Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema, ametoa malalamiko bungeni akiitaka serikali kumlipa posho zake za kustaafu cheo cha Naibu Waziri Mkuu alichopewa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi katika miaka 1990.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mrema, alitoa malalamiko hayo alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, bungeni, mjini hapa jana.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema ili aweze kuwa mdau mzuri wa kutetea amani ya Tanzania ana kila sababu ya kulipwa stahiki zake kutokana kuwa na cheo hicho.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Asilimia 80 ya mafao yako, nipeni basi hata asilimia 20, alisema Mrema na kusababisha karibu ukumbi mzima wa Bunge kulipuka kwa kicheko. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kuna hoja zinazojaribu kutolewa kutaka kuzuia apewe stahiki yake hiyo kwamba, cheo cha Naibu Waziri Mkuu alichopewa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, hakimo kwenye Katiba ya nchi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mrema, ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani sambamba na cheo hicho na baadaye Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana katika serikali ya awamu ya pili ya Mwinyi, alisema anavyofahamu ni kwamba, Rais ndiye anayeanzisha cheo hivyo, hoja za watu hao hazina msingi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Alisema anashangaa kuona posho za majenerali wa jeshi zinapojaribu kuguswa kunakuwa hapakaliki na kuhoji Kwanini Mrema mkimnyima mnaona sawasawa?. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Msije mkaona Simba amenyeshewa mkafikiri nyani. Nyinyi mmenifundisha mambo mengi najua vitu vingi. Sasa kwanini haki zangu hamnipi? alisema Mrema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliongeza: Kwa hiyo, naomba serikali hii na hasa Waziri Mkuu ili niendelee kutetea mambo mengi ya nchi hii, naomba haki yangu mnipe.[/FONT]
CHANZO: NIPASHE