Mramba: Another Challenge!

hawa wanaomtetea Mramba wametumwa! Naona siasa za Kenya zinaanza kushika mizizi Tanzania kuna watu hapa hoja zao ni barabara waliyopelekewa huko Rombo na si kiasi gani anatakiwa kuwa accountable kwa upotevu wa fedha za walipa kodi wa nchi hii! Tuache siasa za ubinafsi jamani hako kamtu kanapaswa kawe Keko sasa! Rombo kuna watu zaidi ya 200,000 na katika hao lazma kutakuwa na wenye sifa za uongozi bora yaani kuchukua barton na kuliepusha jimbo na balaa la kutengwa kwake na serikali na bunge maana hawamtaki! Hizo hela zake anazotaka kuhonga ni bora awekeze maana atabwagwa hata akipita ndani ya CCM!

Mkuu,

Unajua unaposhindwa kujenga hoja na kukimbilia kwamba watu wametumwa unadhalilisha huu mjadala .Sasa na wewe unaemtetea huyo mama umetumwa na nani?

Je,wewe umeona kumtetea Mramba ni kama siasa za Kenya?mkuu ujue kuna watu ambao tuko hapa kujali maendeleo in regardless yanaletwa na mtu kutoka chama gani?

Jaribu kujenga hoja tujadili hawa wagombea na CV zao tuachane na kujadili waungwana wa hapa jamvini.Nimerudia tena,hoja hapa ni za wagombea ubunge wa rombo na title ya Thread inasema...MRAMBA:Another challenge"...akaletwa netburga.so jadili hawa watu na jimbo la Rombo.Salute
 
Siasa za Kenya kwa vile ameiba ila baadhi ya wanajimbo wake hawaoni hilo, ila kumuita mjanja! Kivipi bwana Ben? Mi namfananisha na Prof. Onderi (Waziri wa Elimu) na suala la fedha za elimu bure kwa watoto maskini wa Kenya, mbali ya auditing ya Price House water Coopers kung'amua ubadhirifu wa hali ya juu uliosababishwa na ku-channel fedha za maendeleo kwenye jimbo lake, wa-Kisii yaani wanajimbo lake bado wanamkingia kifua! hizi si siasa chafu mnazotaka kuleta katika nchi hii ya Nyerere!
 
- Ahsante sana!

Respect.

FMEs!
 
Sitetei huyo mama tu kama ukiangalia vizuri nimesema Rombo ina watu 200,000 na naamini watajitokeza wengine zaidi! ninachopinga ni Mramba akae pembeni asuluhishe Kesi yake for the good of you guys!

- Mkuu wangu hebu ongea on sherias line, Mramba kugombea anavunja sheria yoyote ya jamhuri yetu?

FMEs!
 
- Mkuu wangu hebu ongea on sherias line, Mramba kugombea anavunja sheria yoyote ya jamhuri yetu?

FMEs!
Yes ni kwa vile hatuna ustaaarabu huko Tanzania mtu mwenye mashtaka mahakamani hawezi kugombea jimbo lolote kwa nchi zenye demokrasia na zilizoendelea! what if atashinda uchaguzi na on verdict day is withheld to serve a jail sentence! Who will represent that constituent? unafikiria hilo au ushabiki wako tu mzee? kwanini wewe usigombee? au una kesi nawe? kuna watu chungu nzima wanaweza tawala kwa hilo jimbo tangu nizaliwe hako kamtu kako kabunge jamani hamna wakina Obama au Angela Merkel huko?
 
yebo yebo ukiamua kutuliza akili zako huwa unaandika vitu vya maana sana.lakini wakati mwingine huwa sikuelewi kama vile ulivyosema kuwa shayo ni associate professor nilikushangaa sana.

Mkuu,

Wapi huko umesoma nimeandika kuwa Dr Shayo ni Associate Professor?
 
Ndio Mramba ni msomi na mjanja.

Mramba ana weakness zake pia.

Kwanza mramba anawajali baadhi ya matajiri wachache wa Rombo, na anawabagua matajiri wengine.

Kibaya zaidi amewasahau wananchi wa kawaida.

Ameshindwa Tatizo la Maji kwa ukanda wa chini kabisa. Tatizo la maji lipo Tangu mwaka 1995 na halijapata ufumbuzi.

Wameleta kampuni ya Kili water, imesambaza mabomba kwa mchango wa nguvu za wananchi. Lakini hakuna hata siku moja mabomba hayo yametoa maji.Hakuna maji kabisa.

Afya: Afya bado sana. Hakuna Hospitali Ya serikali, Huruma ni ya Missionary.

Mtu akiwa Rongai au Tarakea na anaumwa itakuwaje, na hakuna ambulance???

Mashule: Mashule yamejengwa kwa nguvu za wananchi.

Ila suala la Maji ni issue kubwa na ni Tatizo sugu.

Sasa kwa miaka kumi akiwa Mbunge na Waziri alishindwa kutatua tatizo la Maji?

Kuanzia 2010 hadi 2015 ndo atafanya miujiza? na atakuwa hana nguvu bungeni kwa sababu ya kesi ya ufisadi.

Jiulizeni

Hapo kwenye bold/red mkuu, umegonga mpaka ikulu...!!
 
Yes ni kwa vile hatuna ustaaarabu huko Tanzania mtu mwenye mashtaka mahakamani hawezi kugombea jimbo lolote kwa nchi zenye demokrasia na zilizoendelea! what if atashinda uchaguzi na on verdict day is withheld to serve a jail sentence! Who will represent that constituent? unafikiria hilo au ushabiki wako tu mzee? kwanini wewe usigombee? au una kesi nawe? kuna watu chungu nzima wanaweza tawala kwa hilo jimbo tangu nizaliwe hako kamtu kako kabunge jamani hamna wakina Obama au Angela Merkel huko?

- Mkuu basi hii kitu ni very simple ni mgombea anayetaka kumtoa kumuacha ashinde ahalafu aende kwenye sheria kwamba Mramba amevunja sheria kama amevunja kweli si ni ishu simple sana au?

- Ninakuona ukijaribu sana kuigeuza hii ishu kuwa personal, mimi sio mwananchi wa Rombo na siku zote ninasema hivi hebu yageuze hayo maneno yako ya personal iwe wewe kwanini wewe hugombei au na wewe una kesi hii itawasaidia nini wananchi wa Rombo mkuu? Hapa ninapoishi jirani yangu mmoja aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chadema huko Rombo ndio maana ninakushangaa sana na unayoyasema bila kufikiri wala kujali ukweli wa huko Rombo,

- Ananiambia kwamba tatizo la Mramba huko Rombo ni Salakana, ambaye kwa sasa hana ubavu tena, kwa hiyo Mramba atashinda tena,au? Kama huna la maana ndugu yangu waachie wengine tuendelee mambo yako ya binafsi hapa hatuyahitaji samahani sana!

Acha hasira wewe! Mramba hana chake pale, naona umekazania tu ati nina-turn mambo personal ki-vp? nimekuuliza katika watu zaidi ya 200,000 hamna mtu anayeweza kutawala huko mpk ung'ang'anize hako Kajizi! Niimekuuliza considering ethical background ya Mramba unayemtetea who doesn't deserve to stand for any post in Tanzania!
 
Siasa za Kenya kwa vile ameiba ila baadhi ya wanajimbo wake hawaoni hilo, ila kumuita mjanja! Kivipi bwana Ben? Mi namfananisha na Prof. Onderi (Waziri wa Elimu) na suala la fedha za elimu bure kwa watoto maskini wa Kenya, mbali ya auditing ya Price House water Coopers kung'amua ubadhirifu wa hali ya juu uliosababishwa na ku-channel fedha za maendeleo kwenye jimbo lake, wa-Kisii yaani wanajimbo lake bado wanamkingia kifua! hizi si siasa chafu mnazotaka kuleta katika nchi hii ya Nyerere!

Mkuu,

Suala la kashfa ya ufisadi liko mahakamani

Ukifuatilia post zangu,kama uko makini utaona msimamo wangu kuhusu Mramba ni nini.

Pia Mramba hela anazotuhumiwa nazo,narudia tena ANAZOTUHUMIWA nazo hakuzipeleka Rombo.So wewe kumfananisha na Prof.Sam Ongeri ni irrelevant na usiingize ukabila ktk huu mjadala.

Narudia tena,Mramba kutuhumiwa hakumfanyi awe zezeta au msaada wake wa kimawazo katika kuliongoza hilo jimbo si haramu!
 
Yes ni kwa vile hatuna ustaaarabu huko Tanzania mtu mwenye mashtaka mahakamani hawezi kugombea jimbo lolote kwa nchi zenye demokrasia na zilizoendelea! what if atashinda uchaguzi na on verdict day is withheld to serve a jail sentence! Who will represent that constituent? unafikiria hilo au ushabiki wako tu mzee? kwanini wewe usigombee? au una kesi nawe? kuna watu chungu nzima wanaweza tawala kwa hilo jimbo tangu nizaliwe hako kamtu kako kabunge jamani hamna wakina Obama au Angela Merkel huko?

So,hapa ndipo ulipoongelea on sherias line?

Kwa hiyo tatizo hapa ni Mramba?
 
Nani kakwambia kama baba alishindwa basi na yeye hafai ?? Acha chuki za namna hiyo. Kama anafaa au hafai kura zitaamua.
Nanfahamu huyu binti ni mchapakazi na mwenye uchungu na nchi yake . amekukuwa akiyakemea maovu kila anakopita kama baba yake mzazi ambaye alikuwa mbunge wa kwanza machachari kisiasa naamini waliokuwa nae bungeni miaka hiyo watakubali na ndio maana mramba kabla hajawa fisadi alimchagua kuwa kampeni meneja wake ...naamini kama siasa inarithiwa basi huyu binti atakuwa muadilifu na mchapakazi atakayeleta maendeleo makubwa katika wilaya ya rombo... big up sana Notburga usiogope wanaoweka chuki binafsi kaza buti....
 
Acha hasira wewe! Mramba hana chake pale, naona umekazania tu ati nina-turn mambo personal ki-vp? nimekuuliza katika watu zaidi ya 200,000 hamna mtu anayeweza kutawala huko mpk ung'ang'anize hako Kajizi! Niimekuuliza considering ethical background ya Mramba unayemtetea who doesn't deserve to stand for any post in Tanzania!

- Haya maswali yako waulize wananchi wa Rombo ambako anaelekea Mramba atashinda tena ubunge!

ES!
 
Uhai wa kisiasa wa mh.basil mlamba kule rombo unadhihirika kwa namna walivyojitolea ktk kesi yake na nidhamu waliyoionyesha kwa mwakilishi wao hata pale alipotuhumiwa na kupelekwa mahakamni. Hatujaona mabezo wala kejeri dhidi yake toka rombo+ kilimanjaro as a region. Ni vema yeyote anayetaka kupambana naye alifahamu hilo kwa kina kabla ya kujiingiza ktk uadui na jamii yake na hatimaye kupeperusha hata fursa yake 2015. Ni tofauti na sisi moro ambako mtu wetu akipata fursa za kupaa kidola basi sisi wenyewe hutumika kumpopoa na mawe ya chuki na kejeli mpaka kumchusha ktk medani. Big up rombo-kilimanjaro except mwanga wanaoiasisi dhambi ya kimorogoro morogoro, maana magembe ameundiwa zengwe la kung'olewa sababu za msingi hakuna!!!!!

To me mlamba still stand a chance for those rombo people na zaidi ili kujilinda na haya yanayomuandama ni lazima akomae kwenye siasa mpaka tenure ya kikwete
 
Mramba na Kimaro wakimbilia kanisani

Salome Kitomary

Mbunge wa Rombo, Basil Mramba, ametumia fursa ya kuwahutubia wachungaji 42 wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) kwa kujitakasa kwamba yu mtu safi na mchapa kazi na kwamba ataendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Sambamba na Mramba, pia Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro ambaye aliitisha mkutano wa wachungaji hao ulioanza saa 4:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni, aliwasilisha rasmi maombi ya kutaka wamsaidie kuwasilisha ujumbe kwa waumini wao kwamba anakusudia kuwania tena ubunge katika jimbo hilo.
Katika mkutano huo ambao ni nadra kutokea katika kipindi hiki cha kupanda kwa joto la uchaguzi, Mramba na Kimaro, walitumia jukwaa hilo kujisafishia njia ya kuwania ubunge huku Mramba akitamba hakuna wa kumzuia isipokuwa kama tu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikimkataa.
Wachungaji hao wanatoka Jimbo la Kilimanjaro Mashariki la Dayosisi ya Kaskazini ya kanisa hilo linalojumisha sharika kutoka wilaya za Rombo na Moshi Vijijini.
Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya jimbo hilo, Himo, Mramba ambaye aliwasili ukumbini saa 7:00 mchana na kulakiwa na Kimaro, alisema si kila mwanaume anayevaa suruali au mwanamke anayevaa sketi anastahili kuwa mbunge na kuwataka wananchi kuwa makini na watu wanaojipitisha pitisha katika majimbo yao.
Mramba alisema ingawa anakabiliwa na kesi mahakamani ambayo imempunguzia muda wa kuwahudumia wapigakura wake, bado anakubalika katika jimbo lake na hiyo inatokana na jitihada zake za kuwatumikia wananchi kwa moyo wake wote kuhakikisha wanajikwamua dhidi ya wimbi la umaskini.
"Siasa sio kamari, kuwa kiongozi ni lazima uwe na wito fulani ndani yako na vile vile siasa ni kazi mbaya," alisema bila kufafanua.
Aidha, aliwaponda baadhi ya wabunge ambao kwa sasa wanahaha katika majimbo yao kwa kurudi kuwabembeleza wananchi dakika za mwisho ili hali muda wao wa miaka minne waliutumia kwa kukaa jijini Dar es Salaam na kuishi maisha ya starehe.
"Wabunge wengi hawaendi kwenye majimbo yao kwa ajili ya kufanya mikutano na kujua kero za wananchi, wametoa ahadi lukuki, lakini hakuna walizotekeleza na kwa sasa ndio wanahaha..haya ni mambo ya kutisha sana kwani ni wachache sana wanaopata ubunge na kutatua kero," alisema.
Mramba alisema viongozi wanaandaliwa na hawaibuki tu kwa kuwa si kila mtu anaweza kuwa kiongozi na kama Mungu amepanga mtu awe kiongozi atakuwa tu hata wanadamu wakiweka vizuizi.
Alisema baadhi ya watu wanadhani kuwa mbunge ni mtu mwenye uwezo bila kujua kuwa mbunge ni yule ambaye ana nia ya dhati na uwezo katika kuwakwamua wananchi kwenye lindi la umaskini.
Alisema aliteuliwa na Mwalimu Julius Nyerere kama mbunge wa kuteuliwa miaka ya 80 ambapo alitumia miaka mitano kujifunza na baada ya hapo alikuwa mzoefu na kwamba kila mara anakumbuka kauli ya Mwalimu Nyerere iliyomwambia 'mimi nastaafu ila wewe baki Rombo wasaidie wananchi wa Rombo'jambo ambalo amekuwa akilifanya hadi sasa.
Alisema kuwa yeye ni mzoefu katika utumishi wa umma na ubunge na amefanya kazi na marais wote wa awamu nne.
"Dunia ina watu wazuri na wabaya, tunaishi nao na tunafanya kazi nao, mimi ni mzoefu wa kushtakiwa na hilo halinikatishi tamaa ya kuwatumikia wananchi wangu ambao bado wana imani kubwa na mimi," alisema Mramba.
Mramba anakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa Waziri wa Fedha kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.
Akimzunguzia mbunge huyo, Mchungaji Elias Sillayo, alisema alimfahamu miaka ya 80 akiwa usharika wa Mengwe na kwamba wananchi bado wanamuhitaji na wanaomba kesi yake imalizike haraka ili aendelee kuwatumikia.
Naye Kimaro akizungumza na wachungaji hao alisema utumishi wa umma si fursa ya kunufaisha mtu binafsi, rafiki, wapambe na si fursa ya kutukuza itikadi za kisiasa.
Alisema utumishi wa umma ni dhamana na fursa adimu kwa ajili ya kulinda na kutetea maslahi ya wananchi wote.
Kimaro alisema daima ataendelea kuwa mkweli kwani mtu anapokosea asipoambiwa kuwa amekosea ni kutenda dhambi na anapoona maovu na kutokusema ni kumkosea Mungu na ndio maana amekuwa akisimama kidete bungeni na kuwaeleza.
Wachungaji hao kwa kauli moja waliunga mkono kazi zilizofanywa na Kimaro na kuahidi kuhakikisha anarudi tena jimboni kwa kusoma maazimio yao.
Akisoma azimio la wachungaji hao kutoka katika sharika za jimbo hilo, Mchungaji wa Usharika wa Karimeni Mwika, Elias Sillayo, alisema kwa kauli moja wachungaji hao wataenda kuwaeleza waumini wao kuwa mapungufu yaliyopo yanarekebishwa hivyo ni vyema wakampa nafasi nyingine ya uongozi.
Alisema kipindi cha miaka mitano amejitahidi kufanya mambo mengi na alitumia muda huo kujifunza hivyo ni vyema wakampa nafasi ya kumaliza aliyoyaanza.
Mchungaji Sillayo aliongeza kuwa jimbo hilo linahitaji viongozi bora na si bora viongozi na kuhoji kama wanaweza kuchagua viongozi wazuri wa kanisa ni kwanini washindwe kuchagua viongozi wazuri wa jamii.
"Mbunge wetu huyu tumpe nafasi nyingine ya kutuwakilisha bungeni," alisema.
Aidha, wachungaji hao walimtaka mbunge huyo iwapo atapata ridhaa ya wananchi katika kipindi kingine atekeleze ahadi zote alizoahidi.
Alisema wachungaji hao wanafanya ibada maalum kwa ajili ya kuombea uchaguzi mkuu wa Oktoba ili uwe wa amani na utulivu ikiwa ni pamoja na wananchi kufunuliwa katika kuchagua kiongozi mwenye nia ya kuwaletea maendeleo na si kujinufaisha binafsi.
Mkutano huo ulifanyika chini ya uenyekiti wa Mkuu wa jimbo hilo, Mchungaji Luca Kessy.
Akiwakaribisha wachungaji hao, Mchungaji John Mlay alisema kila serikali ni lazima imkubali Mungu kwani hakuna serikali inayoweza kufanikiwa bila kumtambua Mungu kwani pasipo yeye hakuna serikali inayoweza kusimama.
"Tambueni kuwa mnaongoza kwa niaba ya Mungu, pasipo Mungu hatuwezi lolote na ni vyema tukawa macho uchaguzi usitufikishe katika machafuko ya kupoteza lulu ya amani na utulivu iliyopo kwa sasa," alisema.
Mbali na wachungaji na wabunge hao, pia mkutano huo ulihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Musa Samizi, ambaye aliwataka viongozi wa dini waombee amani wakati nchi inapoelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Alisema Serikali inatambua mchango wa makanisa katika elimu, afya, maji kwani yamekuwa yakitoa huduma bora ndiyo maana shule zake ni bora katika kufaulisha.
Alimsifu Kimaro kwa kusema Vunjo wana bahati ya kuwa na mbunge muwazi kwani kama mtu ni mlarushwa anampa wazi kuwa ni mlarushwa; ni jasir.
Pia alikuwapo Katibu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Stephen Kazidi, ambaye aliwataka viongozi wa dini kutokukubali makanisa kutumika kama majukwaa ya kisiasa; wasaidie kuhubiri amani; waonye wanaoleta chokochoko; wasikubali nchi kuingia katika machafuko kama majirani zetu. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Katibu CCM Wilaya ya Moshi, Kingazi, ambaye hakusema kitu. Mkutano huo ulifungwa saa 12 jioni.

NIPASHE
http://www.ippmedia.com/frontend/fun...le.php?l=14107
 
At time we are talking about Raisi na mawaziri wake wameifanyia nini nchi na tunafanya assessment.
As well tunaweza ongelea Mbunge amefanyia nini jimbo na tunafanya assessment

Ni muhimu katika mjadala huu tukaweza tofautisha the role of Mramba kama mbunge wa jimbo lake ana role of him kama waziri.

Kama hatutatofautisha, kamwe hatutaweza elewana kutokana na hoja zinazoibuka kwenye mjadala huu. Nina imani hapa tunamjadili Mramba kama mbunge na ndipo assessment ya alichokifanya kule jimboni kinatakiwa kijadiliwe bila kufikiri kuwa yeye ni alikuwa waziri akiitumikia nchi.

Si kusema namkubali Mramba 100% katika jimbo issues la hasha... lakini kuna mengi aliweza kufanya kama alivyo ahidi. Ila nisinge penda kabisa aendelee kutuwakilisha....lets have someone else.
 
-Mkuu shapu,

Hizo ndizo hoja ambazo wakulu wengi wameshindwa kuzielewa.I salute you bro.hata mie sitaki Mramba aendelee kutuwakilisha lakini akienda kwenye kampeni bado anaweza kupeta kama hakutakaua na real challenge against him
 
Kama zile barabara za Marangu - Mkuu Rombo -Tarakea, Mwika - Kilacha, Tarakea - Kamwanga zinaelekea kuisha.....kutakuwa na kazi kubwa sana ya kumuondoa huyu Mramba....labda watumie vigezo vya scandali zake CCM wasimpitishe......

Kwani fedha za mamayake?
 
Back
Top Bottom