‘Mradi wa uranium utakuwa wa manufaa’

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,110
Mwandishi Wetu, Namtumbo
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, amesema mradi wa uranium katika Mto Mkuju, wilayani Namtumbo, Ruvuma utakuwa wa manufaa makubwa kwa wananchi na taifa kwa jumla.

Amesema kwa msingi huo kuna haja kwa Watanzania kuunga mkono.Alisema dhana potofu kuwa mradi huo utakuwa na madhara kwa wananchi katika siku za baadaye, hazina ukweli kwa sababu inakosa ushahidi wa kisayansi.

Dk Bilal ambaye ni mtaalam wa Fikiziia aliyasema hayo juzo alipotembelea mradi huo akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma.

Makamu wa Rais alikuwa katika ziara ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo.
Alisema Serikali inafuatilia hatua zote muhimu za mradi huo ili kuhakikisha kuwa unakuwa na manufaa kwa nchi na watu wake.

“Tanzania ina wataalamu wa kutosha na wenye uwezo wa kufanya kazi katika masuala ya mionzi katika kuhakikisha usalama wa waajiriwa, wananchi na mazingira kwa ujumla,” alisema.

“Serikali inatarajia kufanya kazi vizuri na Kampuni ya Mantra Tanzania ili kuhakikisha kuwa mradi huu unawanufaisha pia wananchi wa Wilaya ya Namtumbo na nchi nzima kwa jumla,” alisema Dkt.Bilal
Akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Likuyu-Seka-Maganga kilichoko jirani na eneo la mradi, Dk Bilal alielezea kuridhishwa kwake kuhsu hatua za kampuni hiyo kutimiza vigezo vyote muhimu katika hatua za kuchimba madini hayo.

“Ombi langu kwenu ni kuwasihi muwashawishi vijana wenu kusoma masomo yanayohusu madini na utafiti na hususani katika maeneo ya mionzi, mazingira na madini,” alisema.Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Uranium One ya Canada inayosimamia kazi za Mantra Tanzania, John Sibley, alisema mradi utakuwa unazalisha paundi milioni 4.2 za uranium kwa mwaka.

“Utakuwa mradi wa kwanza mkubwa katika ukanda huu wa Kusini Mashariki mwa Tanzania na utaleta faida kubwa ikiwa ni pamoja na uwekezaji wa moja kwa moja wa Dola 450 milioni za Marekani,” alisema.

Dk. Bilal alipewa taarifa ya usalama, afya, na utunzaji wa mazingira baada ya kukamilka kwa shughuli ya utafiti wa mradi huo.

Chanzo. ‘Mradi wa uranium utakuwa wa manufaa’
 
Back
Top Bottom