Mradi Kigamboni: Hakuna Fidia

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,006
1,254
SERIKALI imesema haitowalipa fidia wakazi wa eneo la Mradi wa Mji Mpya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Tamko hilo, lilitolewa bungeni jana na Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye, wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Kigamboni Dk Faustine Ndungulile (CCM), aliyetaka kujua lini Serikali itaanza ujenzi rasmi wa mji huo wa Kigamboni na kama iko tayari kuwalipa wakazi wake fidia.
Akijibu swali hilo, Ole Medeye, alisema haitowalipa wakazi hao fidia kwa kuwa haikuwazuia kuendelea na shughuli zao za kawaida isipokuwa tamko la Serikali la Oktoba mwaka 2008, lilisitisha maendeleo ya ardhi wanayomiliki ikiwemo ujenzi wa majengo mapya ya kudumu.
Alisema tamko hilo lilitolewa kwa mujibu wa Sheria ya Mipango miji ambayo inahusu kusitisha maendelezo ndani ya maeneo husika kwa muda wa miaka miwili ambapo alisema tamko hilo halikumzuia mmiliki yeyote wa mali Kigamboni kuuza mali zao katika kipindi hicho cha mpango.
“Napenda kulitaarifu Bunge hili tukufu kuwa amri ya kusitisha ujenzi ilikoma Oktoba mwaka jana na baada ya hapo hakukuwapo na pingamizi la kisheria la kuendeleza maeneo husika kuanzia wakati huo kwa kuzingatia matumizi ya ardhi yaliyoanishwa kwenye mpango huo wa mji mpya,” alisema.
Alisema kwa kuzingatia kanuni, Februari mwaka huu Wizara ya Ardhi ilitoa tamko lililowakumbusha wamiliki ardhi katika eneo la mji huo mpya kuwa hawana budi kuomba vibali vya ujenzi kabla ya kufanya ujenzi wowote.
Alisema vibali hivyo ni ili ujenzi huo uzingatie matumizi ya ardhi yaliyoainishwa katika rasimu ya Mpango Kabambe wa mji mpya Kigamboni kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria ya Mipango Miji.
Kuhusu kipengele kuwa wananchi wa Kigamboni nao watanufaika na mradi huo, Ole Medeye, alisema watanufaika kutokana na ujenzi wa mji huo utawapatia fursa ya makazi bora na ajira wakati wa ujenzi wa mji huo.
Kuna mtu ataulizia....source?
 
Wameshauza na kugawana zamaaaani...!!!!!!! Fidia itoke wapi kama wananchi hawataki kulipa kodi?
 
jamaa walioko kule akiri hawana wanauzwa huku wanajiona kushinda kupiga bao tu..wacha wakome.
 
Mnashangaa nin?
Dar es salaam ndivyo walivyoumbwa, swali lenyewe mpaka kufikia kuulizwa bungeni limegharimu vikao vingi na vya muda mrefu vya usiku na mchana huku hela za wakaazi wa eneo hilo la mradi zikiliwa kama michango ili kuifanikisha kamati hiyo kukutana na eti kufanikisha kile wakiitacho kumualika mbunge vikaoni.
 
Back
Top Bottom