Mradi wa mabasi ya wanafunzi wazinduliwa Dar

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Mradi wa mabasi ya wanafunzi wazinduliwa Dar

Na Stella Nyemenohi, Habari Leo

HUENDA ile adha ya siku nyingi ya wanafunzi kunyanyaswa na daladala mjini ikapungua kama si kutoweka, baada ya kuzinduliwa mradi wa mabasi ya kuwasafirisha.

Uzinduzi wa mabasi hayo umefanywa jana Dar es Salaam na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kwa Shirika la Usafiri la Dar es Salaam (Uda) kuhadharishwa mradi usifie mikononi mwake.

Mradi huo ambao unatarajiwa kuanza wiki ijayo, umetokana na msaada wa magari matano yenye thamani ya Sh milioni 500 wa benki ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wa Dar es Salaam.

Waziri Mkuu alitangaza kwamba Serikali iko tayari kuwaondolea ushuru watu binafsi, kampuni na mashirika watakaoguswa na kununua mabasi kwa ajili ya mradi huo uliokabidhiwa Uda kwa mkataba na utaratibu maalumu wa uendeshaji.

"Hatutakubali kuona mradi uliozinduliwa leo ukifa au ukapotea kimaajabu tu," alisema Pinda. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uda, Martin Milanzi, magari hayo yatatoa huduma kwa njia za Kariakoo-Tegeta, Chanika-Kariakoo na Kariakoo-Mbezi Shamba kwa nauli ya Sh 100 kwa mwanafunzi.

Kulingana na idadi ya wanafunzi zaidi ya 500 jijini Dar es Salaam, asilimia 1.8 ndiyo imetajwa na Waziri Mkuu kuwa watafaidika na mabasi hayo matano.

Takwimu zilizowahi kutolewa zinaonesha Dar es Salaam yenye wanafunzi zaidi ya 500 inahitaji zaidi ya mabasi 10,000 ya kawaida, kubeba idadi hiyo ya wanafunzi kila siku asubuhi wanapokwenda shuleni na jioni wanaporudi.

"Tunahitaji mabasi mengi zaidi ya kubeba wanafunzi wengi zaidi. Kwa mfano, kama tuna wanafunzi 550,000 wanaohitaji usafiri kila siku, tunahitaji mabasi takribani 275 yanayobeba abiria 100 na yatakayofanya safari 20 kila moja na kila siku ya shule ili kuondokana na tatizo hili," alisema Pinda.

Hata hivyo, kutokana na msongamano ambao Waziri Mkuu alisema umeshakuwa gumzo si tu nchini bali pia wageni wanaotembelea nchi, ni vigumu mabasi hayo kumudu safari 20 na kuwahisha wanafunzi shuleni au nyumbani.

Akiisisitiza Uda kuhakikisha kuwa mradi unakuwa endelevu, Pinda alisema, "tatizo litakalojitokeza ni pale ambapo baada ya muda mfupi, mabasi yale hayaonekani barabarani kama ilivyokuwa Chai Maharage… kesho jukumu hili muhimu la kuwapatia wanafunzi usafiri linadorora na mabasi hayaonekani tena, kwetu sote tuliopo hapa na tunaoshuhudia itakuwa fedheha na aibu kwa watoto wetu.

"Tujitahidi kuonesha watoto kuwa tunabuni mambo yanayowezekana. Kampuni mbalimbali zione jambo hili ni letu sote. Basi moja ni Sh milioni 100 na ushuru, bila ushuru ni Sh milioni 75.

Hili la kuondoa ushuru mabasi yapatikane linawezekana," alisema Pinda na kumwelekeza Mkuu wa Mkoa, William Lukuvi, wakae kuangalia namna ya kutoa msukumo kwa wengine kuchangia.

Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam zilitakiwa kuona wajibu wa kuiwezesha Uda ijiimarishe kutatua kero ya usafiri kwa wanafunzi.

Kauli ya Pinda kuisisitiza Uda kuwa makini inatokana na uzoefu uliojitokeza katika mradi mwingine wa usafirishaji uliobuniwa takribani miaka 20 iliyopita lakini ukafa.

Mradi huo ambao pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Lukuvi aliyekuwa miongoni mwa waasisi wake, aliutumia kuisisitiza Uda kuwa ikiwa na usimamizi mzuri wa mabasi hayo matano, haiwezi kupata hasara na hatimaye mradi kufa kama ilivyokuwa kwenye mradi wao.

"Miaka 20 iliyopita, nilianzisha mradi kama huu. Tukaomba tukapata basi moja, tulipata Sh milioni 40 tukanunua mabasi matano, tena tukanunua Chai Maharage sita, tukatengeneza faida … baada ya hapo nilipandishwa cheo nikaondoka kwenda mikoani, niliporudi mwaka 1995 nikakuta mradi umekufa jamaa wamegawana mbao," alisema Lukuvi.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema benki yake imekuwa ikiguswa na kero zinazowakabili wanafunzi kupoteza muda mwingi kusubiri usafiri hali inayowaathiri kisaikolojia na wengine, hususan wasichana, kujiingiza kwenye vishawishi vya ngono.

Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na wanafunzi kutoka baadhi ya shule za Dar es Salaam, viongozi na watendaji akiwamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Adam Kimbisa, Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Israel Sekirasa.

My take: Mradi kama huu, in early 1990s ulianzishwa na augustne Mrema alipokuwa Home Affairs minister na kukabidhiwa UVCCM kuu-run, na baadaye waliutafuna. Nadhani akina Nchimbi hawa, kama sijakosea.
 
Ukisimamiwa vizuri utasaidia kuondoa kero za usafiri kwa wanafunzi Dar. Pia ni vizuri na wanafunzi wa mikoani hasa mikoa iliyo na kero za usafiri wa wanafunzi kama Dar nao wangefikiria utaratibu kama huu!
 
Mradi wa mabasi ya wanafunzi wazinduliwa Dar

Na Stella Nyemenohi, Habari Leo

HUENDA ile adha ya siku nyingi ya wanafunzi kunyanyaswa na daladala mjini ikapungua kama si kutoweka, baada ya kuzinduliwa mradi wa mabasi ya kuwasafirisha.

Uzinduzi wa mabasi hayo umefanywa jana Dar es Salaam na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kwa Shirika la Usafiri la Dar es Salaam (Uda) kuhadharishwa mradi usifie mikononi mwake.

Mradi huo ambao unatarajiwa kuanza wiki ijayo, umetokana na msaada wa magari matano yenye thamani ya Sh milioni 500 wa benki ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wa Dar es Salaam.

Waziri Mkuu alitangaza kwamba Serikali iko tayari kuwaondolea ushuru watu binafsi, kampuni na mashirika watakaoguswa na kununua mabasi kwa ajili ya mradi huo uliokabidhiwa Uda kwa mkataba na utaratibu maalumu wa uendeshaji.

“Hatutakubali kuona mradi uliozinduliwa leo ukifa au ukapotea kimaajabu tu,” alisema Pinda. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uda, Martin Milanzi, magari hayo yatatoa huduma kwa njia za Kariakoo-Tegeta, Chanika-Kariakoo na Kariakoo-Mbezi Shamba kwa nauli ya Sh 100 kwa mwanafunzi.

Kulingana na idadi ya wanafunzi zaidi ya 500 jijini Dar es Salaam, asilimia 1.8 ndiyo imetajwa na Waziri Mkuu kuwa watafaidika na mabasi hayo matano.

Takwimu zilizowahi kutolewa zinaonesha Dar es Salaam yenye wanafunzi zaidi ya 500 inahitaji zaidi ya mabasi 10,000 ya kawaida, kubeba idadi hiyo ya wanafunzi kila siku asubuhi wanapokwenda shuleni na jioni wanaporudi.

“Tunahitaji mabasi mengi zaidi ya kubeba wanafunzi wengi zaidi. Kwa mfano, kama tuna wanafunzi 550,000 wanaohitaji usafiri kila siku, tunahitaji mabasi takribani 275 yanayobeba abiria 100 na yatakayofanya safari 20 kila moja na kila siku ya shule ili kuondokana na tatizo hili,” alisema Pinda.

Hata hivyo, kutokana na msongamano ambao Waziri Mkuu alisema umeshakuwa gumzo si tu nchini bali pia wageni wanaotembelea nchi, ni vigumu mabasi hayo kumudu safari 20 na kuwahisha wanafunzi shuleni au nyumbani.

Akiisisitiza Uda kuhakikisha kuwa mradi unakuwa endelevu, Pinda alisema, “tatizo litakalojitokeza ni pale ambapo baada ya muda mfupi, mabasi yale hayaonekani barabarani kama ilivyokuwa Chai Maharage… kesho jukumu hili muhimu la kuwapatia wanafunzi usafiri linadorora na mabasi hayaonekani tena, kwetu sote tuliopo hapa na tunaoshuhudia itakuwa fedheha na aibu kwa watoto wetu.

“Tujitahidi kuonesha watoto kuwa tunabuni mambo yanayowezekana. Kampuni mbalimbali zione jambo hili ni letu sote. Basi moja ni Sh milioni 100 na ushuru, bila ushuru ni Sh milioni 75.

Hili la kuondoa ushuru mabasi yapatikane linawezekana,” alisema Pinda na kumwelekeza Mkuu wa Mkoa, William Lukuvi, wakae kuangalia namna ya kutoa msukumo kwa wengine kuchangia.

Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam zilitakiwa kuona wajibu wa kuiwezesha Uda ijiimarishe kutatua kero ya usafiri kwa wanafunzi.

Kauli ya Pinda kuisisitiza Uda kuwa makini inatokana na uzoefu uliojitokeza katika mradi mwingine wa usafirishaji uliobuniwa takribani miaka 20 iliyopita lakini ukafa.

Mradi huo ambao pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Lukuvi aliyekuwa miongoni mwa waasisi wake, aliutumia kuisisitiza Uda kuwa ikiwa na usimamizi mzuri wa mabasi hayo matano, haiwezi kupata hasara na hatimaye mradi kufa kama ilivyokuwa kwenye mradi wao.

“Miaka 20 iliyopita, nilianzisha mradi kama huu. Tukaomba tukapata basi moja, tulipata Sh milioni 40 tukanunua mabasi matano, tena tukanunua Chai Maharage sita, tukatengeneza faida … baada ya hapo nilipandishwa cheo nikaondoka kwenda mikoani, niliporudi mwaka 1995 nikakuta mradi umekufa jamaa wamegawana mbao,” alisema Lukuvi.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema benki yake imekuwa ikiguswa na kero zinazowakabili wanafunzi kupoteza muda mwingi kusubiri usafiri hali inayowaathiri kisaikolojia na wengine, hususan wasichana, kujiingiza kwenye vishawishi vya ngono.

Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na wanafunzi kutoka baadhi ya shule za Dar es Salaam, viongozi na watendaji akiwamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Adam Kimbisa, Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Israel Sekirasa.

My take: Mradi kama huu, in early 1990s ulianzishwa na augustne Mrema alipokuwa Home Affairs minister na kukabidhiwa UVCCM kuu-run, na baadaye waliutafuna. Nadhani akina Nchimbi hawa, kama sijakosea.

Wenye kumbukumbu naomba mtusaidie. Hivi Mkuu wa Kaya, hakuweko kule UVCCM wakati ule wa utafunaji wa mradi?
 
Kipindi hiki cha kampeni mpaka tufike kwenye uchaguzi, tutasikia mambo mengi sana. Mi yangu macho.
 
Nimeona picha ya Mkuu wa Mkoa wa DSM wakati wa makabidhiano, nikakumbuka yale mabasi yetu ya TATA!
 
Back
Top Bottom