mh. John Mnyika, hongera sana.
napenda kukiri kuwa wewe ni mmoja wa wanachadema walio hazina kubwa sana kwa chadema yenyewe na Tanzania kwa ujumla. nafurahishwa sana na umakini wa hoja zako na ujasiri wa hali ya juu unaoambatana na busara ambayo kwa kweli sikuitegemea kutoka kwa kijana wa umri wako na uzoefu wako wa masuala ya bunge. kwa kweli unawashinda kwa mabli wabunge chungu mzima baadhi yao wakiwemo waliokaa bungeni kwa miongo kadhaa. hongera sana mheshimiwa.
pia nimeguswa na aina hii ya uwajibikaji kwa wapiga kura na washabiki wako. yaani hapa umeweka changamoto kwetu sote juu ya kiwango cha uwazi na hulka anayopaswa kuwa nayo mbunge atokanaye na jimbo la uchaguzi kwa wapiga kura wake. ni dhahiri kabisa sasa kuwa wapiga kura wa jimbo la ubungo hawakukosea kukuchagua kwa kura nyingi kuwa mbunge wao. walau sasa wana mwakilishi aliye sauti yao bungeni na mtoto wao arudiye kutoa taarifa kwa kazi aliyotumwa.
mwisho nakuahidi kuwa, kama mmoja wa wabunge wapya wa CCM lakini mwenye ari kuuna uthubutu wa mabadiliko, nitajitahidi tufahamiane kibinafsi ili tuweze kubadilishana mawazo na mikakakti kwa karibu zaidi kwa manufaa ya wananchi wa majimbo yetu tunayowakilisha. mimi japo natokana na CCM ila kwangu taifa ndilo la kwanza kabisa na mamabo mengine yanafuata. wakati mwingine ushabiki husaidia kutawala siasa lakini si mara zote huwa na tija kwa taifa. mfano sasa ni dhahiri kuwa tunapata tabu sana kwa sasa kueleweka na wanachi pale tunapoonyesha mshikamano wa kichama kwa mambo mbalimbali kuliko wakati mwingine wowote. hiii inatokana na ukweli kuwa siasa zetu zimebadilika na wanachi wetu nao wamebadilika. kwa msingi huu ni lazima kujinasua na mtego wa u-chama katika masuala yenye manufaa kwa taifa ili angalau wanachi waendelee kutuamini.
tuko pamoja mkuu. nakutakia kila la heri
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Mheshimiwa Mbunge, Ahsante sana kwa kutoa maoni yako kuhusiana na hili suala la Udini. Bila shaka kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa historia na siasa za Tanzania kumekuwepo na shutuma na minong'ono mingi sana kuhusiana na udini nchini Tanzania, shutuma hizi wala hazikuanza kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita tu, bali zimekuwepo kwa muda mrefu sana.Lipo kundi kubwa sana la wananchi Wanaodhani kwamba kuna mfumo unaowabagua katika nyanja mbalimbali tokea uhuru mpaka sasa, Mimi binafsi sina Ushahidi wa Malalamiko yao, lakini UKWELI NI KWAMBA WAO WANAFIKIRI HIVYO NA WANAAMINI HIVYO. na hali hii ni hatari kwa usalama na Amani ya nchi yetu.Sasa Mheshimiwa Mbunge kufuatia malalamiko hayo ya hao ya sehemu ya wananchi wetu, Unampango gani kuhakikisha Ukweli unawekwa bayana ili kama kweli kuna Ubaguzi FORMAL au INFORMAL basi unaondoshwa na wenye kuhusika nao wanafikishwa katika vyombo vya sheria, lau kama Huo ubaguzi haupo basi Ukweli uwekwe wazi na watu waelimishwe?. kwa maoni yangu DENIAL IS NOT AN OPTION, BALI TRUTH PEKEE NDO ITAONDOA MZIZI HUU WA UDINI NCHINI. AHSANTENawashukuru sana kwa ushauri na hata Pili, suala la 'udini'- ni kwa bahati mbaya sikuwa na muda wa kutosha kueleza zaidi lakini mimi kwa maoni yangu, wapo viongozi wanaotumia kivuli cha udini kuficha udhaifu wao wa kiuongozi na kufunika mijadala ya msingi ya kitaifa. Kadiri tunavyoachia viongozi wa namna hii wakafanya hivyo wafanyavyo tunaweza tukajikuta tunaruhusu mbegu ya udini ikapandwa zaidi. Nilisema vyombo vya usalama vishauri viongozi wetu, sio kwa sababu tu ya hotuba ya Rais bungeni, bali kuna kauli nyingi za kabla, wakati na baada ya kampeni zinazodhihirisha haja hiyo. Naamini kwamba masuala haya yangeweza kushughulikiwa kwa kadiri yalivyoanza kujitokeza kwa hatua za kiusalama na kiuongozi badala ya kupigiwa baragumu.
Barua ndefu. Tukifanya impact evaluation hapa, hakuna kitu. Chifu, try to accomplish things. And not reiteriating what we have already seen kwenye vikao vya bunge. Come up with ideas and have balls to work with "mafisadi" if you think the cause is worthy it.
And be independent for a minute. Wadau mtaani wanadai whatever Mbowe/Slaa says--John Mnyika doesn't even question it, anatekeleza tu.
Barua ndefu. Tukifanya impact evaluation hapa, hakuna kitu. Chifu, try to accomplish things. And not reiteriating what we have already seen kwenye vikao vya bunge. Come up with ideas and have balls to work with "mafisadi" if you think the cause is worthy it.
And be independent for a minute. Wadau mtaani wanadai whatever Mbowe/Slaa says--John Mnyika doesn't even question it, anatekeleza tu.