Mradi wa Digital Broadcasting TBC

naomba kujuzwa kidogo hivi ikishakuwa digital inamaana atutatumia tena antena za kawaida watasaplay decoder au sijaelewa jamani

Utaendelea kutumia antena kama zamani. Tofauti kwenye digital picha inaonekana vizuri zaidi na ukiweza kama mpunga unaruhusu unaongeza Digital box ambako makampuni mengi huweka bundles kama vile za channel za sport, adult films, na hub ya fast broadband internet. Vile vile unakuwa na chance ya ku-rewind programme unayoangalia au kurecord any two programmes kwenye channel tofauti at the same time. Au ukachagua programme tofauti tofauti kutokana na chaguo lako. Ukiweka Digital box huna haja ya Aerial.

Kwa UK mfano ukiwanayo unaweza kuona michezo mingi Live kwenye Skysport 1, 2, 3 and 4 pamoja na vikolombwezo kibao ambavyo kwa mwezi utalipa kama £60. Kwa Tanzania inategemea. Digital zilianza kuuzwa UK wakati wa karibu na fainali za World Cup kule Japan na Korea na wakati huo zilikuwa zinauzwa kama £1000.00 na ushee. Hivi sasa bei ni poa sana utapata digital kuanzia £150 inategemea na model.
 
NB. Analogue TV kwa Uk zitaacha kufanya kazi sikumbuki ni lini lakini hilo linatokana na BBC kuacha kutangaza kwa kutumia analogue wakati ukifika. Nchi nyingine zitaamua kutokana na mifuko yao how long wataendelea kutumia analogue. Kama Broadcaster ataendelea kutumia analogue utaendelea kupata mawasiliano Sifahamu kama Tanzania wameweka time table lakini usisahau BBC wanakua sponsored heavily na kodi wanayotoza kwa waangaliaji kila household wanalipa £136 kwa mwaka.

Watakapoacha huwezi kuwapata hasa kwenye nchi zetu ambako kila mtu anafikiria BBC ndio wenye ukweli wote. Khe khe khe.
 
Lakini kulikuwa na ulazima gani wa kuwapa 65%? 45% zingewatosha.
Ndugu yangu Jasusi, usihofu na hiyo 65%, its not of TBC, its of Star Media Corp. A total private entity. TBC is still 100% gvt of Tz. But that TBC has 35% stakes on a newly established subsidiary. The reason is simple Investment. Kama serikali imeshindwa kumalizia jengo la TBC for 10years now.!, itakuwa digital transmiters?.
 
Lakini kulikuwa na ulazima gani wa kuwapa 65%? 45% zingewatosha.
. Its true hizo zingewatosha. Hata 10% only was enough. Are we capable of the remaining 90% investment?. Kwani ni nini kinatufanya tushindwe kuchimba madini yetu na kuretain 100%?. Its only capital. Kama tunawapa Barrick 99.07% na sisi kuretain 0.03% royatily, whats a big deal about 35% stakes?.
 
Ndugu yangu Jasusi, usihofu na hiyo 65%, its not of TBC, its of Star Media Corp. A total private entity. TBC is still 100% gvt of Tz. But that TBC has 35% stakes on a newly established subsidiary. The reason is simple Investment. Kama serikali imeshindwa kumalizia jengo la TBC for 10years now.!, itakuwa digital transmiters?.

hapana hiyo ni National TV siyo Star TV ya Mwanza. Star Digital ndiyo kampuni ya nje itakayochukua hizo 65% na kutuachia 45%
 
Watz bado tuko gizani kuhusu digital conversion. Sio TBC wala TCRA iliyowaelimisic Jamii what does it mean. Kwa wenye DSTV wameonja. More than 100 channels with a single decoder!.
 
Utaendelea kutumia antena kama zamani. Tofauti kwenye digital picha inaonekana vizuri zaidi na ukiweza kama mpunga unaruhusu unaongeza Digital box ambako makampuni mengi huweka bundles kama vile za channel za sport, adult films, na hub ya fast broadband internet. Vile vile unakuwa na chance ya ku-rewind programme unayoangalia au kurecord any two programmes kwenye channel tofauti at the same time. Au ukachagua programme tofauti tofauti kutokana na chaguo lako. Ukiweka Digital box huna haja ya Aerial.

Kwa UK mfano ukiwanayo unaweza kuona michezo mingi Live kwenye Skysport 1, 2, 3 and 4 pamoja na vikolombwezo kibao ambavyo kwa mwezi utalipa kama £60. Kwa Tanzania inategemea. Digital zilianza kuuzwa UK wakati wa karibu na fainali za World Cup kule Japan na Korea na wakati huo zilikuwa zinauzwa kama £1000.00 na ushee. Hivi sasa bei ni poa sana utapata digital kuanzia £150 inategemea na model.

Angalia hiyo rangi nyekundu, ukweli ni kwamba Antena za zamani (analog) haziwezi kushika digital broadcasting, hivyo basi punde watakapoanza kutangaza kwa digital signals itakulazimu kununua antenna nyingine. Hapa USA walioathirika zaidi ni wale wasio na cableTV. Cable campany zinaconvert digital kuwa analog then huhitaji antenna or converter box. Lakini kwa wale wasio na Cable iliwalazimu kununua antenna/converter zingine.
 
Mkuu;

TBC Wameungana na Wachina kuunda kampuni ya
Star Media (Tanzania) Ltd.

Kampuni hii haihusiki na CONTENT kama TBC, bali inahusika na construction ya Digital Broadcasting Facilities.

Hata hivyo nimepata dondoo mahali kuwa hawa Wachina wataleta pia channels nyingine ambazo zitakuwa na content toka nje under Star Media na sito TBC.

Mkuu

Unachokisema hapa wewe ni kuwa hao Wachina watakuwa wanamiliki 65% ya Digital TV Infrastructure ya Tanzania...na TBC wao watakuwa wanamiliki 35%.

Pia, kama nimekuelewa ni kuwa TBC wao watakuwa wanajihusisha na Contents. Wakati huo huo hawa Wachina kwa mujibu wa "dondoo" na pia wataruhusiwa kufanya biashara ya Contents wakishindana na TBC na other local companies.

Sasa mkuu hapo huoni kuwa tumeshafanya makosa...mimi naona Infrastructure ni muhimu zaidi...tungemiliki sisi hiyo 65% na Wachina 35%. Tutawezaje kuwa na sauti kwenye Contents wakati ambapo Infrastructure inamilikiwa na mtu mwingine.???
 
nb. Analogue tv kwa uk zitaacha kufanya kazi sikumbuki ni lini lakini hilo linatokana na bbc kuacha kutangaza kwa kutumia analogue wakati ukifika. Nchi nyingine zitaamua kutokana na mifuko yao how long wataendelea kutumia analogue. Kama broadcaster ataendelea kutumia analogue utaendelea kupata mawasiliano sifahamu kama tanzania wameweka time table lakini usisahau bbc wanakua sponsored heavily na kodi wanayotoza kwa waangaliaji kila household wanalipa £136 kwa mwaka.

Watakapoacha huwezi kuwapata hasa kwenye nchi zetu ambako kila mtu anafikiria bbc ndio wenye ukweli wote. Khe khe khe.

2012
 
Angalia hiyo rangi nyekundu, ukweli ni kwamba Antena za zamani (analog) haziwezi kushika digital broadcasting, hivyo basi punde watakapoanza kutangaza kwa digital signals itakulazimu kununua antenna nyingine. Hapa USA walioathirika zaidi ni wale wasio na cableTV. Cable campany zinaconvert digital kuwa analog then huhitaji antenna or converter box. Lakini kwa wale wasio na Cable iliwalazimu kununua antenna/converter zingine.

Mimi nimeandika experience yangu nilinunua Digital TV HD ready kwa sababu ya fainali za world cup wakati huo kule Japan na Korea sikununua aerial nyingine niliendelea kutumia ya zamani kwa kama miezi sita hivi. Kwa sababu ya michezo nikaongeza Sky digital box hivyo situmii kabisa aerial. Nimeweka kwenye stoo. Ukiangalia mfano wangu nimesema kuhusu UK kwa upande wa USA sifahamu.

Wakati natumia aerial ya zamani niliweza kubadili kutoka analogue kwa vipindi fulani fulani na kwenda digital tofauti ni picha tu. Lakini baada ya kuwa na sky box sina sababu ya kuhama hama kwa sababu wao wamecombine both into one. Hata ukienda kwenye store leo hakuna aerial ambazo zimeandikwa digital only or analogue. {Huenda zipo mimi sijui}

Tena kwa kuongeza hizi Digital TV & Boxes hivi sasa zinakuja na slots za kuweka kadi (more or similar to credit cards) hivyo itakuwa vigumu zaidi huko tunakokwenda kuangalia bila kulipa.
 
Mkuu

Unachokisema hapa wewe ni kuwa hao Wachina watakuwa wanamiliki 65% ya Digital TV Infrastructure ya Tanzania...na TBC wao watakuwa wanamiliki 35%.

Pia, kama nimekuelewa ni kuwa TBC wao watakuwa wanajihusisha na Contents. Wakati huo huo hawa Wachina kwa mujibu wa "dondoo" na pia wataruhusiwa kufanya biashara ya Contents wakishindana na TBC na other local companies.

Sasa mkuu hapo huoni kuwa tumeshafanya makosa...mimi naona Infrastructure ni muhimu zaidi...tungemiliki sisi hiyo 65% na Wachina 35%. Tutawezaje kuwa na sauti kwenye Contents wakati ambapo Infrastructure inamilikiwa na mtu mwingine.???
Ndugu yangu YEBO YEBO, hiyo kitu inayoitwa content isikie hivyo hivyo, Digita TV ni 24/7 for 365 days!. Hakuna hata TV station moja ya Tanzania inaweza kujaza muda huo, hivyo its fair Wachina wakijaza na mavitu yao. Mpaqka sasa Tanzania tuna TV Stations 10 tuu na hakuna hata moja yenye uwezo wa kujaza 50% ya content ndio maana matamthilia yote ni imported!. Sorry to day this, 'hatuna uwezo wa soap opera yoyote'. its a pitty but its a fact!. Sasa kama digital ni channel 100, tutaweza ili hali 10 tuu tunashindwa kujaza!.
 
Contents zitakuja tu Pasco, hilo sina wasiwasi nalo kabisa...unakumbuka zilipoanza FM Radio Station Tanzania...kulikuwa hakuna contents za nyumbani kabisa..ilikuwa America & Europe Imported contents even Caribbean unakumbuka Charanga Time na Charles Hilary on Radio One..?? Bila kusahau Bolingo kutoka Congo etc....huwezi kusema hali ni hivyo leo Tanzania. Vijana wa wanafyatua album kila kukicha na ushindani FM Radio Stations umeongezeka. Kwa mfano huo sioni sababu ya sisi kuwa na wasiwasi na contents ambazo ni Tanzania Made za kujaza Digital Stations 24/7 365 days a year...in time zitakuja tu.

Kinachonishangaza mimi ni kile kile kinachomshanga Mkuu Jasusi...kwa nini tumewapa hawa Wachina 65% ya Digital Infrastructure yetu??

Sababu kubwa ya mimi kuhofia huo mkataba ni kuwa huko mbeleni Wachina wakiamua kutoza gharama/fedha kubwa kutumia Miundombinu yao (wanaimiliki kwa 65%), maana yake ni kwamba Watanzania wenye vipaji na nia ya kutengeneza hizo tv contents watakuwa wameshawekewa kizingiti. Badala yake Wachina hao hao watakuwa na mitaji yao kupitia umiliki wao watakuja kuturushia contents zao wanazozitaka wao. Mwisho wa siku itakuwa sio TBC tena bali China TV.
 
Ndugu yangu YEBO YEBO, hiyo kitu inayoitwa content isikie hivyo hivyo, Digita TV ni 24/7 for 365 days!.

Sina uhakika na ukweli wa hii statement. Kwa uelewa wangu Digital TV haina uhusiano na namba ya channel wala muda kwa channels kuwa hewani. Unaweza kuwa na channel moja inayo air for 1 hour a day kwenye digital TV.

Hakuna hata TV station moja ya Tanzania inaweza kujaza muda huo, hivyo its fair Wachina wakijaza na mavitu yao. Mpaqka sasa Tanzania tuna TV Stations 10 tuu na hakuna hata moja yenye uwezo wa kujaza 50% ya content ndio maana matamthilia yote ni imported!. Sorry to day this, 'hatuna uwezo wa soap opera yoyote'. its a pitty but its a fact!. Sasa kama digital ni channel 100, tutaweza ili hali 10 tuu tunashindwa kujaza!.

Point ya hii switch from analog to digital ni hii: Kwenye analog system kila station inabidi kununua frequency (masafa) na ikishakuwa allotted for say ITV noone else can transmit kwenye hiyo frequency kwa sababu yataingiliana. Kwenye digital transmission matangazo yote (channel zote) zinachanganya kwenye one stream na kuwa transmitted digitally as one signal. Upande wa mtumiaje (receiver) unahitaji kifaa cha kutenganisha the signal kupata ITV, CTN, DTV n.k.

Kunakuwa na mtu anayetoa infrastructure za kufanya transmission (Star Media, IPP na Star TV wameanzisha kampuni ambayo nayo imeomba/pewa leseni ya kufanya hii biashara). Sasa ukiwa na content unaweza kwenda Star Media, au IPP/StarTV au mtu yeyote atakaye kuwa na leseni na mitambo ya kutoa huduma hii. In essence it makes it easy since you don't need to buy equipment nyingi kuwa na TV/Radio station. Afterall TV/Radio business ni business ya content and sio technology na minara. So content providers focus on providing content. Kwa kuwa sihitaji minara na madish ya gharama kuwa TV station, naweza kutengeneza content kwa gharama nafuu na kupeleka Star Media kurushiwa. Inategemewa content zitaongezeka kwa kuwa mtu mwenye idea ya TV show anaweza kuitengeneza bila kumtegemea Star TV au ITV au CTN kui-air.
 
Kunakuwa na mtu anayetoa infrastructure za kufanya transmission (Star Media, IPP na Star TV wameanzisha kampuni ambayo nayo imeomba/pewa leseni ya kufanya hii biashara). Sasa ukiwa na content unaweza kwenda Star Media, au IPP/StarTV au mtu yeyote atakaye kuwa na leseni na mitambo ya kutoa huduma hii.

Sasa hapa umefafanua hivi...then

Inategemewa content zitaongezeka kwa kuwa mtu mwenye idea ya TV show anaweza kuitengeneza bila kumtegemea Star TV au ITV au CTN kui-air.

Ikiwa kama Taifa letu halina Infrastructure za kufanya transmission (kwa sababu Wachina waimiliki kwa 65%) kuna uhakika gani kuwa contents za TBC zitarushwa kwenye hiyo mitambo ya Wachina na sio Wachina waje na Contents zao? na pia Je itarushwa kwa gharama nafuu?

Watanzania wengine wenye kipaji na uwezo wa kutengeneza Contents kwa gharama nafuu, wataweza vipi kumudu vizingiti vya 1; gharama na 2; vigezo vingine vitakavyowekwa na hao wamiliki?

Hey, inaonekana unazungumza kinadharia zaidi kuliko hali halisi. Katika mazingira "perfect" hilo unalosema linawezekana, lakini tukiangalia mifano ya mikataba yetu na utekelezaji wake Tanzania....kuna dalili kuwa tumejifunza lolote?? Sidhani...

TBC ilitakiwa imili 100% au kama ingeshindwa kabisa basi wao Wamiliki 65% na Wachina 35%.
 
[/COLOR][/FONT]

Itizame hivi. Sasa hivi nikiwa na idea ya show, nina options mbili:

1. Nianzishe TV/Radio station (ninunue mitambo, niombe leseni ya masafa, wafanyakazi, na gharama zihusiano.

2. Nitengeneze show, kwa gharama yangu, niipeleke TBC au ITV n.k, kuwauzia idea wanisaidie kui-air (nadhani ndio business model ya kina Benchmark na Maisha Plus)au nitengeneze pilot kwa bei rahisi (camera za kawaida) halafu niwaconvince wenye TV station wanibackup kwa budget n.k kutengeneza show nzima na ku-air the product.

Kuhusu swala la TBC, ambayo kwenye mfumo mpya watakuwa wanafanya biashara ya content, kutumia infrastructure ya star media, kinadharia they have no obligation to. Kama ITV/StarTV au mtu mwingine yoyote mwenye biashara ya transmission atawapa a better deal wanaweza kwenda huko. Mchina anaweza kurusha content zake kwenye hiyo infrastructure pia, akiwa na leseni ya content. Kwa hiyo TBC, mchina, na mimi na wewe tutaweza kupitisha content zetu humo humo kama station/channel tofauti.

Kuhusu gharama...kinadharia zinabidi ziwe nafuu zaidi. Hali ilivyo kwa sasa, kizingiti kikubwa sana kwa a creative type mwenye idea lukuki za TV show ni teknolojia na mitambo. Huoni inakuwa rahisi kwa huyo mtu kutengeneza content zake bila kujali mambo ya madish, transceiver na spare part zake? Pia, kinadharia, vizingiti vya hao watu wa trasmission vinatakiwe viwe ni vile tu vilivyokubaliwa na TCRA. Kwa sababu kama kila mtu anayefanya biashara ya content ataona ni bora kuwa na mitambo yake, then hamna maaana ya hii switch. Kama nilivyosema hapa ITV na Star TV wameungana kufanya hii biashara, kwa hiyo content zao zitapitia humo. Kwa haraka haraka utaona faida kwa wote wawili, maana wataunganisha technical department and hence kupunguza gharama, na hawata hutaji kila mmoja kuwa na masafa yake, which, masafa ambayo siyo tu ni ya gharama, lakini yanakwisha. Halafu watafocus kwenye kutengeneza content za maana na competitive. Na pia wana chanzo kingine cha mapato kwa kuruhusu watu wengine kutumia miundombinu yao. Ubaya ni kwamba mtu wa nje ya huu muungano itamwia vigumu kutumia huduma zao za transmission, while at the same time expected to compete with them on content. Again hapo TCRA itabdi wafanye kazi.

A lot of this is "in theory" or logic. Lakini kama ulivyosema kwenye Tanzania yetu anything is possible.
 
samahani wadau hii digital switch by 2015 itabidi tubadilishe vitu gani kati ya receiver,dish na televion? naomba yeyote mwenye ufahamu anijulishe
 
samahani wadau hii digital switch by 2015 itabidi tubadilishe vitu gani kati ya receiver,dish na televion? naomba yeyote mwenye ufahamu anijulishe
TV nyingi zinazotengenezwa sasa huhitaji kuweka chochote lakini kwa tv za zamani 3 to 5 yrs unahitaji king'amuzi cha kubadilisha digital signal to analogue mfano ni kama king'amuzi cha DSTV
 
Nimemsikia Tido akiuelezea huu mradi katika kipindi cha Pongezi za mwaka mpya kilicho rushwa na Radio yao na aliielezea kuwa unategemewa kuanza majaribio katika mwezi huu wa January kwa Mkoa wa Dar kwa kuanzia na wale wanaohitaji watatakiwa kuwa na Decoder na alisema kwa kuanzia itakuwa na channel zisizopungua 40 ila alifafanua na kusema kuwa inategemewa kuwa na channel kama 200 hivi ambazo zitalipiwa kwa bei nafuu. ukilinganisha na DSTV.
 
naomba kujuzwa kidogo hivi ikishakuwa digital inamaana atutatumia tena antena za kawaida watasaplay decoder au sijaelewa jamani

Mkuu Digital TV Broadcasting ( DVB_T) ikianza nchini uzoefu unaonyesha kutakuwa na phase mbili

Phase ya kwanza inaitwa SIMULICAST

Katika hii phase both analogue na digital vita co exist kwa maana kama una analogue TV Receiver antena yako ya kawaida ( wengi huita CHADEMA) haitaweza kupokea matangazo ammbayo yako digitally encoded kwa hiyo itabidi uendelee kupata Analogue transmitted signal, Ili upate Digitally transmitted sigal kwa kutumia Analogue receiver yako inabidi uwe na kifaa kinachoitwa Set Top Box ( STB) ambacho kazi yake ni ku decode digital encoded signal ili ziweze kutambulika na analogue tv receiver yako. Kama hutaki habari za STB inabidi ununue TV Mpya ( Digital TV receiver) hapa hutahitaji STB ni wewe na kia antenna chako unakula DVT_T signal kama kawa!

kwa hiyo katika phase ya kwanza ( Katika nchi nyingi ambazo zime adapt huu mfumo) hulazimiki kuwa na Digital receiver wala STB unless unataka ku enjoy DVB_T

Phase ya pili ni DIGITAL SWITCHOVER

Katika hii phase hakuna mtu atayeruhusiwa kurusha matangazo ya Analogue so ili uweze kuona tv ni Lazima aidha uwe na STB au Ununue Digital TV
 
Back
Top Bottom