Mramba anasafishwa?

Ni kweli mwaka 1995 Mramba alibwagwa vibaya na Mgombea wa CHADEMA Bw.Alfred Justine Salakana.

Hata hivyo,hayo mapokezi ya huko Rombo itakua dili limechezwa na wananchi wakaingizwa mkenge tu.Hao mafisadi wanajiandalia mapokezi wenyewe kwa wenyewe halafu wananchi wanaingizwa mkenge.

Hata wafanye nini mwaka ujao Mramba harudi Bungeni
 
Ni mwakilishi wao ambaye walimchagua kwa kura zao, acheni wafanye watakavyo maana mwisho wa siku wao ndio waombolezaji
 
- Semo semo mafisadi's style, ilianzishwa na Lowassa, Mkapa, Chenge, now Mramba kwenda kuwadaganya wananchi wa jimboni, maana huku mjini hakuna wa kumpandisha mkenge, akirudi mjini kesi Kisutu iko pale pale, mpaka kieleweke!

- Hivi jamani si nimewahi kusikia kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa kuwa na shule nyingi za secondari na elimu Tanzania au? Kuwa na shule yningi sio guarantee kua wananchi watakuwa na na elimu? I mean this mapokezi ya fisadi is beyond imagination!

Mkuu suala la kutafuta elimu na suala la kuwa na shule nyingi ni vitu viwili tofauti Kilimanjaro kuna shule nyingi sana jiulize wanaosoma/waliosoma hapo ni akina nani sio wachagga ni watu wa makabila tofauti pasipo ubaguzi au ukabila. Suala la B. Pesambili Mramba kutuhumiwa ufisadi na hiyo Alex Stewarts lisiwe kigezo cha kumfanya asitembelee wapiga kura wake. Mcheza kwao hutuzwa. Ieleweke Mramba katika hili hayuko peke yake hii ni chain ya watu ambao wanajulikana na wengine ambao hawajulikani. Isitoshe yeye kama kiongozi inawezekana pia alipotoshwa. Kwa hiyo nasema kumhukumu mtu moja kwa moja sio vizuri ijapokuwa watanzania bado wana maswali mengi juu yake kutokana na kauli zake . Simtetei Mramba ila inabidi tubadili mtazamo kwa namna moja ua nyingine.
 
Waache wampokee kwa Ndelemo bse walifaidika na huo wizi,sioni cha kushangaza apo?
 
....mwacheni bazil wa watu.......si unajuwa ana wenyewe....kule ni kwa wazazi na watoto wake ........hata kama angalikuwa mchafu kama greese...wangempokea na kumsafisha akangaa kama dheluji......

..wakristo tunasema ni furaha kubwa kwa mwenye kondoo pale mmoja anapopotea na kupatikana....,au kuna kisa cha mjane aliyepoteza sarafu.....na akawasha taa na kuanza kutafuta...

malizia na mwana mpotevu aliyerudi nyumbani ....namna alivyopokewa kwa shangwe[mali zake alikuwa ametawanya na marafiki]..baba aliagiza avalishwe vazi lililobora.......hata watu wate walikaribishwa wakala na kunywa.....

kimsingi hakuna kosa kumpokea kwa furaha ndugu yako aliyekuwa na matatizo .....huwezi kumnyanyapaaa...tena ndio wakati wa kumkumbatia....
kwani hii itamsaidia na yeye kutubu na kujutia makosa...
 
Njaa, shida, na kukosa matumaini ni kitu kibaya sana...

Na hii yote inachangiwa na dhambi moja,kuwagawa watu kikabila..Watu wa Moshi wanambiwa watu wanaona wivu kuwa wachaga wana Maendeleo.

Hata chenge alivyorudi Bariadi hivyo hivyo.Kazi kweli kweli

Watu walishalishwa Upupu wenye maneno ya pongezi.Mtu mbaya na mwizi anaonekana mzuri mbele ya jamii,Tena anaweza kupokelwa na Mchungaji au hata vskofu kama livyopokelewa Lowassa!
 
Karibu Nyumbani Mh. Mramba, tunategemea haki itatendeka na kesi inayokukabiri utashinda na baada ya hapo tutaanza mchakato wa uchaguzi 2010 au siyo Mh? Sisi wananchi wa Rombo hatuli NYASI bali mifugo yetu ndiyo inakula MAJANI. Mh hapa Rombo tunaishi kama vile tuko Texas au Melbourne, kwa maana huduma nyingi za kijamii tunazipata, kuanzia matibabu, shule, maji SALAMA, umeme, ma-Barabara, BIA (zingine kutoka Kenya) na kisusio tunakula kama kawaida. Hivi Mh, hawa jamaa wa Darisalamu kwa nini wanakuita FISADI? Hawa jamaa hawakutakii mema au ni NJAA zao kali?

Tunatumaini baada ya uchaguzi 2010 utashinda kwa KISHINDO na kwa maana CCM (M=????) ina wenyewe, utateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania UN au UK au popote pale duniani na maisha yateendelea kama kawaida Mh.

Karibu SANA Rombo na Mungu akubariki
 
Mwakyembe alipoandaa ripoti nzuri ya Richmond, wapiga kura wake walimuandalia mapokezi makubwa, lakini kuna watu walimuwekea vikwazo kibao na mikwara juu kwa watakaotoa sapoti. Watuhumiwa wa ufisadi wanarudi majimboni kwao kwa kuandaliwa mapokezi makubwa, lakini hakuna anayewawekea vikwazo. Nadhani unaweza kupata picha fulani hapo !!
 
Wafuasi wa hawa watu hawaelewi wanachokifuata, mwisho wa siku wanajikuta wapo katika hali ile ile na mheshimiwa yumo kwenye gari la kiyoyozi wao wapo nje wengine miguu peku wanashangilia ukiwauliza wanashangilia nini hawana jibu la maana.
 
- Semo semo mafisadi's style, ilianzishwa na Lowassa, Mkapa, Chenge, now Mramba kwenda kuwadaganya wananchi wa jimboni, maana huku mjini hakuna wa kumpandisha mkenge, akirudi mjini kesi Kisutu iko pale pale, mpaka kieleweke!

- Hivi jamani si nimewahi kusikia kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa kuwa na shule nyingi za secondari na elimu Tanzania au? Kuwa na shule yningi sio guarantee kua wananchi watakuwa na na elimu? I mean this mapokezi ya fisadi is beyond imagination!

Mkuu FMES upo sawa...
Tatizo sisi watanzania kama vile tumelishwa kitu...Tunaona lakini hatuelewi,tunasikia lakini hatufahamu..Kwamba na Mramba ameandaliwa mapokezi makubwa kama wenzake ni jambo lakutia kichefuchefu.Waendelee kuwadanganya wanachi,waendelee kutupaka mafuta kwa kgongo wa chupa,waendelee kututukana lakini yanamwisho wake.Mtaji wa CCM ambao upo vijijini utameguka,kwao itakuwa kilio na kusaga meno!
 
Ni kweli kabisa Kichuguu. Hili linasikitisha sana. Kwanza Lowassa alipewa mapokezi ya nguvu baada ya kujiuzulu kwa kashfa ya Richmond/Dowans, akafuata Mzee wa Vijisenti naye akapewa mapokezi ya nguvu kwenye jimbo lake na sasa Mzee wa "Hata Majani tutakula lakini Rada ni lazima inunuliwe" halafu CCM imeyafumbia macho na kukaa kimya kabisa kuhusu mapokezi haya ya Watuhumiwa. Halafu wakati huo huo inajitangaza inapambana na mafisadi!!!!
Huyu angepewa masharti na korti unaenda kwenu basi hustahili kupokewa kwa mapokezi makubwa lakini kaachiwa tu sasa anapeta!!! Bongo inastaajabisha kweli kweli!!!

Ninaamini kabisa wengi wa watakao mpokea fatafanya hivo sbb tu ta uoga kwa wale wachache wanaojipendekeza kwa mramba mwenyewe kwa ajili ya manufaa yao binafsi, jamani mi nnavojua mramba hapendwi kabisa rombo na walo wengi, ama sivyo pesa hapo itatumika kama alivotumia lowassa kwao...
 
Hii ni dalili tosha kwamba vita dhidi ya ufisadi haijawafikia wananchi wetu. Ebu imagine wakati wa vita vya wahujumu uchumi, eti mtuhumiwa anapokewa na wananchi?

Hawa viongozi waliofunguliwa mashitaka na serikali ilitakiwa wajiuzulu hata huo ubunge. Hii sio case ya madai, ni case ya wao kushitakiwa na serikali yao, kweli wanafaa kuendelea kuwepo bungeni?

Mwizi anapokewa kwa shangwe? Kweli sisi Miafrika ndivyo tulivyo, wajingaaa!!! labda sasa tunazidiwa na Waarabu tu, ndugu zao Wapalestina wanapigwa, wao wanafunga mipaka!
 
Ni kweli mwaka 1995 Mramba alibwagwa vibaya na Mgombea wa CHADEMA Bw.Alfred Justine Salakana.

Hata hivyo,hayo mapokezi ya huko Rombo itakua dili limechezwa na wananchi wakaingizwa mkenge tu.Hao mafisadi wanajiandalia mapokezi wenyewe kwa wenyewe halafu wananchi wanaingizwa mkenge.

Hata wafanye nini mwaka ujao Mramba harudi Bungeni

Masahihisho kidogo Mkuu.

Salakana alishinda kiti cha Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA mwaka 1990 na si mwaka 1995. Na alishika kiti hicho kwa term moja tu.
 
Utaendeshaje vita dhidi ya ufisadi kama wananchi sisi wenyewe tunasema pole kwa kushikwa kwa ufisadi lakini hongera sana, siku nyingine uhakikishe hushikwi!!!!!!!!!


kwi kwi point well said , yani hapo ndio nashindwa kuelewa na kushangaa jinsi gani sisi binaadamu tulivyo. yani mtu ana kesi ya upotevu wa pesa zenu wenyewe (wananchi) halafu eti mna shangilia duh !!! hii kali only in TANZANIA !!!!!
 
Tofauti kati ya Janet na Sophia ni kwamba Janet ana mume Mzee Kahama na Sophia ni msela tu hana mume kwahiyo kumpa uongozi wa aina yeyote hasa serikalini anakuwa ni security risk!!!.Anawezakupambana na njemba fulani ikamchanganya akauza siri za nchi!!
 
Back
Top Bottom