Mramba achaguliwa Mwenyekiti Bodi ya TANROADS MKOA.

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,126
MBUNGE wa Rombo, Basil Mramba, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Kilimanjaro.

Mramba ambaye amepata kuwa Waziri wa Fedha wakati wa Serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa, alichaguliwa kushika wadhifa huo jana wakati wa kikao cha bodi hiyo kilichofanyika mjini hapa.

Mbunge huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya ufisadi ya matumizi mabaya ya fedha za serikali zaidi ya sh bilioni 11.7 wakati akiwa Waziri wa Fedha, atashika nafasi hiyo chini ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambaye kwa utaratibu mpya wa serikali, ni mkuu wa mkoa huo, Monica Mbega.
 
Hii huwezi iona sehemu yeyote duniani isipokuwa TZ tu,kiongozi mwenye kesi kubwa mahakamani juu ya matumizi mabaya ya pesa za walalahoi;anachaguliwa tena kusimamia maamuzi ya matumizi mengine ya pesa bila kungoja hatma ya kesi yake iishe?

Why Mramba?Kilimanjaro as a region,they dont have any other potential candidates to hold that substantial post?Shame on them TANROADS kulea mafisadi!!
 
Kama hii ni kweli basi sasa tumefanywa wajinga wa kutupwa. Mtu ana kesi mahakamani ya wizi wa fedha halafu ana pewa wadhifa kama huo? ONLY IN TANZANIA, THE LAND OF KILIMANJARO & UFISADI!
 
Mnashangaa nini? Mbona Patel ana kesi ya kujibu lakini alipewa tenda kubwa kabisa ya kuingiza matrekta kwa ajili ya wakulima? Hao wote ni jamaa zake JK. Na ninafikiri kwa kukubali kwao kudhalilika kwa kusimama mahakamani watalipwa mipesa ya kumwaga. Acha tuendelee tu kujipa mahope kwamba JK amewashitaki mafisadi. Tumepigwa changa la macho wanawane!
 
Kama hii ni kweli basi sasa tumefanywa wajinga wa kutupwa. Mtu ana kesi mahakamani ya wizi wa fedha halafu ana pewa wadhifa kama huo? ONLY IN TANZANIA, THE LAND OF KILIMANJARO & UFISADI!

Je mmesahau kuwa Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu!!!!!
 
Kama hii ni kweli basi sasa tumefanywa wajinga wa kutupwa. Mtu ana kesi mahakamani ya wizi wa fedha halafu ana pewa wadhifa kama huo? ONLY IN TANZANIA, THE LAND OF KILIMANJARO & UFISADI!
Si utani tena Kilimanjaro yenyewe iliyotakiwa iwe mfano?Teh teh teh!Ndio imekuwa mfano wa ufisadi moja kwa moja...Hata hivyo ni muhimu tuwajuwe hao wanabodi,maana mafisadi wako kila mahali na wanajuana,ama labda wanabodi hao wanataarifa za kiundani kwamba kesi ya Mramba ni usanii tu?
 
..watu tukisema CCM imeoza mnafikiri tunatania.

NB:

..hivi kwanini serikali hawaidai Alex Stuart fedha za tax exemption waliyopewa na Mramba na Mgonja?
 
- Ni lazima ujue kwanza forces zilizohusika kumtoa kwa dhamana, the dataz ni kwamba nguvu kubwa ya ukabila ilitumika tena na wenye nafasi kubwa sana Nationally sasa na zamani, sasa hii ni in your face message kwa Muungwana na waziri wake wa sheria, don't you dare again!

- Nani anabisha?

Respect.

FMEs!
 
FMES,

..kwa kweli hili suala la ufisadi ili Muungwana aonekane yuko serious angeburuza mafisadi wooote na kuwatupa segerea.

..yeyote yule ambaye alizembea kazi na serikali ikaingia hasara alipaswa kuwa mahakamani sasa hivi.

..binafsi naona kuna watu wanajiuliza: mbona kuna mafisadi wako mtaani na wamesababisha hasara zaidi ya hiyo bilioni 11 iliyompeleka Mramba & Co mahakamani?

..wenye kuuliza maswali kama hayo ndiyo wanaom-challenge JK na serikali kwa kumchagua Mramba kwa nafasi kama hiyo.

..na kesi yao isipoamuliwa kabla ya 2010 usijeshangaa CCM-Rombo wakarudisha jina la Mramba bila kupingwa.

..binafsi mpaka leo najiuliza ikiwa Mramba,Yona,na Mgonja, wanashitakiwa kwa kutoa tax exemption illegally kwa kampuni ya Alex Stuart kwanini serikali haiendi hatua moja mbele na kujaribu ku-recover fedha hizo?
 
- Ni lazima ujue kwanza forces zilizohusika kumtoa kwa dhamana, the dataz ni kwamba nguvu kubwa ya ukabila ilitumika tena na wenye nafasi kubwa sana Nationally sasa na zamani, sasa hii ni in your face message kwa Muungwana na waziri wake wa sheria, don't you dare again!

- Nani anabisha?

Respect.

FMEs!

Heshma mbele Field Marshall ES; Unasema "Nguvu kubwa ya ukabila" iliweza kumtoa kwa dhamana na hiyo nguvu ya ukabila kama "in your face message" ndiyo inamtisha muungwana na waziri wake wa sheria...How?
 
Yaani Majambazi na Mafisadi wa CCM wanazidi kupeana tu, R.I.P TANZANIA.
 
Heshma mbele Field Marshall ES; Unasema "Nguvu kubwa ya ukabila" iliweza kumtoa kwa dhamana na hiyo nguvu ya ukabila kama "in your face message" ndiyo inamtisha muungwana na waziri wake wa sheria...How?

- Mkulu Mushi, heshima yako bros nani amempa Mramba hii nafasi ya kuwa makamu wa RC, aliyechaguliwa na Rais? Halafu masuala mengine ni logic zaidi kuliko facts of the matter, hivi Tanzania nzima mafisadi ni yona, Mramba, na Mgonja tu? Na wote ilikuwa ni lazima wawe kutoka Kilimanjaro tu kama mfano kwa taifa why not makabila mengine?

- Now think about it, then utaelewa ninachosema ambayo ni maoni yangu tu!

Mkuu labda ungestick na point moja ya "Mkoa" badala ya ukabila kwa sababu wote uliowataja hapo juu niliowa highlight ni makabila tofauti to begin with.....Na kama hayo ndiyo maoni yako, basi nimeelewa.
Pia kwenye pointi ya kwanza naomba usisahau tena nilipokuuliza kwamba ni kivipi nguvu hizo za "mkoa" zilikuwa "a slap in his face?" pamoja na madai kwamba zitamzuia ama zinamzuia muungwana na waziri wake wa sheria kutekeleza majukumu yao....?Mwisho,kama bado unaamini kwamba ni "nguvu ya ukabila"(jambo ambalo siamini kwasababu uliowataja si kabila moja,Yona na mgonja ni wapare na Mramba ni mchaga)je ni kivipi nguvu hiyo ni tishio kwa maamuzi ya JK na waziri wake wa sheria?
Ningelishukuru.lol!
 
MBUNGE wa Rombo, Basil Mramba, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Kilimanjaro.

Mramba ambaye amepata kuwa Waziri wa Fedha wakati wa Serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa, alichaguliwa kushika wadhifa huo jana wakati wa kikao cha bodi hiyo kilichofanyika mjini hapa.

Mbunge huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya ufisadi ya matumizi mabaya ya fedha za serikali zaidi ya sh bilioni 11.7 wakati akiwa Waziri wa Fedha, atashika nafasi hiyo chini ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambaye kwa utaratibu mpya wa serikali, ni mkuu wa mkoa huo, Monica Mbega.
Malafyale,
Mbona haya ni ya Musa tu, Subirini ya Firauni(Farao) yako njiani. Kwani hamjasikia kuwa kufa kwa Msamba mavi hutawanyika??
 
Hivi ni Mungwana yupi atawapereka mafisadi segerea. Bado mna tumaini kuwa iko siku huyo mungwana wenu atawapereka. Pole sana Tanzania.
 
Hii kali sana kuliko zote!!wanapima upepo hata kwa EL kuja kumpa nchi ck moja ......
 
..watu tukisema CCM imeoza mnafikiri tunatania.

NB:

..hivi kwanini serikali hawaidai Alex Stuart fedha za tax exemption waliyopewa na Mramba na Mgonja?
Hawawezi kudai. Wanajua ziliishia mifukoni mwa akina nani. Nasikia hata Mramba kutinga mahakamani ni kwa sababu ya kumpunja mshiko muishimiwa.
 
Hivi hawa watu watatuachia lini nchi yetu? Sasa kweli Tanzania tumekosa viongozi chipukizi mpaka tuendelee na hawa wazee ambao hawataki mabadiliko kazi ni kuendelea kutuibia kila siku.. lakini lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho sasa tusubiri utafika mwisho wa haya yote hiki kilio cha Wananchi machozi yao hayawezi kwenda bure
 
Tanzania tumelogwa!Mramba ana kesi,lakini bado yuko TANROADS!Oh my God!
Anna Mkapa na Wachaga wanachekelea
 
Back
Top Bottom