Mradi wa one stop border Horohoro,Wakenya wamewazidi fikira watawala wetu.

matongo manawa

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
336
79
Nimepita ktk mpaka wa Horohoro nikitokea Mombasa nikaona upande wa Kenya uko bize na ujenzi wa majengo na
nyumba za watumishi kwa kasi kubwa afisa niliyeongea naye aliusifia sana mpango huo nami nikamwelewa kweli
baada ya mradi kukamilika hakutakuwa tena na uchelewaji.

Nikaja upande wa Tanzania ndo nikachoka,tofauti na Wakenya wanaokwenda kasi,
Kwetu kuna jengo moja la ghorofa moja ambalo lina muda miezi Saba toka lianze kunengwa site ipo kama imekufa vifaa duni.

Nikapenya penya nikampata staff mmoja wa pale mpakani nikamwuliza vipi mbona
mradi wetu unasuasua wkt wenzetu wameanza juzi na inaonekana wako serious?
Jamaa akaiuliza wewe huijui Tz?kila kitu sanaa wenzetu ona akanionesha upande wa Kenya eneo lote la mpaka wanalifance kwa tofari pili ujenzi wa ofisi unaenda
sambamba na ujenzi wa nyumba za watumishi,hapa kwetu watumishi tulivunjiwa
nyumba tukaambiwa tujitafutie makazi serikali yetu haitujali.

Baada ya mazungumzo nikapanda zangu basi,
Jirani na pale mpakani sikuona nyumba za kufaa hata kupanga watumishi,nikajiuliza
wenzetu Wakenya wao wanapata wapi fikira chanya hizi?
Wenzetu wanaona mbali,hata watawala wetu wakija kukagua mradi huu hawzioni
changamoto hizi ambazo mimi mpita njia nimezibaini?
Walikaa na watumishi kabla ya mradi wakapewa mahitaji Mahususi?

Watanzania mbona tunataka kuwa nyuma kwa kila kitu?
 
bongo kila kitu ni hivyo sana..Ikulu tu imepakwa rangi miaka ya juzi juzi na kiongozi mmoja mkubwa sana wa serikali akaja na kujisifu "NA TUMEPAKA RANGI IKULU KWA HIYO WAPINZANI WATAENDELEA KUPAONA TU KWA MBAALI". so don't mind this is the TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE
 
Back
Top Bottom