Mrejesho wa kuvunjwa kwa mkataba wa soko la Kilombero

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Ndugu
mtakumbuka kuwa niliahidi kuwajulisha kuhusu sakata hili la mkataba kuvunjwa
Ni kweli kuwa mkataba wa soko kukusanya ushuru na kufanya usafi kwenye soko la kilombero,ulivunjwa rasmi,baada ya jitihada kubwa,kimsingi huyu wakala alishindwa kufanya usafi,na soko kuwa chafu sana,lakini pia alishindwa kuwasilisha malipo,kwa halmashauri.Mimi kama mtetezi wa wananch nikashinikiza mkataba kuvunjwa kwa kuwa haukuwa na maslahi kwa wananch..Sasa halmashauri inakusanya mapato na hali ya usafi ni nzuri
nawasilisha
 
ahsante mh. ila nna swali ila naomba nikuulize tu japo inaweza ikawa ni offtopic hivi kuna mchakato wowote wa kukarabati na kujenga hizi barabara za makao mapya, levolosi na zote zinazolink kata ya ngarenaro na mjini? Lingine hapa karibu na seuri bar kuna ghorofa linajengwa watu wanasema ni soko je ni kweli? Ka ni kweli hebu mheshimiwa fuatilia hata likamilike ili litoe ajira zaidi kwa vijana hasa apolo wengi wako town mererani ni magongaa tu hamna ramani ahsante
 
Halmashauri inakusanya yenyewe mapato,na usafi pia ni halmashauri yenyewe,soko limekuwa safi sana
Barabara tutazitengeneza,kuanzia Ngiwaranecha ipite selian hadi kaloleni,na mchakato unaendelea.Ni ghorofa gani kamanda?
 
Kama Halmashauri ilikuwa na uwezo wa kukusanya mapato ni sababu zipi zilisababisha watoe tenda?

Na je suala la halmashauri kutoa leseni kwa wenye maghala kinyume na utaratibu umelifuatilia mheshimiwa? Pia, kuna malalamiko kwamba malori yanalipa sh elfu tano badala ya kulipa kwa rate iliyopitishwa, inakuwaje? Hili lilipitishwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa na Mwanasheria wa Halmashauri.

Nina maswali kuhusu utaratibu wa kuvunja mkataba huo, taarifa ya tume iliyoundwa na malalamiko ya aliyekuwa wakala kupuuzwa au kutofanyiwa kazi.

Naamini kwamba kwa sababu Halmashauri imefungua kesi ya madai mahakama kuu basi haitajikuta inalipa fidia kwa kukiuka uvunjaji wa mkataba bila kufuata utaratibu na pia kwa kutoa sababu ambazo ni za kisiasa zaidi badala ya kibiashara na kisheria.

Nitoe angalizo Mheshimiwa, endapo mahakama itatoa hukumu kwamba taratibu hazikufuatwa au kulikuwa na matatizo ya kisheria basi itakuweka between the rock and ground.

It is fair and just to allow the law to take its course, ni mapema mno kwa sasa kupiga makofi.
 
Kamanda ni stori ndefu,naomba nikutafute kesho ili nikupe picha halisi
shinikizo la mkataba wa kilombero limefanya mikatba mingine ya kinyonyaji kuvunjwa,ikiwa ni pamoja na ya kukusanya ushuru wa mabango,huu wa kilombero sababu ziko wazi kabisa na ni za kibiashara na kisheria
Hilo la malori nalifuatilia,bado sijapta data za kutosha
 
Sawa Mheshimiwa. Tutazungumza. Kesho nitarudi Moshi kwenye kata. Nina mikutano ya vocha za pembejeo. Ni vurugu tupu. Wananchi hawajaelimishwa, wizi na ulaghai wa mawakala, ujambazi wa watendaji nk. Heri yako wewe unayepambana na mikataba ya mjini...hahaa! Just a joke.
 
Pole kamanda,changamoto ni nyingi,na nchi imejaa changamoto kuanzia vijijini hadi mijini,hali ni mbaya na watu wamekataa tamaa we must fight for our people and nation
 
Back
Top Bottom