Mramba, Mrisho, Mgonja, et al.. chunguni?

Haya kaka Mgonja karibu Sero bwana mudogo!! Hivi murifiliria kuwa hamutakamatwa eh?? Hebu afande Chare riweke kure ndani hiri riarifu jingine......... Uache na nafasi kwani kuna menzake mengine mengi yanakuja hasa rire rinene renye kitambi kama afande Arufonsi.
 
Halafu mke wa Mgonja anaishi California toka kitambo sasa.

Ni kweli mkuu, Lilian Mgonja anaishi California, alikuwa nurse, sasa hivi anaishi kwenye jumba la kifahari sana na kuendesha magari ya kifahari sana hafanyi kazi tena. Kila mwezi huwa anakuja Tanzania. Watoto wao wanasoma shule za private. Lilian alikuwa anafanya biashara za nguo na saloon kabla mzee hajaanza ufisadi na kuhamia US. Kweli mama hajatulia kabisa anajirusha na wa Kenya na jamaa zetu wa West Afrika Magharibi....sasa hivi mama amapata pressure maana mzee alikuwa anasubiriwa US kwa Xmas....hii kitu hawakuwa wakijua kabisa ndani ya familia.

Ushi
 
Kuzomea, kuibua kashfa za serikali, kupinga na kukosoa ni kazi muhimu sana ya chama cha upinzani, lakini hii peke yake haikufanyi wananchi wakuchague. Ili uchaguliwe lazima uonyesha kwamba wewe ni alternative government kwa kuwa na timu imara na sera mbadala utakazotekeleza mara ukabidhiapo madaraka. Kwa hiyo, kwa maoni yangu, hiki kilichokwishafanywa so far na opposition, hasa CHADEMA, is sufficient enough to make us a credible opposition, but not good enough to convince the masses that we are a better government in waiting. Ili tuwe a credible government in waiting lazima tuchukue the next step, ambayo ni kuwaonyesha wananchi kwamba sisi tuna mawazo,sera, mikakati na timu mbadala murua na bora zaidi zitakazotatuta, pamoja na matatizo mengine, tatizo la ufisadi kama wakitupa tuendeshe serikali yao. Kuna haja kubwa sana sasa kujikita katika kuelezea sera na mikakati yao juu ya matatizo mbalimbali ya nchi yetu.
QUOTE]

Kaka Kitila nakubaliana nawe 100%. Huu ndio mtazamo wangu kwa muda mrefu sasa. Kazi kwako kushurutisha hili ndani ya chama...

Tanzanianjema
 
Mzee ES naomba kama una inside kuhusu kesi ya Mama Meghji, maana ninavyosikia mimi ni kuwa hakuna suala lolote kuhusu Mama Meghji alilofanya ambalo ni la kifisadi. Issue yake ilikuwa tu kuwapa auditors info kuhusu TISS kuhusika na pesa za Kagoda kwa mambo ya kiusalama ambalo alilirekebisha within days.

Adhabu aliyopata ni kutoswa kutoka kwenye cabinet.
 
Unamshukuru polisi kwa kufukuza mwizi ?

Unamshukuru Mkuu wa Tume ya kupambana na rushwa kwa kupambana na rushwa ?

Unamshukuru Mwanasheria Mkuu kwa kufuata sheria ?

Mimi ni kuli. Kwa kila mzigo ninaopakia na kupakua kwenye malori ya kampuni bosi anadunduliza hela sehemu kila mwisho wa siku. Zikifika wiki mbili karani wa kampuni ananipa hundi. Sijawahi kuambiwa ahsante. Tena mwenye mizigo hii, mmiliki wa kampuni, sijawahi hata kuteta nae.

Nikadai shukurani ?

ilikuwa wafanye tangia zamani hawakuweza. wakiweza leo na tuwape heko. kuwashughulikia watu wanene kama wale kwa uhakika yahitaji moyo. labda kama tunadanganywa
 
Haya kaka Mgonja karibu Sero bwana mudogo!! Hivi murifiliria kuwa hamutakamatwa eh?? Hebu afande Chare riweke kure ndani hiri riarifu jingine......... Uache na nafasi kwani kuna menzake mengine mengi yanakuja hasa rire rinene renye kitambi kama afande Arufonsi.

ritaenda sero. ritapata ridhamana. kesi itaenderea miez/miaka kadhaa. ritaachiwa huru kwa vile harikutoa maamuz peke yake/renyewe ririkuwa rinashauri tu.
muda na pesa zetu zitakuwa zimetumika. and then?
 
Haya kaka Mgonja karibu Sero bwana mudogo!! Hivi murifiliria kuwa hamutakamatwa eh?? Hebu afande Chare riweke kure ndani hiri riarifu jingine......... Uache na nafasi kwani kuna menzake mengine mengi yanakuja hasa rire rinene renye kitambi kama afande Arufonsi.

ritaenda sero. ritapata ridhamana. kesi itaenderea miez/miaka kadhaa. ritaachiwa huru kwa vile harikutoa maamuz peke yake/renyewe ririkuwa rinashauri tu/ushauri wa kutosha utakosekana.
muda na pesa zetu zitakuwa zimetumika. and then?
 
Hilo la preferential treatment,watu wa magereza nafikiri walishalitolea ufafanuzi.walisema hata zombe hawajamuweka na watuhumiwa wengine kwasababu wapo wanatuhumiwa wenye hasira naye wanaweza kumdhulu.Zombe yuko pamoja na Jeetu na Johnson Lukaza selo moja.

ni kweli. walishalitolea maelezo kama unavyosema.
lakini wakudhuriwa ni wao tu?
wakukaa sehemu nzuri huko sero kwanini wawe wao tu?
sehemu zote ziwe sawa. hakuna apendae kukaa sehemu chafuchafu. kama ni ukarabati ufanyike magereza yote.

anayetia hasara ya mil 2 anaenda kwa ovyo. wa bil 11 anaenda sehemunkuzuri.

du.

kuiba kidogo noma?
 
Mzee ES naomba kama una inside kuhusu kesi ya Mama Meghji, maana ninavyosikia mimi ni kuwa hakuna suala lolote kuhusu Mama Meghji alilofanya ambalo ni la kifisadi. Issue yake ilikuwa tu kuwapa auditors info kuhusu TISS kuhusika na pesa za Kagoda kwa mambo ya kiusalama ambalo alilirekebisha within days. Adhabu aliyopata ni kutoswa kutoka kwenye cabinet.

- Mkulu wangu, the inside nilizonazo ni kwamba mawaziri wote waliotemwa kwa kuwa na harufu ya ufisadi, wako njiani kwenda Kisutu, infact hata Warioba yumo njiani kwenye Mwananchi Gold, na hii operation inaenda mpaka 2010 by then wote watakuwa wameshafikishwa kwa Pilato.

- Mramba ana kesi nyingi sana, kiasi kwamba ni kupoteza muda kwake kujipanga na mawakili, nusu ya kesi za Mramba zinamvuta Mama Meghji, aliyekua aki-act under orders za RA, ndiyo sababu ya RA kutolewa kiungwana na Muungwana kule Hazina ya CCM.
 
Mkuu Field Marshall ES,

Je ushahidi wa kutosha (Complete and Exhaustive) umeshapangwa na hawa waendesha mashitaka? Manake mambo ya viini macho au stori za kuwa watu wemeshindwa kesi au wanapewa vifungo vya kijinga kijinga wakati tamaa na uhujumu wao umesababisha maafa kwa wadanganyika chungu nzima miaka nenda rudi hatuzitaki.
 
- Mkuu Pilato mmoja ameniambia hivi, hizi kesi ni ngumu sana kuzifanikisha kutokana na njaa za Majaji na mahakimu, hilo ma-Pilatos wanalijua sana, ndio hasa lililopelekea kumshauri rais awape muda wa kurudisha pesa wale watu wa EPA, maana iliogopwa kwamba iwapo watakusanywa wote kwa pamoja, watashinda kirahisi sana kwa kutumia rushwa,

- Siko hapa kuahidi kufungwa kwa viongozi, na hata Pilato aliniambia kua hawezi kuahidi hilo, lakini aliahidi kuwa sheria itachukua mkondo wake to the fullest na hakuna wa kupona, kabla ya kuanza hii Op, wakulu walipelekwa Zambia kula darasa kidogo, ingawa wanasema kwamba kule Zambia safari ya kamata kamata ilisimama kwa mstaafu wa Idara wa huko, bwana Chungu, kwa sababu kumbe Mwanawasa aliibiwa uchaguzi na huyu mkulu, sasa swali ni kama na bongo itafika kwa mstaafu wa idara.

Otherwise, wakati Pilato ananipa hili darasa nilikuwa ninamuangalia sana usoni na kuyapima kwa makini sana maneno aliyokua akiyatumia, wallahi wote wanaenda na hakuna wa kupona, at one point Pilato alinipa mfano wa mtoto wa Mramba anayeitwa Godfrey, aliyejairbu kuiomba serikali imuachie baba yake kwa muda tu ili ahudhurie harusi, halafu waje wamchuke, Pilato alisema that was one of the biggest joke of his time! na hata sahau maana inaonyesha jinsi hawa mafisadi wasivyo na heshima kwa serikali na sheria kwa ujumla!
 
Back
Top Bottom