Mradi wa mabasi yaendayo kasi

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,358
6,422
Wapendwa tunaomba anaye fahamu mradi huo utapita njia/sehemu gani za Dar atuhabarishe. Naona wanabomoa gerezani, hiyo barabara itapita wapi kuja mpaka gerezani. Kuuliza si ujinga.
 
Me sijui,ila barabara inaonesha itapita maeneo ya USWAHILINI
SABABU:ALWAYS WANABOMOA MAENEO YA USWAZ,cjasikia kama kuna eneo huko masak limevunjwa coz of this,
 
Me sijui,ila barabara inaonesha itapita maeneo ya USWAHILINI
SABABU:ALWAYS WANABOMOA MAENEO YA USWAZ,cjasikia kama kuna eneo huko masak limevunjwa coz of this,

Salute kwako!

Naomba kukusaidia kufikiria nje ya box. Siku zote usipende kujidharau kwani kuwa maeneo ya uswahilini ndiko kunakohitaji msaada wa maendeleo. Mradi wa DART kwenye awamu ya kwanza utapita katika barabara ya Morogoro, Kawawa, Msimbazi, Sokoine na Kivukoni.

Lengo kuu la mradi ni kuboresha usafiri wa umma. Huko masaki demand ya usafiriwa umma ni ndogo. Uswazi ndiko kunahitaji usafiri. Na kama nimekuelewa vizuri, shida kubwa huko uswazi ni kuwa hakujapangika na sasa kunahitaji kupangika na ndio sababu kuu za kuvunja maeneo hayo.

Kituo kikuu cha Gerezani ndio hub ya mradi mzima wa DART katika jiji letu. Eneo hilo lililengwa kwa kuwa ndio mahali ambapo watu kutoka maeneo yote ya Jiji wataweza kufikia katikati ya Jiji.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom