Elections 2010 Mrema aapa kuivuruga Chadema

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,268
17,097
BAADA ya kulia na propaganda chafu za Chadema, mgombea ubunge katika Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP, Augustino Mrema, amesema anapanga kujibu mapigo kwa kuhamishia nguvu zake katika majimbo matatu ambako Chadema wana matumaini ya ushindi.

Amesisitiza kwamba, haendi kwa bahati mbaya, bali kuwavurugia kama chama hicho kinavyomtibulia mipango yake ya kuingia bungeni, baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31.

Mrema alisema hayo jana kwenye Viwanja vya Majengo Sokoni, mjini hapa, wakati akimnadi mgombea ubunge wa TLP Moshi Mjini, Godfrey Malisa.

Alisema kutokana na kufanyiwa siasa chafu na Chadema, sasa chama chake kitahakikisha kinaelekeza nguvu Hai (Freeman Mbowe), Moshi Mjini (Philemon Ndesamburo) na Vunjo (John Mrema).

Mrema alisema madhumuni ya kuelekeza nguvu katika majimbo hayo, ni kutokana na alichokiita upinzani wa kinafiki unaofanywa na Chadema, ambapo alisema kauli ya Chadema kuwa Mrema atakwenda kufia bungeni, ni matusi huku akisisitiza kwamba hakuna mtu asiyekufa na kutaka aachwe akafie huko.

Aliwaonya mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, Mwenyekiti Mbowe na Ndesamburo kutokanyaga jimbo la Vunjo.

Alisema wakikaidi, waende kistaarabu, lakini wakiendelea kumchezea rafu za kisiasa, atahakikisha kati yao hakuna anayeshinda katika uchaguzi mkuu, kwani atafanya kampeni za nguvu kuhakikisha anagawa kura za Hai na Moshi Mjini.

“Kama wao wanadai kuwa mimi ni mzee eti niwaachie vijana, sasa mimi niulize kati ya Kikwete na Dk. Slaa, nani mzee?... inatakiwa Slaa amwachie Kikwete uongozi, kama Slaa anataka kwenda Ikulu atafia huko nami nifie bungeni, mbona kuna wabunge wanafia humo?

“Kama Chadema inavyogawa kura zangu Vunjo, vivyohivyo nami nitahakikisha Mbowe, Mrema na Ndesamburo, hawanusi Bunge … nitafanya kampeni kubwa katika majimbo yao, kuhakikisha TLP inakuwa na wapiga kura wengi, ili kuzuia ushindi wanaotarajia Chadema, nitahakikisha hadi kinaeleweka,” alisema Mrema.

Alisema anashangazwa na upinzani uliopo sasa miongoni mwa vyama vya upinzani, kwani havijalenga kuchukua madaraka ya nchi, bali kushambuliana, jambo linalozidi kuvidhoofisha na kuiacha CCM ikitamba.

Malisa, alisema kwa miaka 10 sasa Chadema imeongoza jimbo hilo, lakini hakuna mabadiliko yoyote yaliyopatikana zaidi ya wananchi kubaki mashabiki wa chama hicho.

Alisema tatizo la wananchi wa Moshi ni kudanganywa na gari la kubebea wagojwa la Hospitali ya Mkoa, Mawenzi, ambalo lilitolewa na Ndesamburo, ambalo kwa sasa alidai ni bovu na halijafanyiwa matengenezo.

Pia aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua, akisema akipewa ridhaa atahakikisha viwanda vilivyoshindikana kufufuliwa na Chadema vinafufuliwa, ili kutoa ajira kwa wakazi wa Moshi.

Source: Habari Leo
 
Heshima kwako safari_ni_Safari,

Mkuu wangu wapinzani kwa ujinga wao wataendelea kuparurani na kuiacha CCM ishinde.
 
"Kama wao wanadai kuwa mimi ni mzee eti niwaachie vijana, sasa mimi niulize kati ya Kikwete na Dk. Slaa, nani mzee?... inatakiwa Slaa amwachie Kikwete uongozi, kama Slaa anataka kwenda Ikulu atafia huko nami nifie bungeni, mbona kuna wabunge wanafia humo?
Kheeee heeee heeee!... Kampeni katika mkondo mpya sasa!
 
Nani kasema A. L.Mrema ni mpizani? Huyu ni vuvuzela la mgonjwa mwenzake JK. WAFU WANAKOKOTANA
 
Heshima kwako safari_ni_Safari,

Mkuu wangu wapinzani kwa ujinga wao wataendelea kuparurani na kuiacha CCM ishinde.

Kwani Mrema ni mpinzani??? Huyu ndiye alikwenda mpaka kwenye mkutano wa CCM kumpigia debe JK kuwaomba wamwachie jimbo la Vunjo. Nashangaa analilia nini sasa. Au ndiyo maji yameshazidi unga huko na kihsa jua kuwa mjengoni harudi tena.....!!!
 
Heshima kwako safari_ni_Safari,

Mkuu wangu wapinzani kwa ujinga wao wataendelea kuparurani na kuiacha CCM ishinde.

Mrema kwani nae ni mpinzani ?
mrema anaumwa, CHADEMA walilisema hili tangu mwanzo, huyu hayuko TIMAMU kiakili, anawayawaya, anatafuta wakufa nae kisiasa.
CHADEMA ilimkataa Mrema akiwa Hot MWAKA 1995 baada ya kutoka ccm, walimwambia akitaka kujiunga na chama hiki awe mwanachama wa kawaida.
CHADEMA haijengi kwenye mchanga, kisa kufanya mashirikiano hewa na wanasiasa uchwara wa aina ya Mrema, inajengwa juu ya mwamba ulio Imara, ikiwa haitegemei umaarufu wa mtu mmoja, ama uwepo wa mtu fulani chamani.
Mrema alishindwa kuisambaratisha CHADEMA akiwa maarufu, akiwa na akili Timamu, na nguvu za kufikiri atawezaje leo iwapo uwezo wake wakuyaona mambo hauna tofauti na mtoto wa miaka 4.
 
Ha ha haaaa!! Siasa za Lyatonga zinanikumbusa zamani nikiwa mtoto nisipokuta chakula nyumbani nilikuwa naitandika kabati mateke kana kwamba ndio imekataa kupika. Chakula enzi hizo kilikuwa kinahifadhiwa kwenye kabati. Ha haaaa uhu! Mrema bana. Pambana huko kwako vunjo acha kulia lia, hakuna wa kukusaidia kwenye hayo madai ya kitoto.
 
Mrema ananjaa anatafuta ulaji kwa kila namna kachoka kiafya, kiakili, kifikra hadi kiuchumi. Mfamaji haishi kutapatapa...tumuache tu aweweseke.
 
Mrema.gif


Na yeye ana PhD (Permanent head Damage)
 
Pole augustino, usomi alama za nyakatiiiiiii??? Too late its all over,
 
muangalia upande mmoja tu, jee waliomfanyia chadema ni sawa?

au wao kufanya siasa maji taka ni sawa?
 
''Aisee mangi nichangie mafta babaangu....si una sile sa Rich...''

mrema1bc.jpg

Mrema suti na Raba mtoni wapi na wapi??? baaangu. Inabidi wajanja wafuatilie Muhimbili psychiatric department huenda mzee mzima analo file la kale kagonjwa na dose anapata kama kawa.Chunguza Utabaini mjomba
 
Back
Top Bottom