Mradi wa nyumba za kupanga wa Dr. Hussein Mwinyi Dar

10billions.Kwani ni mfanyabiashara wa siku nyingi?. Usifanye mchezo na 10billion kwa mtu mmoja kuwa nazo kama si mfanyabiashara.
 
Huyu jamaa alikuwa mfanya biashara maarufu wakati baba yake akiwa raisi. Baadhi ya biashara zake zilitia ndani kuagiza mafuta (crude oil) ambayo wakati fulani shehena yake ilizua mzozo mkubwa kati ya katibu mkuu na waziri wake pale wizara ya nishati na madini, kwa kuwa hiyo crude oil ilikuwa tofauti na standard iliyokubalika pale refinery (TIPER) na huyo katibu mkuu akaikataa wakati waziri wake aking'ang'ania hiyo crude oil ipakuliwe! (sasa utashangaa kujua nani alikuwa katibu mkuu na waziri Nishati na Madini wakati huo!). Pia alikuwa na biashara ya mazao, ambayo wakati fulani ilileta kelele sana kwa kuwa kuna wakati kulikuwa na issue kwamba walikuwa waki-export mahindi kwenda nje wakati Tanzania kukiwa na uhitaji mkubwa wa chakula. Hiyo biashara ilimuuhusisha pia Mbunge wa mmoja wa kaskazini ambaye pia ni wakili maarufu.

Sasa hao ndio viongozi wetu waliokabidhiwa dhamana ya nchi!

Yaani nachoka kabisa.
 
Ndiyo maana kwa wenzetu (ukiondoa waswahili wenzetu wa Italy) mtu ukipata cheo kama hichi basi masuala ya biashara unaweka pembeni. Kama umeamua kutumikia taifa, tumikia taifa hayo ya biashara weka pembeni. Siamini kama kuna Mheshimiwa mfanyabiashara ambae ataacha kutumia nafasi yake kujifungulia milango kwenye biashara zake.Building Inspekta gani atakuwa na ubavu wa kupitia kwa makini michoro iliyobeba jina la mheshimiwa waziri? Ni waziri gani ambae ataacha kumtumia msaidizi wake kufuatilia building permit yake? Au akienda mwenyewe, kutumia gari la ofisi kufuatilia.? Au simu ya ofisini kuulizia? Yote haya ni matumizi mabaya ya nafasi yake. Akitaka kuwa developer, aachie ngazi.

Amandla........
 
Huyu jamaa alikuwa mfanya biashara maarufu wakati baba yake akiwa raisi. Baadhi ya biashara zake zilitia ndani kuagiza mafuta (crude oil) ambayo wakati fulani shehena yake ilizua mzozo mkubwa kati ya katibu mkuu na waziri wake pale wizara ya nishati na madini, kwa kuwa hiyo crude oil ilikuwa tofauti na standard iliyokubalika pale refinery (TIPER) na huyo katibu mkuu akaikataa wakati waziri wake aking'ang'ania hiyo crude oil ipakuliwe! (sasa utashangaa kujua nani alikuwa katibu mkuu na waziri Nishati na Madini wakati huo!). Pia alikuwa na biashara ya mazao, ambayo wakati fulani ilileta kelele sana kwa kuwa kuna wakati kulikuwa na issue kwamba walikuwa waki-export mahindi kwenda nje wakati Tanzania kukiwa na uhitaji mkubwa wa chakula. Hiyo biashara ilimuuhusisha pia Mbunge wa mmoja wa kaskazini ambaye pia ni wakili maarufu.

Sasa hao ndio viongozi wetu waliokabidhiwa dhamana ya nchi!

Yaani nachoka kabisa.

Syn,
Hii information muhimu sana kwangu...duh mimi niliambiwa hawa wakubwa walikuwa wanagombea mama mmoja cashier toka Mbozi pale wizarani!
 
There is no ustaarabu between Lions and men or more appropriate in this case, commonsense and nonsensical dispositions. Banning me would not solve anything, at least I speak very candidly and open heartedly about substandard threads that undermine the meaning of JF..l say we must discourage people from putting unsubstantiated, defamatory and malicious threads.. so that we can focus on nyani..

Kinyambiss, your reasoning is good, lakini lugha uliyotumia is not nice; you know you could have done better than that!
 
10billions.Kwani ni mfanyabiashara wa siku nyingi?. Usifanye mchezo na 10billion kwa mtu mmoja kuwa nazo kama si mfanyabiashara.

pcman kwa mtu mkubwa kama mtoto wa Mwinyi billion 10 ni fedha ndogo sana. Labda ungesema trillion 100 ndio ningesema ni nyingi. Naomba sana tuheshimu watoto wa maraisi wetu. Tusilete utani kwa watoto wa wakubwa. hata Mungu analijua hilo.
 
Naamini kunatofauti kubwa ya mtu ambaye amepata hela na utajiri kwa njia halali na yule ambaye amepata utajiri kwa njia haramu kama ufisadi. Although its wrong to conclude that Dr Mwinyi ni fisadi without evidence, but its our respeonsibilities and rights as citizen to ask where did he get money to be able to invest on that 10bil TZSH project at this period of recession? ... if he is a shareholder and he has other investment then why does he use his own name for the project? To me by using his own name, ni dalili ya kwamba anamiliki share kuba kuliko wote kama ni partnership investment (that is my thought)
 
pcman kwa mtu mkubwa kama mtoto wa Mwinyi billion 10 ni fedha ndogo sana. Labda ungesema trillion 100 ndio ningesema ni nyingi. Naomba sana tuheshimu watoto wa maraisi wetu. Tusilete utani kwa watoto wa wakubwa. hata Mungu analijua hilo.

Ohh dear are you f..... joking? Kwa hiyo kama mtoto ni warais we all have to bow our head for him? Swali nililonalo kwako... je rais ni mtu mmoja au ni familia yake nzima?
 
Naona unanichanganya na ma corporate lawyers sasa.

Wewe umesema mtaji batili, nakuuliza batili kivipi na wewe unanijibu kwa swali "alipata kwa njia halali?" . Burden of proof iko kwako wewe accuser.Toa data, sio unadandia magari tu.
ndugu yangu unataka data gani? huko nyuma nimeelezea mfano ulikuwepo na kuandikwa kwenye magazeti kuhusu ilipokuwa ofisi za zambia airways, na kuchukuliwa na familia ya kwanza, kuna deal nyingi tu mpaka za kuna shirika moja la ndege liliingia bongo likaishia kimya kimya sikumbuki jina vizuri macsoms? , haya hilo jengo lilikuwa la nhc/kiwanja sasa wewe ulisikia lini hicho kiwanja/myumba inauzwa mpaka useme kilipatikana kihalali? je unajua kuna viwanja vingapi vya wazi vilibadilishwa matumizi yake, kwa ajili ya familia ya kwanza, na ufisadi mwingine, mpaka road reserve maeneo ya kurasini ilifanywa kiwanja na watu walijenga karibu na rtc club au kurasini centre kule kwa wakatoliki ( mkabala ma Barabara ya Mandela. wewe kama una mtu wako nhc muulizie watakupa nyingi tu, madeal ya namna hiyo mpaka wengine walipata nyumba za tpdc upanga , sasa bado yale ya nyuma ya pazia ambayo wengi wetu hatu ya jui.
 
Sasa ufisadi ukowapi?? Hii heading ni defamatory kwasababu hakuna ushahidi.. infact hakuna ata accusation ya maana.. Kujenga apartment ndio ufisadi??? Au kufanya project ya 10million dollars ndio ufisadi? Kwanini alieleta thread hajaongelea funding jamaa katoka wapi..ameconclude kabla hajatoa ushahidi wowote ata theoretical..lol That is too weak and too speculative ndio maana inakera watu wakiandika vitu vya hovyo namna hii. I'm just saying.


hussein mwinyi sio mfanyabiashara mkubwa na hajafikia kuwa mfanyabiashara mkubwa.
kwa TZ huwezi kupewa mkopo wa $10m kama wewe sio mfanyabiashara mkubwa. watu wanaoweza kupata mikopo ya $10m bank hawawezi kufika wa 5 TZ.
bak na nyangumi walikuwa wanataka mikopo ya more than $10m iliwabidi waende IFC kukopa.

kinyambiss je una knowledge yeyote juu ya mikopo inavyokwenda, huwezi tu ukapewa $10m bila kuwa na history ya biashara.
pili benki za TZ hazitoi mikopo ya $10m kwa mtu mmoja kwa ajili wanaogopa default.
ladba awe amepewa na NSSF kama mkapa alivyopewa 17bil na hajarudisha mpaka leo

voda ni kampuni kubwa lakini banki zote za TZ zimeshindwa ku raise $150m, wame raise only $90m loan kwa ajili wanaogopa default.
 
Kiwanja kilikuwa cha NHC na sidhani kabla ya utaifishaji wa 1967 babayake alimiliki jengo hapo Seaview

...ok, kilikuwa cha NHC kisha 'wakagawana' au?...


Posted Date::4/22/2008
Rudisheni nyumba zote za serikali
Na Prof. Abdallah J. Saffari
Mwananchi

Makala hiyo inaelezwa kuwa baada ya kujichukulia nyumba ya serikali iliyopo Sea View, Upanga, Dar es Salaam Rais mstaafu Mkapa aliwaruhusu wenzake wachukue nyumba walizokuwa wanakaa kuficha dhuluma hiyo. Nyumba nyingine zilikarabatiwa kwa mamilioni kabla ya kuuzwa kwa bei poa. Rais Kikwete naye akaambulia yake Mtaa wa Ursino, Ada Estate, Dar es Salaam ambayo hadi sasa hajairejesha serikalini.

source; https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/12516-rudisheni-nyumba-zote-za-serikali-2.html
 
...well said!

na ikithibitika alikipata kiwanja kwa njia halali Mheshimiwa huyu ataombwa radhi? Haikuwa ajabu enzi za Mwalimu waheshimiwa kujenga mitaa ya Seaview, na huenda ameachiwa urithi na wazee wake.

Hakuna ajabu yeyote Dr. Mwinyi kuingia ubia na wawekezaji fulani kujenga apartments Blocks.

Mfano; Maeneo mengi ya Upanga utakuta hizo Blocks zenye majina ya 'Clients' ambao ni watoto/wajukuu wa wazee waliokuwa wanamiliki hizo plots miaka ya 70's... ambazo wengi wao wameingia mikataba yaku-lease plots zao kwa wawekezaji.
sio ukweli
nimekaa mtaa wa mindu for more than 15 years na maghorofa yote unayoyaona mindu ni watu wameuza viwanja, hamna hata mtu mmoja wa zamani. hali iko hivyo kwenye mitaa mingine ya upanga
 
Au kufanya project ya 10million dollars ndio ufisadi?

Kwa Mtanzania kufanya project ya $10 millioni si ufisadi, lakini huyu mtoto wa Mwinyi tunamfahamu hakutoka katika familia yenye pesa kiasi hicho na hata yeye mwenyewe hana biashara yoyote ya kumuwezesha kuanzisha mradi wa kiasi hicho na mshahara wake wa uDR na pia ubunge, Waziri mdogo na sasa Waziri kamili sidhani kama unaweza kumpa uwezo wa kufanya mradi mkubwa kiasi hicho. Kama yuko na mapartners wengine katika mradi huo, je ni akina nani hao? Kumbuka juzi juzi tu huyu mtoto wa mwinyi ndiye aliyetoa zabuni kwa fisadi Jeetu patel ya kuleta matrekta ya Kilimo Kwanza pia inasemekana alishiriki kwa karibu katika ufisadi wa kuleta magari ya kijeshi.

Hivyo maswali yanayoulizwa na Watanzania kuhusu wapi pesa hizo zimepatikana ni maswali muhimu hasa ukitilia maanani miaka ya karibuni tumeona viongozi mbali mbali wa juu kuanzia Rais Mkapa, Mawaziri Mramba, Yona, Karamagi, na hata Wabunge wameshiriki katika ufisadi. Usikute kama ni ubia basi wabia wenbzake ni hao akina Jeetu, Manji, Subhash Patel na mapapa wengine wa ufisadi. Kama kuna wabia badsi majina yao yawekwe hadharani na vyabzo vya pesa hizo pia viwekwe hadharani.

Pia sidhani kama Watanzania hawapendi kuwaona Watanzania wenzao wakiwa matajiri bali wanapenda utajiri huo uwe umepatikana kihalali badala ya kufanya ufisadi katika pesa za walalahoi kama vile ufisadi katika ununuzi wa Rada, mkataba wa Richmond/Dowans, Mkataba wa Kilimo Kwanza, Ununuzi wa ndege ya Rais, EPA etc.
 
sio ukweli
nimekaa mtaa wa mindu for more than 15 years na maghorofa yote unayoyaona mindu ni watu wameuza viwanja, hamna hata mtu mmoja wa zamani. hali iko hivyo kwenye mitaa mingine ya upanga

...dah, haya bana.

mfano wa kwanza; Pale pembeni ya Ubalozi wa Libya (Mtaa wa Mtitu), kuna Ghorofa linajengwa kwa ajili ya Apartments. Lina ghorofa saba tayari. Umesoma jina la Clients?
 
...dah, haya bana.

mfano wa kwanza; Pale pembeni ya Ubalozi wa Libya (Mtaa wa Mtitu), kuna Ghorofa linajengwa kwa ajili ya Apartments. Lina ghorofa saba tayari. Umesoma jina la Clients?

Mkuu Mbu, mimi wasiwasi wangu katika haya maghorofa yanayoibuka kama uyoga ni kuhusu drainage system. Je nazo zinaongezwa ili kukidhi mahitaji makubwa ya ongezeko la watu katika maeneo mbali mbali ya Jiji au bado ni zile zile za mwaka 47!? Kama haziongezwi basi baada ya miaka michache maeneo mengi kama ya Upanga, Oysterbay etc na kwingineko ambapo sasa hivi hakuna tatizo la maji machafu hali itabadilka na maeneo haya kuharibika sana kutokana na mafuriko ya maji machafu.
 
Back
Top Bottom