Mrejesho kwa Mlachake

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Wana bodi habari,

Mkuu Mlachake alianzisha uzi siku chache huko nyuma na kuwataja baadhi yetu kuwa tuunganishe nguvu ili tutoke na kitu. Wazo lako halikuokotwa na kunguru bali tulilichukua na kulifanyia kazi vizuri. Limeleta mwangwi chanya kwa wote walioitikia.

Baadhi ya Wana-Jf tulijikusanya na kufanikiwa kuanzisha kikundi ili tupate kuanzisha mradi wa ufugaji. Asante sana Mlachake kwa kuwataka wale uliowataja wafanye kitu.Tumefanya. Kwa sasa tuna shamba na tunalipanua zaidi, na tayari mifugo ya kwanza imeshafika shambani.

Changamoto zipo na lazima tuzikabili kiume kabisa, naamini kupitia vikundi tunaweza kufaidi fursa za nchi yetu, na mimi nawashauri wenzangu wenye mitaji midogo waunganishe nguvu ili hatimaye wawe na kitu cha kufanya.

Siku moja tutakualika Mkuu Mlachake ili uje uone matokeo ya wazo lako.
 
That's good Malila
Msisahau kuwa mnamwaga uzoefu humu Jamvini pia kwa manufaa ya Jamii
 
Mnafuga nini huko shambani?

Na vipi kuhusu changamoto?

Mkuu tumeanza na mbuzi, lengo la kwanza ni kuwa na terminal ya mbuzi kubwa toka mikoani, na hatimaye tuwe na shamba la mifugo kubwa huko mbele.

Changamoto kubwa ya kwanza ilikuwa kuaminiana kwa wadau waliojitokeza mwanzoni kabisa,wengi walisema tuko pamoja.Ilipofikia hatua ya kukutana live, idadi ilishuka sana. Ilipofikia hatua ya kutoa michango ili tuanze, idadi ilikata kama nusu nzima. Idadi iliteremka mpaka tukawa 14 tu.

Kilichonifurahisha ni imani walioionyesha wadau walio nje ya nchi ambao mpaka leo hatuja wahi kuonana uso kwa uso, wako active sana ktk michango. Changamoto ya pili ni ugumu wa kufanya vikao, mahudhurio sio mazuri.Kulikabili hili, tunaendesha kila kitu online.

Changamoto ya tatu ilikuwa ni manpower, ilibidi tuibe kijana mzuri kwa mwekezaji mwenzetu kwa kuboresha huduma kwa huyu kijana. Ilibidi kujenga nyumba ya tofali, msosi wa maana, mawasiliano,malazi mazuri, mahali pa kujisetiri pazuri ili awe na amani ya moyo.

Changamoto ya nne ambayo ipo kila kwa mjasiriamali ni speed ndogo ya michango, namshukuru Mungu tumekwenda sawa na kalenda tuliyopanga. Hiyo ni phase I, bado hatujaingia phase II.
 
Malila,

Nashukuru sana kwa kunijuza haya.

Ni bahati nzuri kwamba mimi mwenyewe nipo mbioni kuanzisha ufugaji wa mbuzi.

Nikamalilisha utaratibu wa kupata eneo la kama hekari 30 mkoa wa pwani.

Swali je mbuzi huwa wana maeneo na maeneo nikimaanisha kuna baadhi ya sehemu hawastawi? Je kuna majani maalum nitahitaji kupanda ? je kuna chakula maalum apart from majani ambacho itabidi niwape?

Na je hili eneo nikishalichukua nilifyeke nyasi zoote au niliache kama pori lilivyo ili wapate chakula?
 
Vp ufugaji wa Ngomb'e maeneo ya Pwani kama Mkurunga? kuna breed inayoweza kutoa hadi lita 20 kwa siku maeneo hayo? Najua breed nzuri hukubali maeneo ya baridi
 
Hivi Ng'ombe maziwa anayotoa si inakuwa proportional na msosi anaokula na virutubisho?
 
Inategemea na aina ya ng'ombe mkuu chukua hawa ngo'mbe wetu wa kienyeji wenye nundu uwalisha kila aina ya chakula bora unachojua uone kama watatoa hata lita 10 kwa siku,aina ya ng'ombe na matunzo ndo vinadetermine wingi wa maziwa ila breed nyingi zinazotoa maziwa mengi zinakubali sehemu za baridi
 
Wana bodi habari,

Mkuu Mlachake alianzisha uzi siku chache huko nyuma na kuwataja baadhi yetu kuwa tuunganishe nguvu ili tutoke na kitu. Wazo lako halikuokotwa na kunguru bali tulilichukua na kulifanyia kazi vizuri. Limeleta mwangwi chanya kwa wote walioitikia.

Baadhi ya Wana-Jf tulijikusanya na kufanikiwa kuanzisha kikundi ili tupate kuanzisha mradi wa ufugaji. Asante sana Mlachake kwa kuwataka wale uliowataja wafanye kitu.Tumefanya. Kwa sasa tuna shamba na tunalipanua zaidi, na tayari mifugo ya kwanza imeshafika shambani.

Changamoto zipo na lazima tuzikabili kiume kabisa, naamini kupitia vikundi tunaweza kufaidi fursa za nchi yetu, na mimi nawashauri wenzangu wenye mitaji midogo waunganishe nguvu ili hatimaye wawe na kitu cha kufanya.

Siku moja tutakualika Mkuu Mlachake ili uje uone matokeo ya wazo lako.

kaka hongereni sana.

Kuna vichwa ambavyo huwa sina wasi wasi navyo humu ndani.
 
Malila,

Nashukuru sana kwa kunijuza haya.

Ni bahati nzuri kwamba mimi mwenyewe nipo mbioni kuanzisha ufugaji wa mbuzi.

Nikamalilisha utaratibu wa kupata eneo la kama hekari 30 mkoa wa pwani.

Swali je mbuzi huwa wana maeneo na maeneo nikimaanisha kuna baadhi ya sehemu hawastawi? Je kuna majani maalum nitahitaji kupanda ? je kuna chakula maalum apart from majani ambacho itabidi niwape?

Na je hili eneo nikishalichukua nilifyeke nyasi zoote au niliache kama pori lilivyo ili wapate chakula?

Kama ukifuga kienyeji unaweza usipande majani maalumu kwa chakula chao, lakini ukitaka kufuga kisasa na kwa malengo maalumu ya biashara ni lazima upate mbegu nzuri za majani. mbuzi wanakula aina nyingi za majani miti, hivyo eneo lenye vichaka linafaa sana kwa mbuzi,na ndo maana unaona sehemu kame mbuzi wanaishi.

Mkuranga kuna chatu wale wadogo, ni vizuri kuchoma hilo eneo ili kuwafukuza kama wapo, mimi walinyonga mbuzi 11 hivi wakati naanza. Na kama utafuga huria, inabidi uwe makini, mbuzi wanazurura sana kwa hiyo eka 30 kwa mbuzi huria inabidi usiwe na jirani mkorofi. Vijito vyenye maji ya kudumu kule Mkuranga vina mamba na chatu hukaa kando ya vijito hivyo.

bado vibaka sio wengi inategemea uko Mkuranga ipi. Mhimu, mtafute LAT akupe majina ya mbegu bora za majani ili uoteshe ktk shamba hilo.
 
Malila,

Umenistua kuniambia kuwa kuna chatu na mamba hapo Mkuranga.

Bahati nzuri sipo Mkuranga mzee.

Ngoja niulize huo mpango wa majani.

Hivi Chatu anaweza kula mbuzi? Kuna mamba Mkuranga? halafu niulize mbuzi anachukua muda gani kukuwa hadi tayari kwenda sokoni? na je anazaa kila baada ya muda gani? Na unaweza kupata breed inayozaa mapacha tu?
 
Mkuu tumeanza na mbuzi, lengo la kwanza ni kuwa na terminal ya mbuzi kubwa toka mikoani, na hatimaye tuwe na shamba la mifugo kubwa huko mbele.

Changamoto kubwa ya kwanza ilikuwa kuaminiana kwa wadau waliojitokeza mwanzoni kabisa,wengi walisema tuko pamoja.Ilipofikia hatua ya kukutana live, idadi ilishuka sana. Ilipofikia hatua ya kutoa michango ili tuanze, idadi ilikata kama nusu nzima. Idadi iliteremka mpaka tukawa 14 tu.

Kilichonifurahisha ni imani walioionyesha wadau walio nje ya nchi ambao mpaka leo hatuja wahi kuonana uso kwa uso, wako active sana ktk michango. Changamoto ya pili ni ugumu wa kufanya vikao, mahudhurio sio mazuri.Kulikabili hili, tunaendesha kila kitu online.

Changamoto ya tatu ilikuwa ni manpower, ilibidi tuibe kijana mzuri kwa mwekezaji mwenzetu kwa kuboresha huduma kwa huyu kijana. Ilibidi kujenga nyumba ya tofali, msosi wa maana, mawasiliano,malazi mazuri, mahali pa kujisetiri pazuri ili awe na amani ya moyo.

Changamoto ya nne ambayo ipo kila kwa mjasiriamali ni speed ndogo ya michango, namshukuru Mungu tumekwenda sawa na kalenda tuliyopanga. Hiyo ni phase I, bado hatujaingia phase II.
Shamba liko wapi mjasiriliamali? na nikitaka kununua hisa kwenye huo mradi nifuate njia ipi, na garama ya hisa au mchango ni kiasi gani?
 
lipo Mkuranga,
sina jibu kwa sasa juu ya kujiunga.Labda tukionana na wadau naweza kupeleka kama agenda ya kikao. Uzuri ni kwamba wengine wanakusoma hapa jamvini.
 
Malila,

Umenistua kuniambia kuwa kuna chatu na mamba hapo Mkuranga.

Bahati nzuri sipo Mkuranga mzee.

Ngoja niulize huo mpango wa majani.

Hivi Chatu anaweza kula mbuzi? Kuna mamba Mkuranga? halafu niulize mbuzi anachukua muda gani kukuwa hadi tayari kwenda sokoni? na je anazaa kila baada ya muda gani? Na unaweza kupata breed inayozaa mapacha tu?

Ktk mkoa wa Pwani/Tanga/Morogoro ukiona kuna maji mengi kwa mwaka mzima, ogopa sana( hata hapo Mpigi magohe karibu na Mabwe pande- yaani bonde la Mpigi linaloanzia Kiluvya,lina mamba), mto Ruvu/Wami wapo kibao. Hizi ni changa moto ndogo za ufugaji.

Chatu wanakula wanyama size ya mbuzi na kushuka chini.Market size ya mbuzi inategemea mambo mengi, chakula,breed na mahali ulipo. Ila baada ya mwaka mmoja mbuzi huwa ameshakuwa mzuri kwa biashara. Watalaam watasaidia hapa kulingana na breed. Kwa mwaka anazaa mara mbili. Unaweza kupata breed ya pacha mpaka watoto wanne kwa mzao mmoja.

Kuna sehemu fulani kigoma, mbuzi akizaa pacha huyo ndio kazaa kidogo. Dr mmoja ameniahidi kunipa breed hiyo, tuombe Mungu. Ukiweza kuwapata wale mbuzi waliosambazwa na SUA itakuwa safi sana, ni wakubwa sana.
 
Malila,

KUna mdau mmoja alitujuza juzi hapa hapa ndani kwamba wale mbuzi wa kisasa wana matatizo mengi ikiwemo pamoja na kushambuliwa na magonjwa na kuvunjika miguu. Sasa nyie mnaofiupa ni wepi hasa?
 
Mimi bado napenda vya asili na chotara kidogo,
Nilikusanya mbegu ya mbuzi toka visiwani hasa Pombwe, huko kuna mbuzi wenye breed ya pacha, kisha baadae nikachukua cross breed ya madume, napata chotara yenye size nzuri kiasi. Baadae niliwapata hawa wa maziwa majike watatu, maziwa wanatoa vizuri, ila wanaugua ugua sana, na miguu ndio tatizo kubwa. Lakini 60% ni kienyeji pure. Naamini ukichanganya breed unaweza kutoka na size kubwa.

Pombwe kuna size ya kienyeji kubwa.
 
Kama ukifuga kienyeji unaweza usipande majani maalumu kwa chakula chao, lakini ukitaka kufuga kisasa na kwa malengo maalumu ya biashara ni lazima upate mbegu nzuri za majani. mbuzi wanakula aina nyingi za majani miti, hivyo eneo lenye vichaka linafaa sana kwa mbuzi,na ndo maana unaona sehemu kame mbuzi wanaishi.

Mkuranga kuna chatu wale wadogo, ni vizuri kuchoma hilo eneo ili kuwafukuza kama wapo, mimi walinyonga mbuzi 11 hivi wakati naanza. Na kama utafuga huria, inabidi uwe makini, mbuzi wanazurura sana kwa hiyo eka 30 kwa mbuzi huria inabidi usiwe na jirani mkorofi. Vijito vyenye maji ya kudumu kule Mkuranga vina mamba na chatu hukaa kando ya vijito hivyo.

bado vibaka sio wengi inategemea uko Mkuranga ipi. Mhimu, mtafute LAT akupe majina ya mbegu bora za majani ili uoteshe ktk shamba hilo.

Ahhh Malila steam yote kwisha, sasa inakuwaje kumbe mito sio mizuri kabisa
 
Ila hongereni sana kwa kuweza kugeuza wazo kuwa kweli, hii ni changamoto kwa sie kina Tomaso
 
Ahhh Malila steam yote kwisha, sasa inakuwaje kumbe mito sio mizuri kabisa

Hizo ndio changamoto za kilimo huku Pwani, kama kuna maji na wanyama nao ndio wanataka hapo hapo. Sio kwamba wanakaa saa zote,muulize mtu ye yote mwenye shamba mto Mpiji karibu na bunju au Ruvu, atakwambia habari ya mamba.
 
ni kweli hiyo ni fact ila kama hawakai saa zote sio neno maana hiyo inaweza kukufanya ukakosa manpower kabisa kw ahofu familia zao kuliwa na mamba, ila nimeenda sana Rufiji pia mamba walikuwa wanakuja hadi huku utete mjini kipindi hicho watu wakizidi kujaa basi wanahamia maeneo mengine.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom