Mramba Aachie kiti Cha Ubunge!

Wakuu wote,
Respect kwa mjadala makini.

Mkuu Pundit,

Nadhani point yangu kuu inagusia suala la kutuhumiwa na kushtakiwa na jamhuri,suala la mbunge kutuhumiwa tu au kushtakiwa na jamhuri kwa kutumia madaraka yake vibaya ambayo yalitokana na sifa za yeye kuwa mbunge au kupewa dhamana baada ya kupigiwa kura na watu wazima tena wenye akili timamu ni udhalilishaji wa ofisi hiyo pamoja na wale waliomchagua.Wananchi wa Rombo wanayo haki ya kidemokrasia ya kumuadhibu katika kulind kiti cha ubunge wa jimbo hilo.

Kwanza,ni kwa misingi ipi ya kisheria na kikatiba Mramba ataweza kuwawakiklisha wananchi wake ikiwa mahakama imempiga marufuku ya kutoka nje ya jiji la Dar es salaam?



Mkuu Mkandara,

Umegonga kwenye hoja yenyewe.Uwaziri aliokua nao Mramba aliupata bada ya kuwa mbunge kama sifa mojawapo ya kumteua member wa cabinet.Leo hii bado anaendelea kuwa mbunge hata kama ni mtuhumiwa wa kuifisadi ofisi hiyo ya umma.Wananchi wa Rombo wanayo haki ya kumlazimisha ajiuzulu.Kawadhalilisha wapiga kura wake pamoja na ofisi hiyo ya ubunge wa jimbo La Rombo

Mkuu FMES,

Huyu jamaa unakumbua last CC election alipita bila kupingwa katika kura za maoni CCM.Na siri yake kubwa ni kupenyeza shilingi kwa wajumbe.Huyu jamaa inabidi abwagwe tu.Kwanza kawagawa sana warombo.gap kati ya matajiri na maskini ni kubwa mno.


Mkuu Kinyambiss,

Umesema warombo ni watu wa ku-side na mtu wao hata kama ni mwizi? Ati wao ni Warombo kwanza,pili ni wakatoliki kisha Watanzania? Hizi ni tuhuma nzito sana mbona

Nakubaliana na wewe kwamba Warombo wanahitaji sana elimu ya uraia katika lile jimo lakini hili suala la kumtetea mwizi ni no.

Pia Mramba alichofanya kule ni kujijenga yeye binafsi na kujifanya ndiye mwenye hati miliki ya lile jimbo hadi anatngaza kwamba siku atakapostaafu sisa ndipo atawaambia warombo ni mtu gani anawafaa.

Wananchi wa jimbo la rombo wanachohitaji sasa hivi ni hamasa ya mabadiliko tu
 
CHADEMA yajipanga kuchukua jimbo la Mramba



na Dixon Busagaga, Moshi




CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeanza kupanga mikakati ya ya kuhakikisha kinanyakua Jimbo la Rombo, ambalo kwa sasa linaongozwa na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Basil Mramba, anayekabiliwa na kesi ya kutumia vibaya madaraka yake.

Mramba na mwenzake, Daniel Yona, wanashtakiwa katika kesi ya jinai namba 1,200 ya mwaka huu ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7.

Akizungumza katika moja ya mikutano ya hadhara inayofanywa na mbunge wa Moshi Mjini, Philemoni Ndesamburo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Manispaa ya Moshi, Japhary Michael, alisema inajipanga kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo, wanapata mwakilishi atakayewaletea maendeleo.

Michael alisema, CHADEMA hivi sasa kinafanya mikutano ya hadhara ili kutoa mwongozo kwa wananchi wapi chama kilipo na wapi kinaelekea na hivi karibuni kampeni viongozi wa kitaifa wanaoendesha Operesheni Sangara, watatua katika jimbo hilo kuwafahamisha wananchi mustakabali wa cha taifa.

Alisema kampeni hizo zitafanyika ili kukiiimarisha chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.

“Kama chama tunajiandaa kuelekeza nguvu jimbo la Rombo…ni wazi ni miongoni mwa majimbo tutakayoyatwaa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,” alisema Michael.

“Wapinzani ambao tuliambiwa wendawazimu…ambao tumefichua ubadhirifu wa fedha za umma kwa baadhi ya viongozi wa serikali, matunda yake ndio hayo ya kufikishwa mahakamani kwa vigogo hao,” aliongeza Michael. Akizungumza kuhusu kuhamishwa kwa soko la Kiborloni, Michael alisema anasikitishwa na kitendo cha manispaa ya Moshi kubadili uwanja wa mpira wa jamhuri kuwa soko.

“Wamehamisha soko la kiborloni kwa sababu za kisiasa., wasijali wananchi wa manispaa watateseka kwa kiasi gani”alisema. CHADEMA mkoani Kilimanjaro, kinaendelea na mikutano ya hadhara ambapo hadi sasa wanachama kutoka CCM zaidi ya 800 katika kata za Majengo, Mji Mpya, Kiborloni na Rau, wamejiunga na CHADEMA.
 
Back
Top Bottom