Naombeni ufafanuzi tafadhali kwa hilo!

Hii aliyofanya Mrema ipo ndani ya uwezo wake kikatiba?
 
kumbe mbunge ana uwezo wa kumfukuza mwenyekiti wa kijiji?
kama ni kitu cha kweli basi angalau mrema anaanza kufurukuta
 
Mh!jambo la ulinzi shirikishi na kusisitiza uzembe wa mwenyekiti wa kijiji cha TLP si kitu kizuri na hakivumiliki,hapa mrema alifanya kazi nzuri.Wasiwasi wangu tu hivi katiba ya TLP inaruhusu mwenyekiti wa taifa kumvua madaraka mwenyekiti wa chama ngazi ya kijiji!hiki ni kichekesho!
 
Hii imekaa kimtego sana!
1. M/kiti Taifa TLP kamvua uanachama wa TLP na hivyo kupoteza wadhifa wa mwenyekiti wa kijiji kupitia TLP?
2. Mbunge Vunjo kamvua uenyekiti wa kijiji huyo mtuhumiwa

Wenye ufahamu na katiba ya TLP au madaraka ya mbunge watupe ufahamu tafadhali
 
Mumpe au msimpe wizara yake yeye anatwanga mzigo. Twende kazi mrema!
 
Mbunge ana mamlaka ya kisheria kumvua madaraka Mwenyekiti wa Kijiji aliyechaguliwa kwa kupigiwa kura?Naombeni ufafanuzi tafadhali kwa hilo!
Hii aliyofanya Mrema ipo ndani ya uwezo wake kikatiba?

Linapokuja suala la uwajibikaji itifaki inawekwa pembeni...kitendo alichofanya mwenyekiti wa kijiji si cha kuvumilika hasa kwa wakati huu tukiwa na kasi iliyodorora kuelekea malengo ya milenia..heko mzee wa kiraracha!
 
Mbunge ana mamlaka ya kisheria kumvua madaraka Mwenyekiti wa Kijiji aliyechaguliwa kwa kupigiwa kura?Naombeni ufafanuzi tafadhali kwa hilo!

Hii aliyofanya Mrema ipo ndani ya uwezo wake kikatiba?
Mwenyekiti ni mwanachama wa TLP , na Mhe. Mrema ni mwenyekiti wa TLP hivyo nadhani anayo mandate ya kushughulikia uovu kama huo.
 
Mbunge ana mamlaka ya kisheria kumvua madaraka Mwenyekiti wa Kijiji aliyechaguliwa kwa kupigiwa kura?Naombeni ufafanuzi tafadhali kwa hilo!

Hii aliyofanya Mrema ipo ndani ya uwezo wake kikatiba?

Akimvua uanachama wa TLP atakuwa amepoteza cheo chake cha Mwenyekiti wa Kijiji kwani alipitishwa na chama chake cha TLP kugombea hicho cheo. Lakini sijui katiba ya TLP inasemaje kuhusu taratibu wa kuchukuliana nidhamu, hakuna vikao vya kamati ya nidhamu au ni mwenyekiti tuu anajiamulia?
 
MWENYEKITI wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Agustine Mrema (TLP), amemvua madaraka Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyala, Kata ya Marangu Magharibi, Agustino Fabiani kwa madai ya unywaji wa pombe haramu ya gongo.

Mrema ametoa uamuzi huo wakati wakiwa katika operesheni maalumu ya Ulinzi Shirikishi kwa lengo la kukabiliana na uhalifu na ujambazi katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Mwanasiasa huyo ni Mbunge wa jimbo hilo. Katika operesheni hiyo ambayo ilifanywa kwa ushirikiano na Polisi, timu hiyo ya viongozi ilipita katika baadhi ya vijiji katika jimbo hilo na inadaiwa ilimkuta Mwenyekiti huyo wa Kijiji akiwa amelewa.

Mrema alidai kuwa, pamoja na kwamba Mwenyekiti huyo alikuwa mwanachama wa TLP, lakini yeye hawezi kulea viongozi aliodai hawana maadili kwa kuwa watazorotesha maendeleo ya wananchi.

Mbunge huyo alidai kuwa, taarifa za wanakijiji alizonazo zilieleza kuwa Mwenyekiti huyo alikuwa akisikika akiwahamasisha wananchi wanywe pombe hiyo kwa kuwa haina madhara kwa madai ni sawa na bia zilizopimwa kitaalamu.

"Mimi ni Mbunge wa wananchi wote wakiwemo wasio na vyama..nikimtetea huyu Mwenyekiti, wananchi hawatapata maendeleo, nimemvua madaraka yake ili iwe mfano kwa viongozi wengine wasio na maadili," alisema.

Wakati wa operesheni hiyo ilibainika kwamba Kijiji cha Nganjoni ni kitovu cha utengenezaji wa pombe hiyo baada ya kukutwa kwa mitambo ya utengenezaji pombe hiyo huku wananchi wa eneo hilo wakihama makazi yao kwa hofu ya kutiwa mbaroni.

Mrema alisema, Jimbo la Vunjo limeathiriwa na vitendo vya uhalifu kutokana na kukithiri kwa uzalishaji wa pombe hiyo pamoja na unywaji wake na uvutaji wa bangi, hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa huku baadhi ya ndoa zikivunjika na wazazi kuacha kupeleka watoto shule.

Mhe. Mrema ni mwanzilishi wa mambo haya ya ulinzi shirikishi hapa Tz, hakika yeye ni mtu aliyebobea kweye haya ya ulinzi ( covert and overt security )
 
Mrema ana ugonjwa wa kulewa madaraka. Sasa haya ya ubunge yameanza kumlewesha na kabla ya mwaka kupita ataanza kutembea uchi kutokana na ulevi huo wa madaraka.
 
big up mrema...big up ulinzi...big up tanzania....DEMOKRASIA HUDAMAZA MAENDELEO,DISCUSS
 
Bwana we, ukisema mrema amevunja katiba mi nitakuambia bora avunje kwa kuondoa maovu kuliko ailinde na maovu yake
 
tungekuwanaviongozi kamaainayamurema maendereo yasingesuwasuwa kunakiongozi mwingine ariwacharazaviboko warimu ikaonekanaamekoseya reokitaifa yamwisho inatakiwatupateviongoziwakuwawajibisha viongoziwazembe kazabuti ushauri usiishie daga na papa wapo
 
Back
Top Bottom