Mradi wa Digital Broadcasting TBC

Nimemsikia Tido akiuelezea huu mradi katika kipindi cha Pongezi za mwaka mpya kilicho rushwa na Radio yao na aliielezea kuwa unategemewa kuanza majaribio katika mwezi huu wa January kwa Mkoa wa Dar kwa kuanzia na wale wanaohitaji watatakiwa kuwa na Decoder na alisema kwa kuanzia itakuwa na channel zisizopungua 40 ila alifafanua na kusema kuwa inategemewa kuwa na channel kama 200 hivi ambazo zitalipiwa kwa bei nafuu. ukilinganisha na DSTV.

...Mkuu Firdous, Una taarifa yoyote kama hii kitu imeishaanza ili tujimwage?? Nahofia isije ikawekewa Zengwe na jamaa wa nanihii ikaishia kwenye makabrasha! Bongo hii Tunaijua.
 
Babadesi

Alichosema Tiddo ni kuwa itaanza katika mwezi huu wa January kwa kuanzia katika Jiji la Dar. Sina Uhakika ni tarehe gani na kama imeshaanza tayari lakini nafikiri ikiwa tayari watatutangazia. keep waiting
 
wanasema wataanza mwezi huu. wamefungua duka kariakoo karibu na supermarkert ya imalaseko. contact zao 0767 000705/ 0767 000706.
wanasema watakuwa na channel zaidi ya 30 kwa kuanzia.
 
Kabla ya kwenda huko kote, TBC wangeanza kwanza na kurekebisha mitambo yao ya sauti au wale mafundi mitambo wa sauti wawajibike au wapige msasa ujuzi.

Yaani ikifika wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku mpaka inakuwa kero. Sauti mara ipande yenyewe mara ishuke bila ya mpangilio.
Na ikifika wasaa wa habari za uchumi na biashara yule bwana mdogo Stanley inakuwa kama vile anaongea lugha ya kigeni na kisha kufanyiwa dubbing. Mienendo ya midomo yake na matamshi ya maneno hata haviwiani.

Inakera
 
Mimi sina wasiwasi na kuanza kwa digital, tena tutakuwa tumepiga hatua sana; Ila shida iko kwenye content tu, kama wana 65% inamaana wako na uwezo mkubwa wa kudecide what to broadcast na mwisho wa siku tutakuwa tunalishwa mambo ya wachina na kizazi kijacho kitakuwa hakijui tena issue za kwetu hususani utamaduni wetu
 
Hivi jamani Star TV na TBC wamepata license ya digital broadcasting kweli?
 
Mimi sijauelewa bado ila ninayo decoder yake na ni nzuri tu japo ina channel nyingi zisizo na maana, na chache ninazozipenda, zinanitosha sana, ila inabidi wafanyie kazi foleni ya kulipia kwani kila mtu atakuwa na yake, bora waweke electronic mode ya kulipia
 
Haika, hebu tupe kwa undani kidogo. Decoder umenunua wapi? bei gani? unapata channel ngapi jumla? kwa jinsi ulivyoona, ni zipi ni nzuri??

Kabla ya kwenda huko kote, TBC wangeanza kwanza na kurekebisha mitambo yao ya sauti au wale mafundi mitambo wa sauti wawajibike au wapige msasa ujuzi.

Yaani ikifika wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku mpaka inakuwa kero. Sauti mara ipande yenyewe mara ishuke bila ya mpangilio.
Na ikifika wasaa wa habari za uchumi na biashara yule bwana mdogo Stanley inakuwa kama vile anaongea lugha ya kigeni na kisha kufanyiwa dubbing. Mienendo ya midomo yake na matamshi ya maneno hata haviwiani.

Inakera

Upo sahihi kabisa sijui TBC hawalioni hilo tena lipo kila siku na kila mara naomba wawajibike mbona vitu vingine mmejitahidi sana?
 
channel za asia hazina mvuto wowote zaidi ya tamthilia na madhehebu mengi ya mashariki ya mbali yasiyo na imani inayoelewekaeleweka vizuri. hata ukiangalia taarifa za habari. wao na hiyo channel ya wasomi yaani habari za nje wao wanaona ziko CCTV ya China na Urusi tu? huu ni ufinyu wa mawazo sana.
 
Superman,
Kosa ni kuwapa Wachina 65% ownership ya TBC na sisi kubaki na 35%. Huwezi tena kuiita hiyo Tanzania Broadcasting Corporation . Ni China Broadcasting Corporation.
Hizo gharama za digital tungeweza kuzimudu sisi wenyewe, ila siku hizi Tanzania mindset ya viongozi wetu ni kwamba "No we can't. Only foreigners can."

Hapo kwenye red; where is the supporting info; unao huo mkataba ama kama kuna wadau wanaweza kuupata watuletee.
 
Kwa hiyo dar mnapata hizo channel 30? Mbona hawa jamaa wa DSTV na wengine wa cables watakoma!

Wewee thubutu yake; Usidanganyike umeona list ya Channel za kichovu za hawa jamaa mpaka uje na hiyo conclusion; believe me DSTV subcribers wataongeza tu hiyo decorder na kwa uchache lakini usitegemee watu kuhama; kama unazo data uliza wakati GTV wanaingia hapa wangapi tulihama DSTV?

Unless wajipange upya! lakini sio kwa style waliyonayo sasa; ningewaona wa maana kama wangejumuisha local broadcasters wote na redio zao at least ningesema wana kitu lakini maawe! wametujazia channel kibao za ASia!:yuck:
 
zinapatikana, soma michuzi nimeona maelezo kiasi, kwa ufupi wewe kama ni mtu wa kawaida unafanya kazi masaa ya kawaida, basi ni bora kulipa 9000 kwa mwezi kuliko kulipa minimum ya DSTV kwa sasa, labda mabo yabadilike,
mie niweka pending kwanza kulipia dstv yangu, watoto wanaipenda kwani channel zao za watoto ni nzuri (kwangu) kuliko zilizokuwapo DSTV ($30,000)
All in all wana safari ndefu ya kwenda kabla hawajawa competition kwa yeyote yule. Advantage yao ni wamejificha nyuma ya serikali yetu inayochagua makampuni binafsi kuyabeba mpaka yaweze kutemmbea.
Mie sikudhani kama hili ni mojawapo ya priorities ambazo serikapi yetu tukufu ingejiingiza humo, lakini naendelea kushangaa na kushangazwa!!!

Tanzania!!
I cant you!!
is there a place where a group of people sit and look at the whole picture? get it in their heads and set priprorities? hata sidhani,
 
Haika, hebu tupe kwa undani kidogo. Decoder umenunua wapi? bei gani? unapata channel ngapi jumla? kwa jinsi ulivyoona, ni zipi ni nzuri??

Hizo decoder zinatembezwa maofisini nafikiri hata ukienda pale TBC mikocheni zipo.Bei yake ni elfu 70,000 na kulipia channel elfu 9000/= kwa mwezi.
channel wanazogawa ni 30 lakini nyingi zina kwikwi,hivyo zinazoonekana vizuri ni kama 15.
Channel nzuri ni bbc,aljazera,tbc,channel ten,tbn,citizen,bet,setanta,na stve
 
... Jamani huko juu mbona wengine mnaponda?? kama TBC yetu ina channel alizotaja Charity kama BBC, AlJaazera, Channel 10, Citizen (kenya), Setanta (sports) na kadhalika nadhani kwa shs alfu 9 tu sio mbaya kiasi hicho! Ndio Mwanzo. labda niulize tu kama kuna channel yenye Sitcoms kama ile iliyowahi kuwa ITV ya EBN ambayo sijui iliishia wapi iliyokuwa na Sitcoms kama The Parkers, Everybody Loves Raymond, Daimon nakadhalika! Halafu huu ushamba nao, jamani nauliza msinicheke. Hivi hii Decorder unaweza kuifunga mwenyewe bila kulazimika kutafuta fundi na haina haja ya Dishi la nje????
 
Back
Top Bottom