Elections 2010 Mrema aapa kuivuruga Chadema

Au ana ota hizi nyakati....siku hizi hazipati tena

2494140.jpg

Anaota ndoto za mchana!! This will never come again!!!

Kafie mbele AM!!!
 
Malisa, alisema kwa miaka 10 sasa Chadema imeongoza jimbo hilo, lakini hakuna mabadiliko yoyote yaliyopatikana zaidi ya wananchi kubaki mashabiki wa chama hicho
ccm wameongoza Taifa hili miaka zaidi ya 40, bila kuleta mageuzi haswa kimaisha na wala mabadiliko kwanini wastahili kuongezewa Muda....
 
Mrema suti na Raba mtoni wapi na wapi??? baaangu. Inabidi wajanja wafuatilie Muhimbili psychiatric department huenda mzee mzima analo file la kale kagonjwa na dose anapata kama kawa.Chunguza Utabaini mjomba

Duh!kaali kwelikweli.
 
Unapokuwa na ndungu yako anafanya mambo kiwenda wazimu hasusani kiongozi inabidi umwondoe kwenye public na umtafutie wataalam, hii ilimkutaga aliyekuwa PM wa UK Margaret Thatcher(Iron Lady).Sasa ndugu zake Mrema sijui wako wapi kwenye hili.
 
Mkuu,
Mrema ni usalama wa taifa in action kuwavuruga wapinzani. Hiyo ndo kazi aliyotumwa na CCM akafanye huko upinzani.
Sidhani kama usalama wa taifa wanamwitaji mtu kama Mrema anayekwenda majukwaani na kusema yeye ni uwt.
 
Mrema kwa kuiunga mkono CCM alidhani atapata mteremko wa ubunge kule Vunjo. Bahati mbaya CCM nao wakasimamisha mgombea. Ukafanyika mdahalo TBC, Mrema alivurunda kama kawaida yake. matokeo yake Wagombea wa Chadema na CCM walin'gara sana.

Kitakachotokea Vunjo, CCM na TLP watagawana Kura na si ajabu Mgombea wa Chadema ndiye akawa mshindi. (time will tell) an hiki ndicho kinachomsumbua Lyatonga mpaka kuanza kulialia sasa hivi.
 
Huyu kachanganyikiwa

mrema chizi

Huyu mzee, wala huwezi kutia neno kwake. Ana wazimu na yuko desperate kuingia bungeni akalale vizuri.

Hatuchagu wagonjwa sisi, naamini hata Vunjo wanaamini hivyo. Mwache alie lie tu...:biggrin1:

Baba Mpumbavu anayeua watoto wake, ni vyema afe tu....ndiyo salama ya watoto

Mrema nae kawaambia hivi
"Alisema anashangazwa na upinzani uliopo sasa miongoni mwa vyama vya upinzani, kwani havijalenga kuchukua madaraka ya nchi, bali kushambuliana, jambo linalozidi kuvidhoofisha na kuiacha CCM ikitamba"
 
Ndo maana kofia yake huwa haitoki kichwani ana kovu lilisababishwa na ajali kwa hiyo kichwa yake haiko musuri
 
BAADA ya kulia na propaganda chafu za Chadema, mgombea ubunge katika Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP, Augustino Mrema, amesema anapanga kujibu mapigo kwa kuhamishia nguvu zake katika majimbo matatu ambako Chadema wana matumaini ya ushindi.

Amesisitiza kwamba, haendi kwa bahati mbaya, bali kuwavurugia kama chama hicho kinavyomtibulia mipango yake ya kuingia bungeni, baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31.

Mrema alisema hayo jana kwenye Viwanja vya Majengo Sokoni, mjini hapa, wakati akimnadi mgombea ubunge wa TLP Moshi Mjini, Godfrey Malisa.

Alisema kutokana na kufanyiwa siasa chafu na Chadema, sasa chama chake kitahakikisha kinaelekeza nguvu Hai (Freeman Mbowe), Moshi Mjini (Philemon Ndesamburo) na Vunjo (John Mrema).

Mrema alisema madhumuni ya kuelekeza nguvu katika majimbo hayo, ni kutokana na alichokiita upinzani wa kinafiki unaofanywa na Chadema, ambapo alisema kauli ya Chadema kuwa Mrema atakwenda kufia bungeni, ni matusi huku akisisitiza kwamba hakuna mtu asiyekufa na kutaka aachwe akafie huko.

Aliwaonya mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, Mwenyekiti Mbowe na Ndesamburo kutokanyaga jimbo la Vunjo.

Alisema wakikaidi, waende kistaarabu, lakini wakiendelea kumchezea rafu za kisiasa, atahakikisha kati yao hakuna anayeshinda katika uchaguzi mkuu, kwani atafanya kampeni za nguvu kuhakikisha anagawa kura za Hai na Moshi Mjini.

"Kama wao wanadai kuwa mimi ni mzee eti niwaachie vijana, sasa mimi niulize kati ya Kikwete na Dk. Slaa, nani mzee?... inatakiwa Slaa amwachie Kikwete uongozi, kama Slaa anataka kwenda Ikulu atafia huko nami nifie bungeni, mbona kuna wabunge wanafia humo?

"Kama Chadema inavyogawa kura zangu Vunjo, vivyohivyo nami nitahakikisha Mbowe, Mrema na Ndesamburo, hawanusi Bunge … nitafanya kampeni kubwa katika majimbo yao, kuhakikisha TLP inakuwa na wapiga kura wengi, ili kuzuia ushindi wanaotarajia Chadema, nitahakikisha hadi kinaeleweka," alisema Mrema.

Alisema anashangazwa na upinzani uliopo sasa miongoni mwa vyama vya upinzani, kwani havijalenga kuchukua madaraka ya nchi, bali kushambuliana, jambo linalozidi kuvidhoofisha na kuiacha CCM ikitamba.

Malisa, alisema kwa miaka 10 sasa Chadema imeongoza jimbo hilo, lakini hakuna mabadiliko yoyote yaliyopatikana zaidi ya wananchi kubaki mashabiki wa chama hicho.

Alisema tatizo la wananchi wa Moshi ni kudanganywa na gari la kubebea wagojwa la Hospitali ya Mkoa, Mawenzi, ambalo lilitolewa na Ndesamburo, ambalo kwa sasa alidai ni bovu na halijafanyiwa matengenezo.

Pia aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua, akisema akipewa ridhaa atahakikisha viwanda vilivyoshindikana kufufuliwa na Chadema vinafufuliwa, ili kutoa ajira kwa wakazi wa Moshi.

Source: Habari Leo

Angekuwa ndani ningeofia lakini nje! Ni sawa ni kelele za vyura hazimzui tembo kunywa maji!
 
hahaahha hahaha hahaha
Mrema anapaswa kujiunga na ZE ORIJINO KOMEDY tuwe tunapata burdani kila wiki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom