Naona kwanza sijui inajengwa na Wachina. Maana mziki/tune inayosikika kwenye background ya movie, ni wa kichina.
Ningependa kukuunga mkono kuwa style kama hii inaleta ubaguzi na kuongeza matabaka nchini, maana inaoneka itakuwa sehemu ghali ya kuishi.
Bahari Beach project ni mradi wa IPIL, kampuni mama iko Uingereza, wa china ni Wajenzi tu sio wamiliki wa mradi.
IPIL ni real estate developer, amegundua uhaba wa nyumba uliopo DAR, na ameamua kutumia nafasi hiyo kibiashara. Hizo nyumba zitakuwa ni aghali kwa kipato cha mtanzania wa kawaida.
Pamoja na yote nashauri tuwape moyo kwani ni mradi wenye changamoto na wa kipekee hapa nchini, na tuwashauri watumie uzoefu na uwezo wao kujenga nyumba zilizo ndani ya uwezo wa kipato cha mtanzania ambao ndio wengi wasio na nyumba bora.